Kama ni kweli maneno hayo yamesemwa na Rais Samia; kama yalivyo wasilishwa na mtangazaji Salim Kikeke: Maneno yenyewe ni haya: "Nalifanyia kazi jambo hili. Binafsi kutoka moyoni mwangu nataka taifa lenye umoja."
Salim kayaandika maneno hayo yakiwa sehemu ya maongezi yake kwa njia ya simu na Rais Samia.
Kwanza niseme, sina sababu za kumtilia mashaka sana Salim Kikeke kuhusu maongezi yake na rais, pamoja na kwamba mtu huyo simfahamu vyema; ingawa kagusia pia katazo la kuitoa habari hiyo na nyinginezo kwenye maongezi yao; kaamua kughaili katazo hilo na kuitoa hii kama dokezo la nia ya rais.
Lakini hayo maongezi yao tuyaweke pembeni, tujaribu kwanza kushughulika na haya maneno machache
Kinachojulikana ni kuwa haya maneno yanahusiana na yanayoendelea kwenye mitandao, ambayo rais kaeleza anayo taarifa juu yake...
Lakini haikufumbuliwa wazi ni "Jambo" gani linalozungumziwa moja kwa moja. Wewe unajuwa ni jambo gani "Analolifanyia Kazi Rais"?
Kwa kuwa kaongezea maneno kulihusu jambo hilo, kwa kusema "Binafsi kutoka moyoni mwangu nataka taifa lenye umoja"; ni wazi kuwa ni jambo linalohusu uchaguzi mkuu ujao.
Hadharani tunasikia CCM wakijiapiza kuwa uchaguzi ni lazima uendelee kama ulivyo pangwa. Lakini rais sasa anadokeza kuna jambo analifanyia kazi, ili kulinda umoja wa taifa.
Maoni yangu ni kwamba NORNOE imekolea mioyoni mwa watu wote; hata wale ambao walikuwa wannaapa kutotikiswa na dhoruba hili.
Mungu Ibariki Tanzania.