Haya ndo maneno ya Jakaya Mrisho Kikwete Dec 2005 mpaka sasa hakuna cha maana mpaka uchumi umelegalega.
Mtu anaweza kujiuliza je Jakaya Mrisho kikwete kajikwaa wapi?
Uchumi UnaopaaMheshimiwa Spika:
Baada ya mafanikio ya Awamu ya Tatu, haitarajiwi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne italegeza kamba na kupuuza misingi iliyotuletea mafanikio tunayojivunia.
Najua mengi yamesemwa na watu wanaodai wanamfahamu Jakaya Mrisho Kikwete na jinsi atakavyolegeza mambo. Napenda kuwahakikishieni kuwa watu hao wamepotea sana.
Wakati wa kampeni wapo baadhi ya wapinzani waliothubutu, kwa kukosa shukrani, kusema ati Serikali ya Awamu ya Tatu ilikuwa inatekeleza sera zinazobuniwa Washington.
Serikali ya Awamu ya Nne haitaogopa kubuni na kutekeleza sera na mikakati ya maslahi kwa ukuaji wa uchumi na maisha bora kwa kila Mtanzania ati kwa vile zinaungwa mkono au kufadhiliwa na nchi tajiri na mashirika ya fedha ya kimataifa.Hatutafanya lolote lisilo na maslahi kwa taifa letu kwa kuwaogopa au kutaka kujipendekeza kwa wakubwa hao. Lakini vile vile hatutaacha kufanya lolote la maslahi kwa taifa na Watanzania kwa vile tu linaenda sambamba na ushauri wa mashirika ya fedha ya kimataifa. Hatutafanya maamuzi kwa kutaka kupendwa; lakini tutafanya kila maamuzi kwa kigezo cha msingi cha maendeleo na maslahi ya taifa.
Mheshimiwa Spika:
Mbali ya kusukumwa na hoja ya kukuza uchumi haraka ili kupiga vita umaskini, tunasukumwa pia na ukweli wa nguvu za utandawazi na ushindani mkubwa katika masoko ya kanda na ya kimataifa. Hivyo basi, sote tuunganishe nguvu zetu ili tuongeze uzalishaji, tuongeze uwekezaji, tuongeze mauzo nje, tuongeze ubora wa mazao na huduma zetu na tuongeze kasi ya ukuaji wa uchumi wetu ili upae.
Hakuna kurudi nyuma. Kasi mpya inayozungumziwa ni ya kusonga mbele na siyo kuserereka na kurudi nyuma kwa kasi.
Update: source Jakaya Mrisho Kikwete-Jakaya Kikwete Speech,Jakaya kikwete news, Jakaya kikwete bringing world to Tanzania,Jakaya activites in Tanzania