NALETA UCHUMI UNAOPAA: Jakaya Mrisho Kikwete

Hotuba hii alikuwa hayanunuliwa suti, nakutolewa out US,sasa hivi naamini inaweza kuikana kuwa sio yake,anyway kama binadamu tukubali ana mapungufu yake japo yamezidi,ndo hivyo maumivu hadi 2015,tumwombee Mungu amteremshie hekima kama ya Suleimani huenda nasi TZ tukala bata katika regime yake,otherwise God knowa we are in trouble
Haya ndo maneno ya Jakaya Mrisho Kikwete Dec 2005 mpaka sasa hakuna cha maana mpaka uchumi umelegalega.

Mtu anaweza kujiuliza je Jakaya Mrisho kikwete kajikwaa wapi?


Uchumi Unaopaa
Mheshimiwa Spika:
Baada ya mafanikio ya Awamu ya Tatu, haitarajiwi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne italegeza kamba na kupuuza misingi iliyotuletea mafanikio tunayojivunia. Najua mengi yamesemwa na watu wanaodai wanamfahamu Jakaya Mrisho Kikwete na jinsi atakavyolegeza mambo. Napenda kuwahakikishieni kuwa watu hao wamepotea sana.

Wakati wa kampeni wapo baadhi ya wapinzani waliothubutu, kwa kukosa shukrani, kusema ati Serikali ya Awamu ya Tatu ilikuwa inatekeleza sera zinazobuniwa Washington. Serikali ya Awamu ya Nne haitaogopa kubuni na kutekeleza sera na mikakati ya maslahi kwa ukuaji wa uchumi na maisha bora kwa kila Mtanzania ati kwa vile zinaungwa mkono au kufadhiliwa na nchi tajiri na mashirika ya fedha ya kimataifa.Hatutafanya lolote lisilo na maslahi kwa taifa letu kwa kuwaogopa au kutaka kujipendekeza kwa wakubwa hao. Lakini vile vile hatutaacha kufanya lolote la maslahi kwa taifa na Watanzania kwa vile tu linaenda sambamba na ushauri wa mashirika ya fedha ya kimataifa. Hatutafanya maamuzi kwa kutaka kupendwa; lakini tutafanya kila maamuzi kwa kigezo cha msingi cha maendeleo na maslahi ya taifa.

Mheshimiwa Spika:
Mbali ya kusukumwa na hoja ya kukuza uchumi haraka ili kupiga vita umaskini, tunasukumwa pia na ukweli wa nguvu za utandawazi na ushindani mkubwa katika masoko ya kanda na ya kimataifa. Hivyo basi, sote tuunganishe nguvu zetu ili tuongeze uzalishaji, tuongeze uwekezaji, tuongeze mauzo nje, tuongeze ubora wa mazao na huduma zetu na tuongeze kasi ya ukuaji wa uchumi wetu ili upae. Hakuna kurudi nyuma. Kasi mpya inayozungumziwa ni ya kusonga mbele na siyo kuserereka na kurudi nyuma kwa kasi.


Update: source Jakaya Mrisho Kikwete-Jakaya Kikwete Speech,Jakaya kikwete news, Jakaya kikwete bringing world to Tanzania,Jakaya activites in Tanzania
 
Uwezo wa kuongoza anao ila sema kazidiwa na ushkaji,CV yake inaonyesha kashika nyadhifa nyingi nyeti,tukubali kuwa aliingia na stail mbaya,ya kuwakumbatia wanamtandao ambao wamekuwa full kujiachia a.k.a utawafanya nini? inahitajika neema ya Mungu kutunusuru kwani sasa hivi wanamtandao wanakwapua kwa spidi ya ajabu coz ni last chance.
NI kwamba JK hana uwezo wa uongozi. Na hili jambo akina Mangula waliliona mapema kabisa na wakafanya atempt ya kumnyima form ya kugombea urais huyu. Mwinyi ndo aliyetupeleka hapa tulipo. Watanzania tuache unafiki. Mwinyi ni tatizo hapa. Maana yeye ndiye aliyemlazimisha Mangula ampe JK form ya kugombea Urais. Hizi ni habari nilizozipata toka ndani kabisa ya system.
 
Ukimuuliza atakuambia hiyo spichi aliandika Januari Maropes, yeye (Jakaya) alichofanya ni kusoma tu.
 
NI kwamba JK hana uwezo wa uongozi. Na hili jambo akina Mangula waliliona mapema kabisa na wakafanya atempt ya kumnyima form ya kugombea urais huyu. Mwinyi ndo aliyetupeleka hapa tulipo. Watanzania tuache unafiki. Mwinyi ni tatizo hapa. Maana yeye ndiye aliyemlazimisha Mangula ampe JK form ya kugombea Urais. Hizi ni habari nilizozipata toka ndani kabisa ya system.

Hii sasa ni kumtafuta mchawi, si tulimchagua wenyewe tena kwa asilimia 80 plus, Raisi handsome! Tusimlaumu Mwinyi.
 
Inasikitisha sana kwa Mkuu wa Nchi kukosa uelekeo na uchumi wa Taifa letu kuzidi kudidimia kwani hata jana alisikika akisema kuwa kila ahadi aliyotoa itatekelezwa kwani ahadi zote ziko kwenye maandishi.

Uchumi unaopaa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom