Unbounced
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 345
- 435
"Habari za sahizi wakuu natumai mpo vema.
Mimi ni kijana wa kiume waumri wa 26
Nilianza mahusiano na binti mmoja kutoka tangu miezi zaidi ya sita sasa.Hatujawahi kuwa na ugomvi pia malengo yetu ni kuja kuwa mke na mume ikimpendeza mungu.
Huyu binti nilipata kumjua kupitia familia ya kakaangu na ni Mtu wao wa karibu sana na amekua kama ndugu kwao.
Tatizo ni kwamba familia ya kakaangu(yani kaka na mkewe) walikuwa na ushirikiano wa kibiashara na binti yule ,kama mjuavyo biashara ina changamoto zake kuna hasara ,faida pia kuna wakati mwingine biashara huwa ngumu.
Ilitokea kwamba yule binti amepata changamoto ya kifamilia kitu kilichopelekea kuchelewesha kurudisha faida kwa kaka na mkewe kitu kilichosababisha kaka na mkewe kupoteza imani kwa yule binti ambaye alishakuwa kama ndugu .walimdai pesa zile pasipo na ustaarabu wala staha wakimwita majina ya kudhalilisha kama mtu ambaye hawakuwahi kuwa na ukaribu nae.
Yule binti alijitahidi kukopa pesa mahali kwingine ili aepukane na mgogoro huo ulioshamiri.Japokuwa kuna kias kidogo bado anadaiwa kama asilimia tano hivi .
Kutokana na hili kakaangu amekuwa akinambia niachane na Huyo binti kitu ambacho siafikiani nacho mana ni kweli alipitia changamoto ambazo kaka hakutaka kuzielewa wala kuwa na subira kupata pesa yake .Binafsi nilihisi kutokana na aibu ya kumdhalilisha yule binti kwa maneno ndo mana ananisistiza kutoendelea nae akihofia hatutakua na mahusiano mazuri na familia yake baada ya ndoa kutokana na walivomtendea yule binti.
Wakuu naombeni maneno yenu ya hekima ili nibaki salama nisielemee upande mmoja pia .
Asanteni japo kwa kupitia Uzi huu wenye majonzi kwangu.