Habari za weekend wadau?
Nilikuwa naomba ushauri ,miezi kadhaa iliyopita nilikutana na binti ambaye nilitokea kuzoeana nae kidogo,baada ya muda kidogo kupita nilianza kutamani awe mtu wangu.
Basi nikaongeza juhudi ya kumfanya awe karibu nami na aniamini,nilianza kugharamika kiaina ,nilimnunulia zawadi mbali mbali,nilimtoa out pia Mara kadhaa,baada ya kuona kwamba ameanza kuniamini nikaamua nimwambie kilichomo ndani ya moyo wangu,but akachomoa kwa kusema kwamba ana mtu wake,niliendelea kukomaa kwa miezi miwili ila bado aliendelea na msimamo wake
Aisee nikaamua kukata tamaa,nikafuta namba ake lakini yeye aliendelea kunitumia text na kunipigia ninapokuwa kimya muda mrefu,nilijaribu kutongoza tena akachomoa aisee mpaka Leo hajawahi kunikubalia lakini simu ananipigia na hata sms ananitumia kama kawa ninapokuwa kimya .
Nilikuwa naomba ushauri ,je nivute subira au nimpotezee mazima?,nampenda sana ila hakuna namna,bint mwenyewe inaonekana ni Bright brain.