NAKUVULIA KOFIA KAKA YETU MKUBWA

NAKUVULIA KOFIA KAKA YETU MKUBWA

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
5,760
Reaction score
7,487
1.KUOLEWA KWA MDOGO WETU WA MWISHO.
Kaka yetu kwa sasa ni mzee anakaribia miaka 90 na anaishi nje ya nchi kwa sasa.
Ni mtu ambae sijawahi kuona jinsi alivyo na heshima,adabu,nidhamu,utulivu na utu wa ajabu kabisa.Kila siku namuombea kwa Mola ampe maisha marefu.

Kaka alivyoondoka,mimi tayari nilikuwa nisharudi tz na nimeishaoa,na kaka zangu na dada zangu wengine nao wote wakahama,mie nilirudi tx na kabla sijahamia mwanza,nikiishi dar nikifanya kazi.
Mdogo wetu wa kike,nimwite Amina japo sio jina lake,alikuwa anasoma nairobi university,akisoma sheria na msimamizi wake mkuu,nilikuwa mimi.

Sasa mwaka mmoja nilipigiwa simu na kaka yangu kuniatifu kuwa Amina anataka kuolewa hivyo kaka akaniambia mimi ndio nishughulikie suala hilo kwa niaba ya ukoo wetu.

Nikamtafuta Amina kwa simu na tukakubaliana aje dar kwanza.Akaja na akanieleza kuhusu nia yake hiyo ya kuolewa na hapo niliwaita wake zangu wote 2 ili washiriki kwenye jambo hili kubwa.

Na wakati huo dada yetu alikuwa kabakisha miezi 6 kumaliza masomo yake.Itaendelea.............
 
Haya tuendelee sasa.Amina alituarifu kuwa kapata mchumba ambae ni suriyama wa kihindi na kikikuyu,kwamba mchumba wake ni halfcaste wa kihindi na kikikuyu,suriyama ni kiswahili sanifu cha neno chotara.Huyo mchumba wa mdogo wetu kwa jina namwita pravin ambalo sio jina lake amesomea civil engineering ila anafanya biashara ya duka.

Basi tukakubaliana kuwa sasa tupo tayari kupokea posa.Nilipanga tarehe ya kupokea posa na siku ilipofika wageni walifika ambapo pravin alikuja na baba na mama yake,mjomba wake na dada yake mmoja.Walifika na Amina alikuwa kaisha waandalia hoteli ya kufikia,walikuja na mabasi yatokayo nairobi to dar.Amina aliwapokea akisaidiana na dereva wangu mmoja na wake zangu wote 2.Usiku tuliwakaribisha nyumbani kwa chakula cha usiku na maongezi mengine.Amina alishanipa background information ya huo ukoo wote,kwamba ni wakatoliki hivyo kwangu ilikuwa rahisi sana kuandaa chakula na vinywaji.
Na kabla nilishaongea na kaka mkubwa kuhusu mahari,ambapo kaka alisema mahari iwe milioni 10.Nilimwambia Amina kuhusu hiyo mahari,lakini nikamuona kama ana hofu kidogo,ndipo akaniomba nipunguze kwani kiwango hicho ni kikubwa na akaongeza kusema huyo mchumba wake anatoka kwenye familia ya kawaida tu na bado hajajipata.
Nilimwambia mahari haipungui.
Sasa huyo mdogo wangu ni mrembo kwelikweli,ni mchotara maana na sisi tumechanganyika,nywele ndefu mpaka mgongoni,body yake compact na kajaza fulani hivi yaani ni amazingly beautiful.

Haya basi wageni wakafika,tukala na tukanywa na mimi nilialika ndugu na rafiki kuhudhuria kihafla hicho kidogo.Watu walifurahi na tukachanganyika na wageni na mambo yalikuwa murua kwelikweli.

Muda ukafika nikaipokea posa na iliambatana na dola 300 nikaisoma na tukakubaliana majibu niwape kesho mchana saa 8,maana na wao pia waliomba tuwajibu mapema.Kesho yake saa 8 walifika na nikawapa majibu kuwa tumelikubali ombi lao na mahari ni milioni 10 za kitanzania.Itaendelea........
 
Haya sasa nimalizie hii habari masna leo nipo free kabisa.
Baada ya mie kuwaeleza kiwango cha cha mahari,pravin na wazazi wake waliomba waende chemba kujadiliana na tuliwaruhusu,Amina aliwapeleka kwenye chumba kimoja walijadiliana kwa dk 20 na wakarudi kutupa majibu.
Baba yake Pravin aliomba kupunguziwa kwani alisema kuwa hawatoki kwenye familia yenye kipato kikubwa na kwamba mtoto wao pravin ndio kaanza biashara na mtaji wake ni mdogo.Hivyo wao walisema watatoa milioni 6 na watanguliza mil 3 kwanza na 3 zingine watatoa baada ya mwaka mmoja.

Ikabidi nami na wake zangu tuende chemba kujadiliana,na nilimpigia simu kaka mkubwa ambae alishauri tupunguze milioni 2 na tupokee kima chochote kitakachotolewa na tupange tarehe ya harusi.

Tukarejea kikaoni na tukawaatifu kuwa tumepunguza mil 2 hivyo mahari itakuwa mil 8.Wakakubali na wakatanguliza mil 3.Tukazipokea na tukapanga harusi kufanyika baada ya miezi 6 na tukakubaliana.Basi tukaendelea na sherehe hapo nyumbani,kula,kunywa na kuongea.
Tuliagana na wageni baada ya saa 3 hivi na wakatuambia kuwa watasafiri kurejea kenya baada ya siku 2.

Wageni walipoondoka,Amina alikuwa na wiki moja ya kupumzika kabla ya kurejea masomoni,hivyo nilimwita ili kujua mahitaji yake,akiwa shuleni,maana tulikuwa tunamlioia kila kitu.Akanipa hesabu yake,nikaipitia na nikaiona ipo sawa ila kimoyomoyo nikasema nitamuongeza milioni 3 extra.

Amina alirudi nairobi na akamaliza masomo yake,na akarejea dar na baada ya wiki moja alienda nje ya nchi kusalimia ndugu na mahsusi kumshukuru kaka mkubwa kwa malezi mazuri aliyompa

Ilipobakia mwezi mmoja kabla ya harusi akarejea dar,kwa maandalizi ya mwishomwisho ya harusi yake.

Huku nyuma yeye alivyoenda nje,familia ilijadiliana juu ya harusi ya mdogo wetu na chini ya usimamizi wa kaka mkubwa na tulikubaliana mambo yafuatayo:
1.hakutakuwa na kadi za kuomba michango bali harusi hiyo igharimiwe kila kitu na familia.
2.Tuliozaliwa tumbo moja kila mmoja achangie milioni 2.
3.Harusi itafanyika kwenye gereji ya kaka,kwa wale mliosoma ile stori yangu ya jinsi nilivyokutana na singo maza wa kiarabu,mtakumbuka kuwa huyu ni yule kaka yangu ambae alikuwa na malori,maduka na vituo vya mafuta.
4.wake zangu wote ndio walikuwa waandalizi wa kila kitu huku pesa zote kutoka kwa ndugu,marafiki na akiba ya familia nilikuwa napokea mimi.
4.wageni wote watafikia kwenye nyumba ya kaka alijenga mikocheni na hatujaipangisha ila ipo chini ya usimamizi wangu na kuna ndugu 2 wanakaa kuilinda na kuifanyia usafi
5.Tuliandaa orodha ya marafiki 50 ambao watapewa mwaliko kuhudhuria sherehe ya harusi.
6.Tukaunda kamati ambayo ndiyo iliyoandaa kila kitu,chini ya usimamizi wa rafiki yangu mmoja ambae ni mtu mkubwa serikalini ambae sitamtaja jina.
Kamati ilipanga ndoa itafungwa kanisa la katoliki oysterbay ambapo ndipo ndoa ilipoandikishwa na taratibu zote za kikatoliki kuhusu ndoa zilifuatwa,na sikutaka kuelezea jambo kwani ingerefusha stori bila sababu,kaeni mkijua kuwa bwana na bibi harusi walifanya taratibu zote zinazotakiwa.
Kamati ilipanga mambo yafuatayo:
a)ndoa itafungwa oysterbay hivyo usafiri wa wageni wote jwenda kanisani na kurudi nyumbani
b)malazi ya wageni,chakula na usafiri wao
c)kuanda eneo la sherehe ya harusi,mapambo,chakula,vinywaji,usafiri,zawadi.
Siku ilipofika ndoa ilifungwa na sherehe ilifanyika.
Mimi na wake zangu 2 tuliongoza safari ya kumsindikiza Amina Nairobi kwa mumewe,na nilifanya maandalizi yote ya kufikia na tulindoka na gari 3 kuelekea Nairobi.
Tulifika na tulipokelewa vizuri tu,familia ya shemeji haikuwa yenye kipato kikubwa ni ya wastani tu na hata duka la shemeji yetu sio kubwa hivyo.
Niliongea na shemeji yangu in private kujua mipango yake na kuhusu mkewe na akanieleza,shida kubwa ni mtaji ambao kwa makisio yangu ni dola
laki moja mjue hii ni stori ya miaka zaidi ya 10.Niliongea na Amina kujua mipango yake na akaniambia yeye ataomba kazi na pia atashirikiana na mumewe.

Basi tukarejea home kila mtu akafata shughuli zake bami nilirepoti kila kitu kwa kaka mkubwa kuhusu Amina na Pravin.
Baada ya mwezi mmoja,kaka mkubwa alinipigia simu kwamba anatuma dola laki moja na nusu kwenye akaunti yangu na atanielekeza matumizi yake.

Kweli kaka alituma hizo pesa lakini hakunipa maelekezo ya hiyo pesa.

Ilipopita mwezi kaka mkubwa aliniambia,niende nairobi kuongea na pravin na mkewe,kwamba ameamua kuwapa dola laki na nusu kama mtaji wao.Nikaenda,niliwakuta wapo salama na wakiushi vizuri na kwa kushirikiana.Niliwambia kuwa nimekuja kuwaletea mtaji kwa maelekezo ya kaka mkubwa.
Pravin na Amina walishukuru sana na walinipa plan kuhusu kuwekeza hizo fedha,nami nikawatakia kila la kheri,niliwawekea fedha hizo kwenye akaunti na nikarejea dar.

Hivi sasa Pravin na Amina wanaishi Dubai wakifanya biashara za wholesale,wakitoa vitu china na kusupply kenya ambapo wamefungua duka kubwa na magodown ya kuhifadhia mali.

Nakuvulia kofia kaka mkubwa kwa kutoa pesa kumpa shemeji,sio rahisi kwa dunia hii mtu kumpa mtaji shemeji yake.Mungu akupe maisha marefu kaka.
Mwisho.
 
Mnapangaje ndoa kikeni na sio sent off
 
Mnapangaje ndoa kikeni na sio sent off
Tuliamua kufanya hivyo,na ni kwa vile sikutaka kuandika mengi lakini kwenye harusi ile hatukuweka mc,wala hapakuwa na muziki,kulikuwa na watu wa kukaribisha wageni,na hata zawadi palitengwa eneo la zawadi,kila mtu alipeleka zawadi kwa wakati wake na wala hapakuwa na hotuba yoyote iliyotolewa
 
Back
Top Bottom