Nakusudia kumshtaki baba yangu

Pole Sana,inasikitisha
Wazee wengine Kama wamelogwa vile yani
 
Na hapo si mzee tu kuna wadogo zake pia wangeweza kumgeuka pia.
Hapa alibugi.
Unapokuwa na familia unaacha kila kitu na ndugu wote unashirikiana na mkeo kutengeneza maisha ya watoto.
Kosa pia alifanya hapo. Hii ya kuacha hati kwingine na yeye yupo eneo tofauti ni mbaya sana.
 
Sijaona kosa la baba’ko hapo, umeandika mengi ila ukahitimisha kinachokuuma ni 16m tu... itakuwa umeanza kufirisika hivyo unatafuta wa kumbebesha lawama.

Tafuta hela nyingi bwashee, ukizipata tafuta zingine... mwache mzee ale mafao usisahau keshakwambia umlipe gharama za matunzo.

Cheers 🥂
 
Na hapo si mzee tu kuna wadogo zake pia wangeweza kumgeuka pia.
Hapa alibugi.
Unapokuwa na familia unaacha kila kitu na ndugu wote unashirikiana na mkeo kutengeneza maisha ya watoto.
Migogoro ya kifamilia ni mizito sana hasa mzee akiyumba kiuchumi tofauti na alivyokuwa awali lazima uadui utokee kati ya watoto ama mke.
 
Pole sana mkuu, huyu mzee alikutunza vyema wakati hajaanza kufanya huo unaoita upumbavu au alikuwa hivyo tangu zamani?

Je ana mgogoro na mkewe yaani mama yako.?

Umewahi kufuatilia japo kujua chanzo cha yeye kurudi nyuma kiuchumi ni nini.?
Mkuu mzee wangu sitaki kumsema uongo alinitunza vema sana tatzo la uhuni na alipoanza kupata pesa alibadilika sana na hapo ndipo uhuni ulipozidi mpaka mda huu tunafikishana huku na sijui kakamatwaje kwa sasa kawa ni zaidi ya MPUMBAVU ukoo mzima unamshangaa. Yaani Kama nisingesimama kwenye familia basi Hawa madogo wangekuwa wanajiuza na wengine machokoraa hakukuwa na msaada mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ni madhara ya kumtelekeza baba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemtelekezaje mkuu? Mpaka nilimpa 28m kuboost mtaji wa miradi yake, 30m za kumalizia malipo ya nyumba yangu, 12m za viwanja zote kala mkuu yaani angekuwa sio baba ningekuwa nshamramba risasi.

Acha baba, ulishawahi kumlamba risasi hata njiwa.?
 
Ushauri mwingine tuko pamoja, la kumshitaki mzee aachane nalo kabisa.
Inauma lakini lazima asamehe, lazima. Na avumilie hayo maamuzi ya mzee ya kuwa na mwanamke mwingine, si vyema kwenda deep.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Wengi wape" ila si mara zote huyo ni mzee wako hata kama ana mapungufu ya wazi usiungane na ukoo wako kumsakama kwa ujinga wake na uhuni jaribu kutafuta muda ambao unaweza kuonekana ni muda wa kipuuzi omba appointment naye kisha kirafiki anza kuongea naye ukiamini ni mpumbavu, yaani vaa uhusika kama vile wewe ndiye baba yake.

Jaribu kumuuliza anaona hatima gani na maisha yake pamoja na familia ameamua iwe katika njia hiyo au kuna kitu kipo ndani yake. Huwenda mzee wetu amepata mhuni ambaye amevuruga ufahamu wake na haelewi chanya wala hasi. Usimhukumu kuwa ni mpumbavu wala mjinga ila tafuta chanzo cha upumbavu wake huo ambao amekuwa nao hivi karibuni najua upumbavu wake huwenda ni msukumo kutoka kwa yule ambaye anakaa naye sasa.

Ulipambana na kupata zaidi ya milioni 10 na viwanja ukanunua huku wadogo zako wa5 ukikomaa nao na tena wako private schools. Huoni kama wewe ni mtu ambaye unaweza kumudu mambo mazito na kuyatatua? Wewe inatakiwa mzee wako ndiye akuone mpumbavu kwa yote ambayo kakutendea na umekaa kimya. Hebu onesha mzee kuwa amezaa dume lisilotetereka katika magumu kama hayo aliyokupitisha.

Utadai pesa je asipokuwa nazo atakulipa nini? Najua unaweza kuishi bila hizo pesa ambazo unataka kudai kwa huyo mzee wako. Kama uchumi wako haujatetereka achana na kelele za kifamilia unda himaya yako uwe mfalme katika himaya yako uishi katika misingi yako uache kufuatilia huyo unaeita mpumbavu.
 
Pole sana mkuu, huyu mzee alikutunza vyema wakati hajaanza kufanya huo unaoita upumbavu au alikuwa hivyo tangu zamani?

Je ana mgogoro na mkewe yaani mama yako.?

Umewahi kufuatilia japo kujua chanzo cha yeye kurudi nyuma kiuchumi ni nini.?
Achimbe tena kuhusu mama yake na baba yake ?
Hapana asamehe tu Mungu atampigania atanyanyuka. Kuna vitu si vya kujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…