Nakusudia kuishitaki airtel tume ya mawasiliano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakusudia kuishitaki airtel tume ya mawasiliano.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by FADHILIEJ, May 14, 2011.

 1. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa mteja wa Airtel kwa muda mrefu sana,lakini tabia yao kukwepa kutoa msaada kwa wakati linaudhi sana,utakuta unapiga simu customercare lakini unachoambulia ni matangazo marefu yasiyo na msaada unaouhitaji,

  Ukiacha hilo la wahudumu lingine ni hili la Bahati nasibu ambazo hazieleweki zinazokula hela za wateja wasio na hatia bila kusahau hili la kuahidi kutoa 200MB kila unapoongeza muda wa hewani,THEY ARE NOT OPEN na ukijaribu kutuma sms kama wanavyoelekeza unaambiwa hauna MB yeyote,hakuna pa kuuliza!!

  Naomba kama AIRTEL WANANIPATA WANIPE MAJIBU SAHIHI,au kama kuna mwanaJF anayeweza kunipa soln anisaidie,VINGINEVYO KUNA HAJA YA KUWASHTAKI TUME YA MAWASILIANO au BARAZA LA USHINDANI.
   
 2. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nilishapiga simu siku mbili mfululizo na sikuwapata hao wanaojiita huduma kwa wateja.Nilikasirika sana ikabidi niende kwenye office yao ndio nikapata msaada ambao si kwa wakati.WANAUDHI SANA.Awali walikuwa very active !Kuna mtu yupo hapa JF anadai ni mwakilish wa airtel ngoja aje!
   
 3. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Yaani suala la kupiga simu customer service haya makampuni ya simu ni kero kubwa, yote huwa hawapokei lakini uende ofisini kwao. Nilipoteza simu siku kwa siku nne nilikuwa napiga simu ili waifunge lakini hakuna siku nilipokelewa mpaka nilipofika dar na kwenda ofisini kwao wakati huo karibu credit yote imeisha tumika. Mpaka sasa nina hasira nao sana
   
 4. c

  ccr airtel Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu punguza hasira
   
 5. c

  ccr airtel Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu wadau tatizo ni kwamba kupiga simu huduma kwa wateja ni bure so kuna wateja wengi wanapiga simu hasa wa maeneo ya kishapu,katesh,babati,shinyanga,mtwara (haswa masasi),rorya,tandahimba...Hawa wananchi anaweza akapiga simu (ofcoz anapokelewa kama mteja mwingine yeyote anavyopiga coz huwezi jua shida ya mtu au kujua huyu mtu atauliza nini hadi atakapotamka tatizo lake),kisha anakwambia nilikua nataka kukusalimia tu,au naomba nitumie japo 200 ndugu yangu sina kitu kabisa (hapo ana salio la 500),au akakwambia nilitaka tu kujua saa ngapi, au mwingine anasema,au tatizo jingine kubwa tunalokabiliana nalo kwa sasa ni wateja kuuliza maana ya 200MB (kifurushi cha intanet cha ofa baada ya kuongeza salio),kuna mteja mimi binafsi aliwahi kunipigia simu anataka tuombe coz huko alipo kuna tatizo lamtandao...na hii yote ni kwa sababu huduma ni ya bure with no limitation,au unaweza kukuta mteja mwingine haweki salio kazi yake kupiga tu namba 100 na akipokea mwanaume anakata (shida yake ni wadada tu)...ila ukweli ni kwamba kwa siku wafanyakazi wanaokua online kuhudumia wateja ni zaidi ya 350 na bado wanaongezwa na kila mmoja anapokea wastani wa simu 165 wastani wa dk 2.5 kwa simu...AHSANTENI SANA WADAU KWA KUCHAGUA AIRTEL KUMBUKENI WEEKEND OFFER SALIO KUANZIA 1000 UKIONGEZA UNAPATA 10 MINUTES FREE,100 SMS NA KIFURUSHI CHA 200MB KUANZIA SAA NNE USIKU HADI KUMI NA MBILI HASUBUHI
   
 6. I

  Imnyagi Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natumia mtandao wa Airtel tangu umeanza ila ukweli ni kwamba kero ni nyingi kuliko faida nashindwa kuwaacha maana namba hii nimeizoea kwa muda mrefu sana ila ki ukweli wanakera kuliko tunavyolalamika maana watu wengi wengi hatuna muda wa kulumbana hasa na computer zao zizotujibu kwa matangazo yasiyo na idadi
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  unapogundua mteja kapiga cm na anashida ya muhimu unaendelea kumsikiliza wa nn? na ukishapokea cm moja au 2 ya wateja wa hovyo inamana ndio ucpokee cm zingine kwa kuwafananisha wateja wote ni wale wale ili la ofa yenu linahitaji ufafanuzi aidi mana limekaa kisanii zaidi
   
 8. c

  ccr airtel Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  drphone em soma tena nilivyoandika naona hujaelewa nimeandika nini...
   
 9. c

  ccr airtel Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  drphone em soma tena nilivyoandika naona hujaelewa nimeandika nini...halafu hakunaga mteja wa hovyo wala hairuhusiwi kumkatia mteja simu na zaidi ya yote kila mteja ana haki ya kusikilizwa tatizo lake na kushauriwa ipasavyo ili aweze kuendelea na matumizi yake ya simu
   
 10. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ccr Airtel
  Nimekupata lakini sikubaliani na maelezo yako,naamini unawaonea hawa ndugu(maeneo ya kishapu,katesh,babati,shinyanga,mtwara (haswa masasi),rorya,tandahimba...)HATA KAMA NI KWELI JE NDO SABABU YA KUTOPATIKA NA KWA WAKATI KWA WATEJA WENGINE?
  1.naomba muanzishe huduma ya wateja kwa malipo tupo tayari kulipa ili kupata huduma sahihi na kwa wakati.
  2.Mbona wenzenu Voda wanajali wateja hadi huduma za nipige tafu wameanzisha?mnashindwa nini.
  3.Mwisho naomba muwe mnatoa ufafanuzi wa gharama za huduma zenu badala ya kusema gharama zitatozwa au vigezo vitazingatiwa.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280

  Crap,... siasa imeharibu sana nchi hii. Angalau hapo kwenye RED mmetupunguzia udhalilishaji wa kukesha mpaka saa 6 usiku kusubili hizo offer zenu za kisanii.
   
 12. s

  shujaa Member

  #12
  May 17, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ccr airtel, nashukuru kwa maelezo na ufafanuzi, lkn kama kuna wateja mpaka rorya ina maanisha mtandao una tanuka na customer base ina ongezeka which leads to you to add the number of your customer care staff
   
 13. h

  hubby Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona marcopolo imepata ajli, au imekwama kwenye tope, hamia kwenye chopper ( vodacom) ni mauwezo zaidi, au njoo tuishi kama wafalme na elsat
   
 14. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nina Tigo, Voda na Airtell, kati ya wote hawa airtell wanajitahidi sana wengine hopeless ila naendelea kuwa na line zao kwa sababu nilianzia huko sitaki kupoteza contact zangu
   
 15. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mitandao yote ni kero. AIRTEL wameshakuwa more than TIGO, vitu kibao wakati hawana uwezo navyo, sijui ndiyo kuwaua wenzao kisanii. Hiyo huduma yao ya kuhamisha basi nafikiri walifanikwa pale walipowatoa kwenye BITO kwenda kwenye basi la mchina but practically wako ZERO. ukipiga ile namba yao ya hamisha kuna watu wako DESPERATE wametoka nyumbani kwao hawajala au amepanda dala dala kakanyagwa akija pale ana majibu mabaya kuliko ya MAJI TAKA ya mikocheni uswahilini.

  Nahisi wewe hujakumbana na hiyo kero ndiyo maana unatupa story na siyo maelezo tunayataka utueleze. Unapotwambia wanapiga toka tandahimba etc, ni kwamba sisi wa DSM ndiyo tusihudumiwe. kwa nini usiwe mkweli kwamba tunahudumia watu wa LOLIONDO kwanza wewe wa bongo subiri? is that a big deal? Hivi kweli hao customber care wenu mnawapeleka shule mnawaokota bara barani? Jamani unaweza fikia sehemu ukakashfu kazi ya mtu si kwa kupenda ni kutokana na kutokwa na malezi mazuri kikazi.

  Mimi nimefanya kazi sehemu nyeti ambazo ukitoka mezani ext ikaita zaidi ya mara tatu ukirudi unaandika maelezo. Ina maana ulitakiwa uache maelezo ya kutosha kwa walengwa.

  Tafadhali peleka huu ujumbe, ajiri watu wenye sifa na ari ya kazi siyo wale wanakuja wakifika hapo wanaanza kukumbuka boyfriend/girlfriend waliowaacha nyumbani. Sometimes unaeda pale unakuta mtu anaongea na simu yake ya mkono anakutolea macho kama hana hata wasi wasi mpaka amalize upupu wake ndiyo akukumbuke.

  Inachefua sana. Peleka salaam kwa wote.
   
 16. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 80
  Siye tuliyo nje ya nchi ktk mtandao wa One Network ndo tunalia kabsaaa! Yaani ukipigiwa simu au sms toka Tanzania salio lako linakwisha. Pia salio likiisha unakuwa hupatikani.! Gharama ya kupiga simu ukiwa Uganda kupitia Airtel Uganda kwa kutumia line ya Airtel Tanzania ni tsh.500 kwa dakika hata kama uongee sekunde mbili, wakati ukitumia Airtel Uganda kupiga nyumbani Airtel Tz unalipa Ugx 150 kama ukimaliza dakika nzma ila wanakata kwa sekunde, pesa hiyo sawa na jiti la madafu. Hiyo Airtel One Network ina maana gani kwetu? Mbona Vodacom Tanzania nikipigiwa sikatwi hata senti? Hata kifurushi cha data cha Voda kinatumika huku kupitia MTN UG, wakati kifurushi nilichonunua Airtel Tz hakitumiki kupitia Airtel Uganda. Airtel tz wamezidi wizi.!
   
 17. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Kutaka kwenda kushtaki TCRA ni hatua nzuri coz ina maana unaelewa haki zako. Mi nakudokeza taratibu za kufuata, maana nilishawahi kufuatilia suala la namna hii. Kwanza kama hujaridhika hatua ya kwanza ni kwenda kwa mtoa huduma (in this case, airtel) na kuwaeleza tatizo lako (mfano unaweza ukaandika barua kwa airtel, copy TCRA), usiporidhika na response yao ndo unaenda TCRA-wana form za malalamiko online. Utajaza fomu hiyo na utahitaji uonyeshe kwamba uliwasiliana na mtoa huduma kabla ya kwenda TCRA. TCRA can then proceed from there...
   
Loading...