Nakusihi NILHAM RASHED | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakusihi NILHAM RASHED

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mohammed Shossi, Jan 31, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Najua hujaolewa ndio kwanza unaghilibiwa, nakuomba ufikiri utofautishe mapenzi niliyonayo juu yako.
  Naandika huku nalia sina wakunifuta machozi enyi wanaJF hamunionei huzuni??? Wanawake wote nisaidie kwani anaemzuzua amewashusha hadhi kumkataa Michelle na kukana hadhani. Asije kuleta madhara akijakumtosa Nilham pia .......


  Nisikiza Nilham nikupe yakini
  Nenda na laiti na mengi ya ndani
  nakupenda dhati sipati kifani

  Hunijia wakati ukanijia ndotoni
  Viungo vya kati vyako vya mwilini
  Toka magotini kuja kifuani.

  Rangi samawati yako ya machoni
  Husadiki kuketi nenda kiooni
  Huna tafauti na khurulaini

  Nipe wako wakati Nilham tabasamu
  Ishe yangu hamu inirudi fahamu
  pendo kwa thamani lashinda hisani

  Nilham tusitupane zitanizidi huzuni
  Helo njoo tuonane tupane ilo yakini
  Uliyonayo unene nijuwe ni jambo gani
  Nilham umejitenga kunitia majaribuni?


  Nilham nikupendae mrembo nilokuamini
  Nawe usinikimbie tanitia mashakani
  Ulilonalo nambie kilokuudhi ni nini?

  Nilham wanipa dhiki kwa kunitosa jamvini,
  Nilacho hakinishuki kikanituwa tumboni
  Huchekwa na halaiki wanionao jamvini

  Mwanamke uliye bora mfano wako siuoni
  Imenifika hasara tangu wewe kunihuni
  Macho yangu yamefura nimekuwa ugonjwani

  Kishuna nihurumia hali yangu imekuwa duni
  Usiku hujikeshea kwa mawazo akilini
  Hukumbuka mazowea njema na zako hisani

  Nilham usighurike hebu mlani shetani
  Niliwaza usichoke unitowe majonzini
  Mwanzo wetu ukumbuke usisahau fulani.........

  Nilham jua lazama lapotea milimani
  Nimechoka kusimama kukunasihi jamvini

  Nilham nenda ukija mpenzi wangu wa mwanzoni
  Niko pweke nakungoja mwenginewe sitamani
  Kwako ningali na haja nikwambiayo amini  http://www.youtube.com/watch?v=1dxDpWq5H8Y&feature=related

  Nilham sitaacha kusubiri maadam nakupenda
  Subira huleta kheri huvuna mema matunda
  Muhibu nina kuambia nisikize kwa makini
  Sitachoka kungojea kukusubiri muhisani


  Sitaona udhia nikajidhiki moyoni
  Huini raha naumia na kuhisi ni duni
  Itakuja siku moya tatuweka ziewoni
  Muhibu nakwambia nisikize kwa makini
  Sitachoka kungojea nitasubiri muhisani  Japo siku zinapita na hamu yako kuzidi
  Nitapunguza mashairi na moyo uwe baridi
  Utakuja kuniita, name hunu nifaidi


  Sitafanya ghadhabu niingie hasirani
  Lolote ni taratibu nitakula kwa makini
  Nimekuwekea zababibu sitampa mtu thani


  Nitakutunza nafsi nikuambiayo ya ni kweli
  Usiwe na wasiwasi wakati ukiwasili
  Utalila na nanasi, utamu washinda asali
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mh,
  Nilhaam umedondokewa hii leo, letu jicho.
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  I'd still embrace it for I know that in between those thorns, there is a rose that's worth all the pain.
   
 4. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wallahi tena..!
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Eeeee sasa hata mie ntakusaidia Kumbembeliza.lol
   
 6. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  na wewe....
   
 7. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  crap....l.o.l
   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
 9. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  gud decision..vunja ukimya..sio mpaka usubiri wahisan watu wa marekani
   
 10. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mwenye kisu kikali ndie atakaekula nyama..................
   
 12. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  deal
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Shukran AD wewe shahidi jinsi huyu jamaa anavyochezea mioyo ya wanawake si ulikuwepo alipomkana Michelle kweupepeee!
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hasycool VS Mohammed Shossi
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu,tangu ulivyoanza kumsifia na kumpiga senks nilijua tu ushaoza. Sasa jaribu kumpm ajue kuwa uko serious badae ndo muendele, usisahau kutupa updates!
   
 16. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #16
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Shukrani kwa mawazo yako mazuri.........
   
 17. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  genekai stop giving him hopes that will never come true......l.o.l
   
 18. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #18
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mpaka kieleweke...............
   
 19. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  mbona kisha eleweka siku nyingi wewe.....
   
 20. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #20
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mie sitii neno ila nachelea utakuja umbuka omba wanawake wa nyumba hii waendelee kulala maana wanakujua tabia zako. Umeshau ulivyomdhalilisha Damichelle? Si unawajua wadau wa Beijing????????? hiyo ndio silaha yangu muhimu............
   
Loading...