Nakupongeza RC Makonda na vijana wote wanaowakilisha vema vijana kwenye nafasi zao wakiwemo Lema, Happi na Mdee

Butiyangu

Senior Member
May 19, 2018
123
167
Mwanzo sisi vijana hatukukuelewa Kabisa na Wala hatukuwa na Imani na wewe katika kuusimamia mkoa wenye watu wengi Tanzania, kutokuwa na imani na wewe kulitokana na ukweli kuwa madaraka kama hayo wazee ndio waliokuwa wanaweza kuusimamia Government system

Imani hiyo ilitokana na ukweli kwamba miaka ya nyuma wazee ndio waliopewa nafasi za kushikiria nyanja tofauti za Serikali na vijana walisahaulika kabisa na kubaki tu kuitwa vijana ni Taifa la kesho, huku wazee wakiwa ni Taifa la Leo

Ninachokupongeza RC Makonda na vijana wengine kama RC Gambo na RC Happi, Mbunge Lema na vijana wengine mmetuzihirishia kuwa mnaweza na kufuta ile kauli ya kuwa kijana ni Taifa la kesho.

RC Makonda kweli kabisa nakiri ulipokabidhiwa jiji kuliongoza ulikuwa mihemuko sana ya ujana, lakini tunachoshukuru bado Rais alikuamini na kukupa nafasi nyingine ya kujirekebisha na kweli hukufanya kosa ulijirekebisha.

Wewe umekuwa mfano wa kuigwa Kwa vijana wapenda maendeleo, najua kuna nyakati ulipitia Magumu sana kwenye uongozi wako lakini ulisimama Imara zaidi, umeweza kulisimamia jiji na kuwa tulivu kabisa Ujambazi umekuwa historia, najua jiji linachangamoto nyingi sana nakuomba upambane nazo bila kukata tamaa.

Endelea kuudhihilishia umma kuwa kijana akipewa nafasi naweza. Wapo vijana wengi tu wanafanya vizuri kwenye nafasi zao kama vile Mbunge Halima Mdee, Bulaya, Bashe na wengine wengi. Ninacho waomba tukipewa nafasi yeyote katika jamii ya kuongoza watu, ni lazima nafasi hiyo tuitumikie vyema ili hao wazee wakose cha kuongea.

Asante
 
Sawa tunashukuru kwa pongezi zako. Atakaposoma hili andiko lako bila shaka atazipokea kwa bahshasha tele.

Ila tu wakati mwingine na wewe ujitahidi kurusha nafasi kama nilivyofanya mimi hivi; badala ya kuandika tu kwa paragraph ili kuepusha kutokea kama hicho kilichotokea kwenye hii mada yako.
 
Mwandishi si kijana bali ni mtu wa makamo aliyejitoa ufahamu na kupongeza ujinga akitegemea kupewa khanga na kofia.
 
Mwandishi si kijana bali ni mtu wa makamo aliyejitoa ufahamu na kupongeza ujinga akitegemea kupewa khanga na kofia.
Mfano kama Mh. Nasari angepewa nafasi ya Mh. Makonda unafikiria ingekuwaje? Cdm ndio cha wasomi hao wakibidhiwa Nchi wote watahamia Marekani.
 
Back
Top Bottom