Tarehe 10/10/2019 RC Makonda atawatolea nyongo Mawaziri Jaffo na Mpango

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,274
TAREHE TEN YA MAKONDA, JUMBA BOVU LIWAPONDE MAWAZIRI JAFO NA MPANGO

1. Mambo 8 kati ya 10 ya Ilani ya CCM aliyoyataja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Paul Makonda, Mnyika, Halima Mdee na Kubenea mwisho 2020.

2. Makonda aitahadharisha wizara ya TAMISEMI baada ya wizara hiyo kuurushia mpira kwa Mpango wizara ya Fedha 💰, asema kama wataendelea na ngonjera zao, basi jumba bovu litawaponda wao ifikapo tarehe 10 mwezi huu.

inukakisimachafikracha@gmail.com
0784977072

1.Jana tarehe 5 Mkoa wa Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa Ndg. Paul Makonda umetoa Ripoti ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
RC. Makonda ktk ripoti hiyo ameeleza mambo 10 ya Ilani ya CCM yaliyotelezwa ktk Mkoa wake ambayo ni:-
Mosi, Sekta ya Maji, RC. Makonda amelifafanua vyema suala la maji na namna alivyolitekeleza kwa kiwango kikubwa katika mkoa huo, ameeleza kwa Mkoa wa Dar es Salaam karibu kila Wilaya na kata zote pamoja na mitaa yake imewekewa miundombinu ya maji safi, mabomba pamoja na matenki kadhaa ya maji. Hivyo shida ya maji haipo tena na inafahamika kupitia kampeni yake ya kumtua ndoo maama miaka mitatu iliyopita ilifanikiwa kwa asilimia zote 💯.

(ii). Sekta ya Ujenzi, imeelezwa kwamba kwa Dar es Salaam suala la ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimkakati, mabarabara na miundombinu mingine limefikiwa kwa kiwango kikubwa sana, na kueleza kuwa ni baadhi tu ya maeneo ambayo miundombinu yake bado inaendelea kukamilishwa mfano mradi wa mkubwa wa machinjio ya Vingunguti, madaraja ktk mto Ng'ombe na mingine michache itakamilika hivi punde.
Lakini kwingine kote ameeleza kuwa, kero kama ya mabarabara imeshakwisha na kwa ujumla jiji hilo limejengeka haswa katika kipindi hichi cha utawala wa Rais Magufuli.

(iii). Sekta ya Afya, nafikiri hii halihitaji hata ufafanuzi mkubwa kwa sababu tayari limeshavuka boda hadi mikoa mingine hapa nchini. Hakuna asiyejua kazi inayofanywa na Mkuu huyu wa Dar Paul Makonda, tangu mwanzo, kabla ya kampeni iliyopamba moto hivi karibuni ya watoto wanaotoka kaya masikini wanaofanyiwa upasuaji katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Liko wazi kuwa kampeni hiyo imebeba watoto karibu nchi nzima wanaotoka Tanzania visiwani na Tanzania bara na kisha kumfuata Mkuu Makonda ili wapatiwe matibabu na kuokoa maisha yao.
Kwa kuyataja machache tu, Makonda amekuwa akiwasaidia wananchi wengi ndani na nje ya Mkoa huo wa Dar, mbali na hilo, lakini pia ni pamoja na mpango wake wa kutibu watanzania wenye magonjwa mbalimbali mtakumbuka madaktari aliowakusanya pale Mnazi mmoja ambapo wananchi wengi kutoka pembe zote za Tanzania walikwenda kupatiwa matibabu.
Mtakumbuka pia Madaktari walioletwa na Meli kutoka nchini China ambapo watanzania wengi wenye magonjwa sugu walipatiwa matibabu.
Hayo na mengine kama ya miguu ya bandia nk, yanakumbukwa na watanzania.

(iv). Sekta ya umeme, hili liko wazi, kwa jiji kama Dar es Salaam, suala la umeme linaeleweka kwamba jiji hilo limebeba roho za wengi, hospitali kuu, Ikulu, viwanda, safari za lifti za kwenye maghorofa mengi, Bandari, vyombo vya habari, vyombo vya usalama nk.
Pamoja na kuwa Serikali imelisimamia suala la kusambaza umeme takribani nchi nzima, lakini kwa Dar hayo niliyoyataja ni muhimu sana kuwepo kwa umeme wa kutosha, ni bora ukatike umeme nchi nzima lakini sio ktk jiji hilo, sababu kuu ni hizo.

(v). Sekta ya Ardhi, hili ndilo limeelezwa kuwa ni miongoni mwa matatizo makubwa aliyoyashughulikia Mkuu wa Mkoa kutokana na ukweli kwamba, wenye hila wamekuwa wakiwazulumu wananchi wa kawaida na kupelekea kukosa haki zao za msingi kwa kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi ili kudai haki zao hata pale wanapohitaji haki mahakamani. Mkuu wa Mkoa amempongeza Waziri Lukuvi kwa weledi mkubwa alioufanya kwa kutoa ushirikiano katika mkoa huo na kutatua kero hizo na sasa wananchi wa Dar es Salaam wanajisikia amani na utulivu katika nchi yao, tofauti na zamani.
Suala la Ardhi linaelezwa kwamba, Ardhi ndiyo kitu pekee ambacho mtu anaweza kuifia kwa sababu ndicho kitu pekee cha thamani kuliko vyote duniani, ardhi ndiyo chanzo cha utajiri wa binadamu, kutokana na ardhi tunapata madini mbalimbali, chakula, maji na makazi.

(vi). Sekta ya Ndalichako (Elimu), ingawa tunahitaji mapinduzi makubwa ya kimfumo katika sekta hii ya elimu kama kubadili mitaala na kuondoa sheria za hovyo za kuondoa viboko shuleni ambapo imechangia kubomoa maadili ya vijana wengi nchini kwa sababu ya kigezo cha haki za binadamu na ikiwezekana kuondoa kabisa uongozi wa juu katika wizara hiyo kutokana na kutokuwa wazalendo.
Lakini suala la elimu limeelezwa na Mkuu wa Mkoa kuwa mkoa wake umefanya mengi na bado wanaendelea kuboresha Mazingira ya waalimu na wanafunzi na miundombinu mingine muhimu kama makazi (nyumba za waalimu na majengo mapya ya madarasa) kwani mahitaji mengi kama vitendea kazi vya waalimu yameshatolewa.
Asiyekumbuka viwanja vya watumishi vilivyopiganiwa RC. huyo, shehena za makontena za mahitaji ya shule aliyoyaleta Makonda na kuwakabidhi waalimu, basi mtu huyo anayejitia upofu ama hafuatilii vyombo vya habari nchini kabisa au vinginevyo zikiwemo nongwa na hila.

(vii). Sekta ya viwanda, sekta hii kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni tofauti kabisa na mikoa mingine ambako tafasri ya viwanda imekuwa ikitafsiriwa kwa mitazamo ya kisiasa na ufinyu wa fikra, upeo juu ya mambo ya viwanda.
Tofauti hiyo ameieleza kwa wale wakuu wanaofikiri kwamba hata vyerehani mbili tatu navyo wanaviita ni viwanda.
RC. Paul Makonda ameeleza kwa upande wake ni tofauti kabisa, ametaja Mkoa wake unaviwanda vingi na vimeajiri watu wengi, na vile vile ametaja baadhi ya viwanda kadhaa ambavyo vinatengeneza bidhaa vinavyotokana na malighafi, zinazouzwa hapa hapa na kuuzwa duniani kote kama Marekani na kwingineko.
Makonda amesema kuwa viwanda hivyo haviajiri watu wawili au kumi kwa maana ya wachache, bali ni maelfu ya watanzania wanaofanya kazi katika viwanda hivyo.
Hii ni pamoja na miradi mingine mikubwa ya kimkakati inayoendelea kujengwa katika jiji hilo, ni miongoni mwa miradi inayoendelea katika Mkoa huo imeajiri vijana wengi.

(viii). Sekta ya ulinzi na usalama, suala la ulinzi na usalama katika Mkoa wa Dar es Salaam limeelezwa na Mkuu Makonda kuwa, pamoja na kuwa jiji hilo lilionekana kuwa na changamoto kibao wakiwemo watu jeuri, wahalifu vijana kwa wakubwa, sijui panya road na makorokoro mengine ya vibaka amelielezea suala hilo kuwa kwa sasa hakuna tena mtu au vijana jeuri wanaofanya uhalifu.
Sasahivi ametangaza amani tele, wewe park gari lako nenda zako, kama ni disco au kwingineko utarudi na kukuta betri na vyombo vingine katika gari lako viko salama.
RC. Makonda ameielezea sekta hiyo kuwa wamejiimarisha zaidi katika Mkoa na hata kuboresha mahitaji ya jeshi hilo.
Mtakumbuka pikipiki na magari aliyoyafanyia ukarabati aliyoyagawa RC. Makonda katika jeshi hilo la polisi.

Mwisho kabisa ktk mambo 10 aliyoyaeleza Mkuu wa Mkoa Makonda katika mkutano wa jana, ni pamoja na kuvishauri vyombo vya habari kuwa na uzalendo kwa taifa kwa kutojikita katika kuhabarisha umma yale mambo mabaya tu na kupotosha ukweli, mbaya zaidi hata hayo mabaya ni ya kupikwa, yaani majungu. Huu ni ushauri murua sana kwa vyombo vya habari.
Ushauri kama huu uliwahi kutolewa na Rais wa Msumbiji Samora alipowatahadharisha waandishi wa habari nchini humo baada ya kuiacha taaluma yao na kukimbilia kutengeneza pesa tu kana kwamba ndiyo lengo pekee la taaluma hiyo.
Rais Samora aliwaonya kwa kusema kuwa, "Enyi waandishi wa habari, angalieni sana, maana mara nyingi wanasiasa hupenda muwabebe migongoni ili muwavushe kwenye matope. Na wakati mukiwavusha, matope huwarukia nyinyi, lakini mukiwavusha, wanasiasa hushuka migongoni mwenu na kuwaacha huku matope yametapakaa kwenye suruali zenu."
Pia RC. Makonda alitoa salamu ktk Uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu kwamba, ushihidi wa Chama Cha Mapinduzi CCM uko wazi na mapema sana katika serikali za mitaa jijini humo, na kueleza bayana kwamba, anazo taarifa kutoka kwa wabunge wa Ubungo Kubenea, Mbunge wa Kibamba John Mnyika na jimbo la Kawe kwa Halima Mdee ya kuwa, wabunge hao hawafanyi hata ziara kwa wananchi waliowapigia kura kwa sababu wanajua fika kwamba 2020 hawatoboi na hivyo hawaoni sababu ya kutumia fedha zao kufanya ziara katika majimbo hayo ilhali wanajua hawatarudi bungeni. Hivyo wameona bora fedha hizo wazitumie kulea familia zao. Na ndiyo maana ziara zinafanywa na wakuu wa Wilaya na kutatua kero za wananchi wa maeneo hayo.

2. Nilianza na hayo ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa kutokana na umuhimu wake. Suala la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kuhitisha Maandamano kuielekea wizara ya TAMISEMI chini ya Seleman Jafo ili wizara hiyo ipondwe na jumba bovu kabla limeibuliwa katika ziara ya Mkuu wa Mkoa juzi baada ya kufika site na kukuta ngonjera kibao za mratibu wa DMDP.
Baada ya kukutana hali hiyo Makonda alipiga simu ya wazi na ukweli ukajionyesha wazi kuwa lipo kwa Jafo kupitia kabineti yake.
Jambo hilo lilimpa hasira RC. Makonda na kutoa tahadhari kwa wizara hiyo ya Jafo ya TAMISEMI baada ya mratibu wa DMDP kuishushia lawama wizara ya fedha ya Waziri Philipo Mpango kuwa ndiyo inayochelewesha mipango yote, kwani haijatoa fedha ili kutekeleza miradi waliyoingia mikataba na Mkoa wake.
Makonda ameeleza kuwa hoja hizo ni za kipuuzi kwa sababu wananchi hawajui mambo hayo zaidi wanawajua Rais Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kwamba mwisho wa siku yanapoharibika mambo yote ya miradi, jumba bovu anavikwa Mkuu wa Mkoa.
Makonda ametoa kauli ya kiume kabisa huo ndio msimamo unaotakiwa awe nao kiongozi pale anapoona kuna mambo ya hovyo na ngonjera zenye kuashiria cha rushwa.
RC. Makonda ameeleza kuwa ifikapo tarehe 10 kama wizara hiyo itaendelea na ngonjera zake hizo bila kuchukua hatua basi atahamasisha kata 5 zijazohusika na miradi hiyo na iliyopigishwa maktaim kwa muda mrefu ili wananchi hao wachukue hatua ya kuandamana kuielekea katika wizara hiyo ya Jafo ili lile jumba bovu wanalotegemea kumwangushia Makonda liwaangukie wao.
Binafsi nampongeza sana Mheshimiwa Makonda kwa ujasiri na hatua hiyo, na kama ningelikuwepo hapo Dar ningeyatangulia maandamano hayo ya kuwasukumia hilo jumba bovu wanaolielekeza kwa mtu asiye na hatia. Haiwezekani Rais awe anaowanyooshea vidole viongozi wasiohusika na mizengwe hiyo ilhali kunawanaosababisha uzembe huo lakini hawamrikwi kabisa, badala yake jumba bovu linawaangukia wasio na hatia.

Imeandikwa kuwa, kila mtu atabeba msalaba wake, na siku ya tarehe ten kama TAMISEMI wataendelea kuonyesha jeuri na ngonjera zile zile, basi siku hiyo itaeleweka nani ni nani.
Maana umefika wakati mizaha ikomeshwe, na kabla mtu hajakumwagia mboga wewe mwaga ugali wake bila kujali yuko juu yako ili mheshimiane mjini. Haiwezekani mtu akudobole machoni umemwangalia tu bila kuishikisha adabu mkono wake eti kisa we ni mstaarabu!?

Huyo ndiyo Paul C. Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, jiji lenye kila kitu, Dar ya Makonda, maarufu kama sura ya Tanzania.

1570348488054.jpeg
 
Naona umeamua kufanya triangulation, angalau wewe ni demu inaeleweka, ni kawaida Wanamake kuchonganisha Wanaume, shida ipo kwa Wanaume wanaochonganisha wanaume wenzao!
 
Hivi unamfahamu Waziri wa TAMISEMI?
Na ndiye huyo anayemlenga/anayemfikishia ujumbe kuwa hata wewe hunitishi.

Hivi huwa hushangai huyo "waziri" akiwa anamuongelea Makonda huwa anakuwa mnyonge Sana as if nimekuchoka sema tu Sina uwezo wa kukushughulikia?
 
Waziri wa TAMISEMI si ni John Pombe Magufuli? Mara kadhaa nimemsikia akijitapa kuwa yeye ni waziri wa TAMISEMI.
 
Naaam Waziri wa TAMISEMI ni Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli. Yeye pia ni Waziri wa Utumishi na Utawala Bora. Sasa Makaonda anavyoishambulia TAMISEMI hajui kwamba anamshambulia Mkuu wa Nchi. Makonda ana shughuli
 
Imeandikwa kuwa, kila mtu atabeba msalaba wake, na siku ya tarehe ten kama TAMISEMI wataendelea kuonyesha jeuri na ngonjera zile zile, basi siku hiyo itaeleweka nani ni nani.
Maana umefika wakati mizaha ikomeshwe, na kabla mtu hajakumwagia mboga wewe mwaga ugali wake bila kujali yuko juu yako ili mheshimiane mjini. Haiwezekani mtu akudobole machoni umemwangalia tu bila kuishikisha adabu mkono wake eti kisa we ni mstaarabu!?

Save the date...

Cc: mahondaw
 
View attachment 1224789
Sasa hivi msimu wa uchaguzi umewadia,kambale wote wanatunisha sharubu zao.Hiyo miradi si inabajeti,wasimamizi na muda wa utekelezaji?Mbona ni kama maigizo ya kuhitaji sifa binafsi?.
Watanzania Tudai Katiba ya Wananchi sasa kabla hatujapelekwa wanapotaka watawala bali kule tulikopanga sisi wenyenchi na vipaumbele vyetu vya kitaifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom