Nakukumbusha Nape Nnauye kwamba Mbowe si kama Lowassa uliyemtukana utakavyo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,431
Nape Nnauye , mwanaccm na Waziri wa Habari , umesikika Bungeni ukipiga porojo kuhusu Mbowe na Maridhiano badala ya kujadili kuuzwa kwa aibu kwa bandari za Tanzania .

Umefika Mbali sana kwa kusema kwamba wanaopinga ujinga wa kuuzwa kwa Bandari washughulikiwe , maana mbegu ikiwa ndogo iko siku itakua (VITISHO)

Hata hivyo nakutahadharisha kwamba Freeman Mbowe , mtu mwenye exposure ya kimataifa kuliko kiongozi yeyote wa Tanzania siyo fala , huyu hafanani na Lowassa uliyemtukana matusi ya nguoni na kumdhalilisha utakavyo kwa kulindwa na Kikwete , kwa Mbowe wewe ni mtu mdogo mithili ya Piritoni , kwa hiyo unapomjadili mtu huyu ambaye Serikali yako IMEMUOMBA RADHI KWA KUMSINGIZIA UGAIDI unapaswa kuwa makini mno !

Ninachokifahamu ni kwamba hukutumwa na mtu kushambulia Mbowe , bali ni kiherehere chako tu , hata hivyo hatutakunyamazia , hii ni kwa sababu hata ubunge wako si wa kuchaguliwa , japo uko bungeni lakini huna unayemwakilisha .

FB_IMG_1589397986327.jpg
Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
JamiiForums1267461471_387x387.jpg
 
Hizo kelele za mlango tu, ngoja Mbowe aongee tena uone watakavyoanza kuhangaika, hii Tanzania bara ni ya wabara, wazanzibari kwao visiwani kule bahari ya Hindi.

Lazima tuongeze sheria mpya kwenye Katiba iliyopo;

Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuwa Rais wa Tanzania kama ana akili ndogo.

Utajuaje uwezo wake kiakili;

Apewe mtihani wa kujieleza na kuandika, atuambie ataifanyia nini Tanzania, kama akisema ataishia kuomba mikopo kila siku, huyo hatufai.
 
Wabunge wa Tanzania ni aina flani ya watu ambao hawana uchungu na taifa wao wana uchungu na chama chao na tumbo zao, haiwezekani wabunge wote wawe sawa kwenye hili
Kuna uwezekano kabla ya mjadala Bungeni wa kuridhia IGA, Wabunge wa CCM walikaa kukubaliana ya kuwasilisha, na kuteua wa kuyawakilisha. Aiingi akilini waliochangia mjadala waongee lugha moja ya kusifia kama CHAWA
 
Nape Nnauye , mwanaccm na Waziri wa Habari , umesikika Bungeni ukipiga porojo kuhusu Mbowe na Maridhiano badala ACH]View attachment 2653199
Binafsi sikuipenda kauli ile.....

Ndio maana KUCHUNGA ULIMI NI VIZURI SANA.....

Ninamheshimu sana komredi wangu...anajua hilo.....

Kwa hili...komredi amekosea kwani "naye ni mhanga".....anatakiwa awe mfano.....

Mihemko kitu kibaya sana...

Komredi punguza mihemko...

#MamaAnaupigaMwingi

#Tuko Na DP WORLD burdaaaan

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hizo kelele za mlango tu, ngoja Mbowe aongee tena uone watakavyoanza kuhangaika, hii Tanzania bara ni ya wabara, wazanzibari kwao visiwani kule bahari ya Hindi.

Lazima tuongeze sheria mpya kwenye Katiba iliyopo;

Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kuwa Rais wa Tanzania kama ana akili ndogo.

Utajuaje uwezo wake kiakili;

Apewe mtihani wa kujieleza na kuandika, atuambie ataifanyia nini Tanzania, kama akisema ataishia kuomba mikopo kila siku, huyo hatufai.
Mataifa tajiri yanakopa sembuse sisi ?!!!

Marekani ndio inayoongoza kwa MADENI.....

Tanzania ni taifa la wote....

Hiyo KATIBA yako ni mfu kama ile katiba hovyo ya mh.Jaji Warioba

#Tuko na DP World ,burdaaan
#MamaAnaupigaMwingi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi ina vituko

Kwahiyo unasema Nape ni piritoni kumlinganisha na Mbowe?
Hapo Mbowe ni kama nini Kwa ukubwa?malizia mifano ..
Na Lowasa nae unamlinganishaje Kwa Mbowe??...

Hii mipasho inachekesha sana...basi tu
 
Serikal imemomba radhi kwa kumsingizia ugaidi? Wewe kada hunaga hoja kabisa na ndo mnaomharibia Mbowe mali yake yaani CHADEMA. Ungekuwa mzalendo kwa kukemea Mbowe alipoleta mambo ya ubara na uzanzibari kwenye ishu ya Bandari. Kabla ya kupost uzi uwe unafikiria kwanza sio kukurupuka.
 
Hebu uliza moja basi usaidiwe , unataka la Nape au la Lowassa ?
 
Serikal imemomba radhi kwa kumsingizia ugaidi? Wewe kada hunaga hoja kabisa na ndo mnaomharibia Mbowe mali yake yaani CHADEMA. Ungekuwa mzalendo kwa kukemea Mbowe alipoleta mambo ya ubara na uzanzibari kwenye ishu ya Bandari. Kabla ya kupost uzi uwe unafikiria kwanza sio kukurupuka.
Hujui kitu wewe
 
Wabunge wa Tanzania ni aina flani ya watu ambao hawana uchungu na taifa wao wana uchungu na chama chao na tumbo zao, haiwezekani wabunge wote wawe sawa kwenye hili
Mmmh, hiki ndiyo kipimo halisi. CHADEMA walilewa na maridhiano wakaamini kuwa watapata dola kama mgawo wao wa maridhiano.
 
Back
Top Bottom