herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,364
Ni kweli Watanzania walio wengi wanapenda sana udaku udaku haya ni mambo ambayo siyo muhimu kabisa katika kujitafutia maendeleo, hata mkipinga hapa huu ni ukweli.
Hata rais Magufuli naye anajua hili ndiyo maana alisema siku ya jumatatu uzinduzi wa ujenzi flyover ya Ubungo.
Namnukuu "Tumejielekeza mno katika masuala ya udaku ambayo hayatuongezei chochote, hayatusaidii chochote na ndio yanachukua muda wetu mwingi.
Zipo hata tafiti rasmi zinathibitisha hili moja ilihitimisha kuwa ni Watanzania wengi hawapendi kusoma vitabu na magazeti ya msingi lakini wanapendelea sana kusoma magazeti ya udaku hili hata ukifanya kauchunguzi kidogo tu utabaini kaulize muuza magazeti ni yapi yanaisha kwa haraka atakujibu udaku.
Mijadala mingi ni matukio, fulani kafanya hivi yule vile, yule siku hizi hasalimii anhaa si wajua kapata ajira!
Kiongozi akikosea na kama kweli ushahidi upo watu wenye akili timamu hawaishii tu kusema sema wanachukua hatua kumuwajibisha ili mambo mengine ya kimaendeleo yafanyike, mataifa yaloendelea ya dunia ya kwanza wamefankiwa na wanazidi kufanikiwa kwa kufanya hivyo.
Kila mtu inatakiwa awe na dira/malengo kwenye maisha yake, taasisi vilevile hata taifa pia lazima liwe na dira siyo kwenda kwenda tu hovyohovyo kwa kuyafanya matukio ndiyo agenda/dira.
"Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people"