Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Kuanzishwa kwa makampuni ya ulinzi SUMA JKT GUARDS na CHINA-TANZANIA SECURITY kunakwenda kuuwa kabisa makampuni binafsi ya ulinzi hapa nchini. Sababu SUMA JKT -wamehodhi kulinda ofisi zote za serikali, mashirika ya uma na taasisi zake . CHINA-TANZANIA SECURITY-wamehodhi kulinda miradi yote ya wachina na inayofadhiliwa na serikali yao. Wakati huo huo makampuni ya ulinzi ya kigeni wamehodhi kulinda makampuni yanayotoka kwao na kwenye ofisi zote za kibalozi. Sijui hawa wenzangu na mini watalinda wapi, labda kwenye hivi vijumba vyetu mbavu za mbwa, na vibaa vyetu uchwara ambako malipo yao ni kidogo sana na hayalipwi kwa wakati
TAFAKARI