Nakerwa na neno hili "MPIGA DILI"

Mzee Chapuuka

Member
Apr 21, 2017
97
243
Wasalaam
Najua kila mmoja humu ni shahidi
Tangu utawala huu wa awamu ya 5 uingie madarakani na kushindwa kuboresha maisha ya watz wengi hasa wa hali ya chini kuna haka kamsemo "wanaolalamika walikua WAPIGA DILI" ushakua wimbo wa Taifa
Kwa hiyo kila mtanzania anaelalamika kupanda Kwa bei ya sembe,sukari,kukosa ajira,huduma mbovu za jamii(elimu &afya) nao ni walikua wapiga dili,vijana wa familia maskini waliosomeshwa Kwa tabu ili baadae waikomboe familia yao lakini baada ya kuingia huu utawala wakabana ajira zote na fedha mtaani kijana akakosa cha kufanya nae ni mpiga dili
Kama hazina hakuna fedha za kuingiza mtaani kwenye mzunguko waseme Tu kuliko kupakazia kila mwananchi anaelalamika fedha mtaani ngumu kwamba alikua mpiga dili
Kazi zinafanyika tena halali lakini unakuta malipo ni Kwa mbinde hasa huku private mtu ukiomgea hali halisi unaambiwa mpiga dili
Inaboa Sana .
 
yaah huu msemo hata mie unanikera ukilalamika kuhusu life kuwa ngumu unaambiwa unajua mmezoea kwa sababu wapiga dili wamebanwa sasa Mimi ni fundi simu kuna upigaji dili gani kwangu??
 
Mkuu kama wewe sio mpiga dili kwanini unaumia!
anaumia kwa sababu uchumi unakua kupitia makaratasi
lakini kivitendo hamna kitu

uchumi wetu umekua kwenye karatasi
mzunguko wa pesa uko vibaya sana hadi huruma
hospitali hakuna madawa sukari bei juu sembe bei juu kodi lukuki ambazo zinawafanya wafanya biashara wachukie biashara
 
Shida yetu WaTz ni kushabikia kila kiongozi anachoamka nacho eg Mwl (Uhuru na kazi, ujamaa na kujitegemea)
Mwinyi (Ruksa, ufagio wa chuma etc)
Mkapa (mtaji wa maskini ni nguvu, ukweli na uwazi)
Kikwete (Nguvu, ari na kazi mpya, maisha bora kwa kila MTz etc)
Na sasa mara wapiga dili sijui na nini!! Hua tunashabikia bila kujihoji neno (kauli mbiu) inatuvushaje kama nchi bali ushabiki
 
Halafu eti ukitaka maisha mazuri "fanya kazi". Hivi wenye maisha ya shida wote hawafanyi kazi?
 
Back
Top Bottom