Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Aleji ni ugonjwa?
Na hutibiwaje kama ni ugonjwa au sio ugonjwa?
Mfano-kutokwa na viuvimbe kichwan vinavyojaa tunga usaa asili ya ring worm ni aleji au na kiasili hutibiwaje?
 
Mkuu salito,Hali ya mkeo kula udongo na mchele mbichi kipindi cha ujauzito ni carving inayotokana na ujauzito.Ni aghalabu kushauri tiba kwa wajazito kama wanaafya njema na wanatatizo kama la mkeo.Mjamzito anapaswa apate tiba pale tu inapoidi kwa sababu afya yake ni muhimu na ugonjwa wake unaweza kuwa na madhara kwa mtoto.Ningependa kama ungefunguka zaidi je mkeo ana washwa ukeni?amekuwa mwekundu kwenye eneo la uke?

Hapa nilivyomuelewa jamaa.......anamaanisha kitu kama pica........ mkewe si mjamzito.......
 
Last edited by a moderator:
naomba kujuzwa candidas creams zinavofanya kazi kutibu fangus
Kila dawa ina mechanism yake of action kutokana na group ya dawa lilopo.

Mfano dawa kama clotrimazol ni fungicide.

Maanake inaua hao fungus kwa kuzuia eregestrogelsythesis hatimae kuweak umbo la cell membrane ya fungus.
 
Sikio linauma kwa ndan mkuu ila sio lile la kutoa usaha hapana linauma tu
Nenda kwa daktari akufanyie uchunguzi mimi siwezi kujua una tatizo gani ukisema sikio linauma tu kwa ndani inawezekana ngoma ya sikio ina tatizo na since hutoki usaha huna infection.
 
ulcers. nitumie dawa gani
Ni muhimu ufahamike una ulcers ipi mkuu na hilo linajulikana kwa vipimo vya maabara kama ureasetest,cultures na gastroscopy.
Kuna Gastroesophageal reflux disease(GERD) inasababishwa na vitu vilivyopo kwenye tumbo kwenda kwenye oesophagus.Kwasababu muscle kati ya tumbo na oesophagus imelegea.Hali hio inasababisha mucosa ya esophagus kupata majeraha na mtu anapata symptoms za regurgitation na heartburn.
  • Ukiwa na mild syptoms tiba ni ANTACID (ACID NEUTRALIZERS) kama sodium bicarbonate,magnesium/aluminium hydroxide na
  • Moderate to serious symptoms tiba ni PROTONPUMPINHIBITORS mfano pantoprazole au HISTAMIN( H[SUB]2-[/SUB]ANTAGONISTS) mfano ranitidin
PEPTIC ULCERS DISEASE inasababisha vidonda kwenye mucosa ya tumbo inayosababishwa na acid inayotoka kwenye tumbo.Damage katika utumbo inatokea pale balansi kati ya production ya acid na factors zinazokinga mucosa zinapishana.Bacteria kama H.pylori na matumizi ya muda mrefu ya NSAID´s (non-steroid antiinflammatory drugs)unbalance niloiongelea hapo juu.
Dawa zinazoweza kutibu peptic ulcers disease ni
  • PROTONPUMP INHIBITORS kama(pantoprazol,esomeprazol,omeprazol) na hii inatumika ukiwa na ulcers inayosababishwa na H.pylori na NSAID´s.

  • ANTIBIOTICS pia inatumika pamoja na protonpumpinhibitor kutibu ulcers inayosababishwa na H.pylori.Inakuwa antibiotic mbili clarithromycin +metrodinazole/amoxicillin(Helicokit)
 
Ni kiwango gani cha haemoglobin mwanaume hutakiwa kuwa nacho ktk damu? Na ferroton capsules husaidiaje kuongeza wingi wa damu?
13,4 - 17,0 g/dL ikiwa pungufu ya 13 utakuwa na iron deficencey anemia.Ferroton capsules vina Iron kwa kula hivo vinaongeza wingi wa ferritin mwilini,tukiwa na mapungufu ya iron mwilini,Vitamin B[SUB]12[/SUB],Folic acid na erytropoietin inasababishwa mapungufu kwenye hemoglobin synthesis.
 
13,4 - 17,0 g/dL ikiwa pungufu ya 13 utakuwa na iron deficencey anemia.Ferroton capsules vina Iron kwa kula hivo vinaongeza wingi wa ferritin mwilini,tukiwa na mapungufu ya iron mwilini,Vitamin B[SUB]12[/SUB],Folic acid na erytropoietin inasababishwa mapungufu kwenye hemoglobin synthesis.

Asante mkuu nmeridhika, je anemia husababishwa na nn, na haemoglobin level ikiwa chini ya 13 g/dl kuna madhara gani? Asante
 
nashukuru sana nina maswali 31.Nini tofauti kati ya Diabetes type-1 na diabetes type-22.Je kwa nini mtu mwenye diabetes type-2 anashindwa kufanya vizuri tendo la ndoa na nini dawa yake3.je kama tatizo limesababishwa na over weight je akipunguza tatizo linakuwa limeisha?au kuna dawa anatakiwa kutumia pia
Hello chasuzy!
  • Diabetes type 1 inasababishwa na mwili kutokuwa na production ya insulin,hali hii mtu anazaliwa nayo na inaweza kuwa genetic pia.Wagonjwa wa diabetes type 1 wanahitaji sindano za human insulin.Diabetes type 1 haina tiba unatakiwa uchome sindano ya insulin maisha yako yote.


  • Diabetes type 2 wanakuwa na production ya insulin lakini si ya kutosha.Kitu kingine ni insulin resistance( jinsi unavyokula vyakula vya sukari/unhealthy ndivyo mwili unajaribu kuproduce insulin ili kuvunjavunja hio sukari na baada ya muda kwasababu ya overproduction uzalishaji wa insulin inapungua),mapungufu ya insulin receptors,matatizo ya insulin binding au insulin receptor haipati signal za kutosha.Diabetes type 2 unaweza kupona ukibadili lifestyle kwa kula vyakula healthy,kufanya mazoezi,na kujitibu ipasavyo.Usipofata tiba kwa uyakinifu unaweza kupata complications kwenye viungo vingine kwasababu sukari inaathiri nerves na mishipa ya damu mfano ya macho, pia mafigo.Kitu kingine ni pia wenye diabetes type 2 wanaweza kuworsen na kwenda kwenye diabetes type 1 kwasababu uzalishaji wa insulin unapungua na hatimae kupotea kabisa.


  • Nimegusia complication za diabetes kuwa zinaweza kuathiri nerves na mishipa ya dam na inahusiana na mishipa ya uume, ya miguu na kusababisha (diabetic foot)-unakosa sense kwenye miguu kwa sababu nerves ziko damaged au kuathiri mishipa miyembamba ya dam ya macho na kupeleka kutokuona vizuri hatimae upofu.


  • Insulin ni hormone inayotengenezwa kwenye pancreas.Kwa lugha nyepesi naweza kusema ni ufungo kwasababu insulin inasafirisha sukari kutoka kwenye damu na kwenda kwenye cells za mwili.Na pia inavunjavunja glucose to glucagon.
insulin.jpg
 
Asante mkuu nmeridhika, je anemia husababishwa na nn, na haemoglobin level ikiwa chini ya 13 g/dl kuna madhara gani? Asante
Mkuu anaemia zipo aina tofauti kama nilivyokujibu awali inaweza kusababishwa na blood loss(mfano kutokana na kujifungua, vidonda vya tumbo, matumizi ya baadi ya dawa n.k), mapungufu ya uzalishaji wa chembechembe nyekundu za dam(mf. erytropoetin hormone inayotengenezwa kwenye figo ili kustimulate uzalishwaji wa chembechembe nyekundu kutoka kwenye bone marrow haiwajibiki ipasavyo) au kuharibika kwa chembechembe nyekundu za dam kwasababu zinatengenezwa zenye kasoro(sickle cell anemia) !

Haemoglobin ikiwa chini ya 13g/dL cells za mwili hazitopata oxygen ya kutosha.Na dalili mojawapo ni mwili kuchoka ni kwasababu viungo vya mwili vinakosa mahitaji muhimu ili vifunction ipasavyo.
 
Back
Top Bottom