Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Hv Nurobion zinatibu nin na matumizi yake yakoje kadhalika nn dawa ya kufa ganzi kwa mikono na miguu
Hello Gilbert Lekelaho,Neurobion ni multivitamin tablets yenye supplements za Vitamin A ,Vitamin C,Vitamin D,Vitamin E ,Thiamin (B1) Riboflavin (B2),Niacin ,Vitamin (B6), Folate ,Vitamin B12 na Fluoride (as sodium fluoride).

Hii dawa inatumika kwa watu wenye mapungufu ya nutrients mwilini ili usipate deficiencies za vitamins tofauti.
 
Last edited by a moderator:
human papilloma virus , je ugonjwa huu unatibika , na je chanzo chake nini??
Human Papilloma Virus ni ugonjwa unaotokana na maambukizi ya virusi.Virusi hawa wamegawanyika kwenye group la virusi 120 ambao wanaweza kusababisha warts kwenye maeneo tofauti ya mwili kama vidoleni, miguuni n.k virusi 40 wa kundi hili wanaambukizwa kupitia kwenye sexual contact.

Maambukizi yanatokea kupitikia mgusano wa ngozi(skin to skin contact)kwahio hata condom haisadii kujikinga na ugonjwa huu.Ugonjwa huu hauna hatari kiafya na mara nyingi huondoka wenyewe baada ya miaka 2 kati ya asilimia 80 ya watu wazima wanao.

Ugonjwa huu unaweza kusababisha cancer ya shingo ya kizazi kwa wanawake ambao wanabadilisha sana wenza,inaweza kusababisha vilevile cancer ya uume, haja kubwa na kuendelea.

Ipo chanjo ya kujikinga na ugonjwa huu inayokinga na HPV 16 & 18 ambayo husababisha cancer ya shingo ya kizazi.Tiba nyingine ukishapata ugonjwa huu ni dawa ya kupaka iwapo una warts(podophyllotoxin/imiquimod)
 
Samahani dr, nina mtoto wa miezi mitatu anatatizo la kushtuka mara kwa mara akilala, tatizo hilo linatatuliwaje? Asante
 
Naomba kujuzwa nitumie dawa gani ili macho yangu (white layer) yawe meupe, situmii sigara wala kilevi chochote,
 
mimi kijana wa miaka 28 nina tazizo la kutoona mbali kwa sasa natumia miwani naweza pata tiba au nifanye nini ili nipone?
 
Halo Daktar,hili tatizo LA nyama za pua kusababisha MTU kukoroma sana nyakat za usiku ni Nn tiba yake
 
Halo Daktar,hili tatizo LA nyama za pua kusababisha MTU kukoroma sana nyakat za usiku ni Nn tiba yake
Inategemea na ukubwa wa hivo vinyama njia tofauti zinaweza kutumika mojawapo ni upasuaji na njia nyingine ni cortocosteroid kutibu eneo hilo locally au systemic so aidha ni prednisolon tablets au mometasone/budesonide nasal spray.
 
Hili tatizo la kuwa na kama michubuko kwenye ulimi (kuwa/kuhisi na kama muwasho flani wakati wa kula hasa dagaa) sababu yake ni ipi na tiba ni ipi? With thanks giving heart
 
Dr. mke wangu anatatizo la malaria ya kujirudia mara kwa mara tena inakuwa juu sana, huwa anachomwa sindano za quinine alafu anameza panado.

Nifanye nin dr. maana tunazngatia dozi vizuri tu na tumetumia ha mseto na sp pamoja na kutumia chandarua lakin tatizo linajirudia. Naomba msaada wako please!!
 
Samahani doctor mm mwanangu anakuwa anapata joto sana nimejaribu kutumia dawa hzi hapa amoxillin dry suspension na ya minyoo alatrol syrup lakn bado anajoto
 
Docta mimi nina tatizo la sikio upande wa kushoto,ilitokea tu wakati nimekaa basi hali ya km sikio moja linapoga kelele kama ya mluzi ivi!nilipojaribu kuziba la upande wa pili nikahic kelele nyingi kwenye sikio la kushoto na sikuweza kusikia kabisa mpaka hii leo nasikia kelele nyingi tuu bila sikio la upande wa kushoto kusikia kitu chochote!Naomba msaada wako doctor nifanyeje ili niweze kusikia tena
 
Dr tatizo langu nikiamka asubuhi nikiwa ninapiga mswaki huwa napata kichefuchefu na kuanza kutapika hadi nyongo NB mimi ni
wanaume na nimeshawahi kwenda hospita dr. akaniambia itakuwa minyoo nimetumia dawa nyingi bila mafanikio
 
Docta mimi nina tatizo la sikio upande wa kushoto,ilitokea tu wakati nimekaa basi hali ya km sikio moja linapoga kelele kama ya mluzi ivi!nilipojaribu kuziba la upande wa pili nikahic kelele nyingi kwenye sikio la kushoto na sikuweza kusikia kabisa mpaka hii leo nasikia kelele nyingi tuu bila sikio la upande wa kushoto kusikia kitu chochote!Naomba msaada wako doctor nifanyeje ili niweze kusikia tena
Hellow alec4ril,
Una tatizo linaitwa "tinnitus",ni kusikia kwa sauti zenye milio tofauti kwenye sikio bila ya kuhallucinate.Hizo sauti zinaweza kuwa na intensity tofauti na zipo tofauti kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwengine.Huu si ugonjwa bali ni dalili ya vitu tofauti kama mwanzo wa kupoteza uwezo wako wa kusikia,una majeraha kwenye sikio au hauna msukumo mzuri wa damu kwenye eneo la ndani la sikio.Kama tatizo lako lipo zaidi ya miezi 6 ni "chronic tinnitus" ambayo inasababishwa na majeraha ndani ya sikio ambayo hupelekea kupoteza uwezo wako wa kusikia.Nakushauri ukaonane na specialist wa sikio ili igunulike chanzo cha hili tatizo lako ili upate tiba sahihi/ushauri nasaha.Kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:
Dr tatizo langu nikiamka asubuhi nikiwa ninapiga mswaki huwa napata kichefuchefu na kuanza kutapika hadi nyongo NB mimi ni
wanaume na nimeshawahi kwenda hospita dr. akaniambia itakuwa minyoo nimetumia dawa nyingi bila mafanikio
Kutapika nyongo kunasababisha kupatwa na kichefchef.Ukipiga mswaki usijisugue ulimi mpaka ujihisi kutapika.
 
Samahani doctor mm mwanangu anakuwa anapata joto sana nimejaribu kutumia dawa hzi hapa amoxillin dry suspension na ya minyoo alatrol syrup lakn bado anajoto
Kwanini unampa mtoto antibiotics na dawa za minyoo wakati ana joto tu?Joto ni dalili ya homa(fever).

Umempima joto na thermometer na ukajua ni degrees ngapi?

NB:Temperature ya mwili ya kawaida ni 37,5[SUP]o[/SUP]C.Temperature ikizidi degrees 38 hio ni dalili ya homa.Homa inaweza kusababishwa na vitu tofauti kama viral/bacterial infections,malaria n.k

Ili kushusha joto la mwili unapaswa kumvua nguo mtoto,muweke kitambaa cha maji baridi kwenye kichwa.

Temperature ikizidi 39 degrees mpatie paracetamol syrup/suppositories kutokana na uzito wa mtoto na umri.Fuata dosage sahihi.
Nakushauri uwe makini na kumpatia dawa mtoto bila kujua chanzo cha ugonjwa,antibioticis kama amoxicillin inaweza kumjengea resistence iwapo atapata maambukizi ya bacteria dawa hio haitofanya kazi mwilini kwasababu vijidudu vitakuwa vimeshajijengea mechanisms za kusurvive.

Ni vyema ukionana na daktari vilevile ili kuondoa utata juu ya suala hili.
 
Dr. mke wangu anatatizo la malaria ya kujirudia mara kwa mara tena inakuwa juu sana, huwa anachomwa sindano za quinine alafu anameza panado. Nifanye nin dr. maana tunazngatia dozi vizuri tu na tumetumia ha mseto na sp pamoja na kutumia chandarua lakin tatizo linajirudia. Naomba msaada wako please!!
Njia pekee ya kuepuka malaria ni kutokungatwa na mbu.

Chumba chenye baridi A/C kinakuwa na kiwango kidogo cha mbu.Wakati wa jioni ajaribu kuvaa nguo zinazoziba eneo kubwa la mwili ili usiwe exposed na mbu mfano avae nguo inayoziba mikono na miguu,asipende kukaa maeneo yenye giza na yaliyo karibu na mitaro/takataka kwasababu hapo mbu wapo wengi zaidi.

Zipo spray/roll on zenye DDT za kujipuliza/kujipaka mwilini ili asingatwe na mbu sina uhakika kama zinapatikana huko ni vyema ukiulizia famasi.
 
Back
Top Bottom