Najuta sana kuwakoleza kwenye mahusiano; kwa sasa inaniwia vigumu kuwaacha.

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,421
40,409
Nimekuwa kwenye mahusiano na michepuko kwa nyakati tofauti, na wote wanajua nina familia, ila kutokana na mazingira ya kuwajali na kuwa mchangamfu, wakajikuta wananogewa, na wengine mpaka wakaamua kunizalia.

Kwa wale walionizalia, nikawa nawapa nafasi ya mbali kidogo ili wasije kujipandisha cheo na kuwa mke, au kufanya mapinduzi kwenye ndoa iliyopo.

Kwa sasa nipo kwenye harakati za kuachana na michepuko, ili niweze kutulia na familia yangu, pamoja na kulea uzao wangu uliopatikana, bila kufanya mapenzi nje ya ndoa; kwa sababu uzee umeshanianza, na ndevu zimeshakuwa na mvi; wanasema simba mzee akizeeka, hata uwezo wa kuwinda hupungua.

Bahati nzuri, michepuko miwili imekubali matokeo kishingo upande, lakini ndio hivyo, kila kitu kina mwanzo na mwisho pia.

Waliobaki wawili, bado kukubali matokeo; kuna mmoja atajifungua hivi karibuni, ananiuliza ''utaniachaje mwanamke mzuri kama mimi, hujui mimi ni mzuri?'' Najaribu kumwambia nataka, nipate muda mzuri kwa ajili ya kuwekeza kwa hao wanaokuja.

Mwingine, chura matata, ni mke wa mtu; haelewi kabisa, na hataki kusikia mapendekezo yangu.

Nimebaki, kuwafariji tutaendelea na mahusiano; ila kiuhalisia akili yangu inaniambia sasa ni muda wa kutulia na familia yangu, kwa sababu umri unanitupa mkono.

Kweli umri mkubwa ni kuwa na busara.

Najuta sana kuwakoleza kwenye mahusiano; kwa sasa inaniwia vigumu kuwaacha.
 
mkuu mkeo nae umri umeenda? au ndo mna shift? isijekuwa wewe unapumzika na yeye anakolezwa huko nje
 
Kamwe usiseme hakuna anayemkoleza wife. Sema HUJAMWONA mtu anayemkoleza.

Usidhani unaweza kuwa na michepuko kadhaa mkeo asijue. Ila anaweza akajua akatulia kukuwekea heshima.

Lakini, kuna mwingine atajifanya kutulia saana, kumbe huko nje anajiacha kishenzi lakini kwa kujificha mno. Na huko nje akienda anatoa kama zote (mpaka vile ambavyo wewe huwezi kumfanyia wife)
 
Amekuzalia mtoto ?

Maana yake ni nini?

Kwamba amefanya surrogate mother?

Kwa hiyo huyo mtoto ni wako 100% yeye mama hahusiki?

Wakati wa kujifungua leba hakuonyeshwa?

Mtoto sio wa mama hata kidogo?!

Ingekuwa kuwa vyema kusema mmezaa mtoto au watoto na sio kusema nimemzalia mtoto, amekuzalia mtoto and the like !
 
Mke mwema anapaswa kujua njia za watu wa nyumbani mwake including mume wake.

Iwapo mume akiwa na michepuko ang’amue mapema na kuingilia kati,

Kinyume na hapo Sifa ya kuwa mke mwema inaondoka.

Imeandikwa; Mithali 31:10 nakuendelea

Mume anachepuka hadi kuzaa mke huna Habari uko tu kwenye “comfort zone “
 
Nimekuwa kwenye mahusiano na michepuko kwa nyakati tofauti, na wote wanajua nina familia, ila kutokana na mazingira ya kuwajali na kuwa mchangamfu, wakajikuta wananogewa, na wengine mpaka wakaamua kunizalia.

Kwa wale walionizalia, nikawa nawapa nafasi ya mbali kidogo ili wasije kujipandisha cheo na kuwa mke, au kufanya mapinduzi kwenye ndoa iliyopo.

Kwa sasa nipo kwenye harakati za kuachana na michepuko, ili niweze kutulia na familia yangu, pamoja na kulea uzao wangu uliopatikana, bila kufanya mapenzi nje ya ndoa; kwa sababu uzee umeshanianza, na ndevu zimeshakuwa na mvi; wanasema simba mzee akizeeka, hata uwezo wa kuwinda hupungua.

Bahati nzuri, michepuko miwili imekubali matokeo kishingo upande, lakini ndio hivyo, kila kitu kina mwanzo na mwisho pia.

Waliobaki wawili, bado kukubali matokeo; kuna mmoja atajifungua hivi karibuni, ananiuliza ''utaniachaje mwanamke mzuri kama mimi, hujui mimi ni mzuri?'' Najaribu kumwambia nataka, nipate muda mzuri kwa ajili ya kuwekeza kwa hao wanaokuja.

Mwingine, chura matata, ni mke wa mtu; haelewi kabisa, na hataki kusikia mapendekezo yangu.

Nimebaki, kuwafariji tutaendelea na mahusiano; ila kiuhalisia akili yangu inaniambia sasa ni muda wa kutulia na familia yangu, kwa sababu umri unanitupa mkono.

Kweli umri mkubwa ni kuwa na busara.

Najuta sana kuwakoleza kwenye mahusiano; kwa sasa inaniwia vigumu kuwaacha.
ZERO IQ anakutafuta washa simu
 
Back
Top Bottom