Najuta sana kubeza watetea mifumo imara

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Nilipowaona wanaharakati wakipambania Katiba mpya ili kama Nchi tuwe mifumo imara na sikutegemea mtu mmoja niliwananga!

Aliposimama Mbowe kutukumbusha kuhusu uhuru na wajibu nilimuona hayawani.

Nilipomuona Tundu Lissu akitokwa na povu akililia Nchi kuwa na mifumo imara nilimpuuza na hata alipopigwa risasi nyingi nilishangilia.

Watetea mifumo imara wote niliwabeza na hata walipodhulumiwa haki zao nilicheka.

Kwa dhati ya moyo wangu najutia hayo yote na naomba radhi kwa Mungu wangu na wote niliowafurahia kwa mabaya.

Punde, natarajia kuchukua mkondo na imani nyingine.

Amina.
 
Nilipowaona wanaharakati wakipambania Katiba mpya ili kama Nchi tuwe mifumo imara na sikutegemea mtu mmoja niliwananga!

Aliposimama Mbowe kutukumbusha kuhusu uhuru na wajibu nilimuona hayawani!...
Bado siamini haya madudu yamefanyika chini ya utawala wa JPM, mbele ya hawa Wasaidizi wake sasa walikuwa wanamsaidia nini?

Serikali nzima inawajibika kwa hili, maana walikuwepo wote kwenye kupiga makofi na vigelegele kwenye kuzindua na kuzindua huku wakijua wanazindua machungu kwa watanzania.

Inauma Sana, sana.
 
Bado siamini haya madudu yamefanyika chini ya utawala wa JPM, mbele ya hawa Wasaidizi wake sasa walikuwa wanamsaidia nini?. Serikali nzima inawajibika kwa hili, maana walikuwepo wote kwenye kupiga makofi na vigelegele kwenye kuzindua na kuzindua huku wakijua wanazindua machungu kwa watanzania. Inauma Sana, sana.
JPM alikuwa sawa asilimia 1000 sema alizungukwa na mashetani.
 
Usijute sana, majuto yako hayataisaidia nchi chochote badala yake washawishi makada wenzako kama johnthebaptist YEHODAYA mama D FaizaFoxy Waberoya Pulchra Animo Ruttashobolwa cocochanel Statesman waone umuhimu wa kupata katiba mpya na wao waongeze nguvu kupaza sauti ya katiba mpya ambayo watawarithisha watoto na wajukuu wao kwa taifa imara, lenye haki sawa na linalotoa fursa sawa kwa wote.
Umemsahau Kawe Alumn

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Bado siamini haya madudu yamefanyika chini ya utawala wa JPM, mbele ya hawa Wasaidizi wake sasa walikuwa wanamsaidia nini?. Serikali nzima inawajibika kwa hili, maana walikuwepo wote kwenye kupiga makofi na vigelegele kwenye kuzindua na kuzindua huku wakijua wanazindua machungu kwa watanzania. Inauma Sana, sana.
UKIELEWA HILI UTAJUA KILICHO MSIBU JPM:

Stalin baada ya kifo chake alirithiwa na Nikita Khrushchev., Siku mmoja akiwa ana hutubia Kamati Kuu huku akipinga sera nyingi ya mtangulizi wake, Mjumbe mmoja bila ya kujitambulisha alikereka na akamundikia ki note cha kumshutumu na kumlaumu, "we Nikita ulikua msaidizi wa Stalin, "kwa nini hukusema haya kipindi hicho Stalin akiwa hai?"

Khrushchev akakisoma na akaomba Mjumbe aliye andika anyooshe mkono juu amtambue ili amjibu .Hakuna mkono uliyo nyooshwa, Khrushchev akasema "kinacho kushinda wewe kunyoosha mkono leo , ndo hicho hicho kilicho nishinda mimi kusema enzi hizo"

KIONGOZI WA ENZI ZA MAWE ALIPATA FURSA KUTAWALA ENZI ZINAZOONGOZWA NA TAARIFA.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Nchi inapata shida sababu moja tu, hakuna taasisi Imara zitazoongozwa na katiba bora, zitakazozaa uongozi bora.

Watanzania tungekuwa na akili tungeidai katiba mpya inayoendana na mahitaji na matakwa ya nyakati hizi kwa nguvu zote, Sema kuna watu walioshikilia "mpini" hawatakubali afe kipa afe beki.
 
Back
Top Bottom