Ngao Ya Imani
Senior Member
- Nov 14, 2013
- 172
- 510
Hapa ndipo unapoonekana aidha unafiki au udhaifu wa toba yako. Iweje useme mwendazake alikuwa sahihi 1000% kama:JPM alikuwa sawa asilimia 1000 sema alizungukwa na mashetani.
- Alikuwa anatamka hadharani kuwa yeye hashauriwi na kama ukimshauri ndio umeharibu kabisa
- Alitengeneza mpasuko mkubwa kijamii kupitia siasa chafu za kibaguzi
- Aliwapa watu vyeo kishkaji na kijamaa pasipo kuzingatia weledi na ufanisi.
- Alifumbia macho mauaji, mateso na kupotea kwa critics wa serikali walioshindana kwa hoja.
List ni ndefu mno.
Wewe kusema kuwa unatubu kwa kuwabeza watetea mifumo imara wakati huo bado aliyekuwa mstari wa mbele kunajisi kila mfumo unamuona alikuwa sahihi binafsi naona ni unafiki uliovuka viwango