Najuta kuzaliwa

Najuta kuzaliwa

ulaya12

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2017
Posts
834
Reaction score
909
Huwa ninajiuliza hadi nakosa jibu labda wenzangu mtanisaidia,wazazi wangu ndiyo walifanya mipango hadi mimi wamenizaa wakati huo mimi wala hawakunishirikisha na nilipokuwa mtoto walinijali sana kila kitu walikuwa wananihudumia hadi nimeanza kupatapata akili walikuwa wananijali sana namimi nikayaona maisha ni mazuri sana,lakini nashangaa miaka ilivyokuwa inasonga nao wamenitelekeza sipati huduma kama zamani wanasema nijitegemee yaani maisha yamekuwa magumu kupita kiasi naona hapa wameniingiza mkenge kwanini wanifanyie hivi wakati mimi sikuwaomba wanilete huku duniani wangeniacha hukohuko walikonitoa hapa hawajanitendea haki kabisa" nawasilisha
 
Pambana na hali yako mkuu. Watu wanahali mbaya kuliko wewe. Maisha ni vita chalii.

[HASHTAG]#olewakouandamane[/HASHTAG]
 
Inatakiwa ushukuru ,tatizo no wew wala siyo wazazi wako,jiulize kwanin wenginw wapo vile na Mimi Niko hivi,jitathimin chukua hatua,mawazo yako ndiyo unayoyaishi komaa
 
Mshukuru Mungu kwa kila jambo, amini kuna ambao wanatamani hiyo pumzi yako saa hii hata waseme asante Mungu wanashindwa!!
 
Huwa ninajiuliza hadi nakosa jibu labda wenzangu mtanisaidia,wazazi wangu ndiyo walifanya mipango hadi mimi wamenizaa wakati huo mimi wala hawakunishirikisha na nilipokuwa mtoto walinijali sana kila kitu walikuwa wananihudumia hadi nimeanza kupatapata akili walikuwa wananijali sana namimi nikayaona maisha ni mazuri sana,lakini nashangaa miaka ilivyokuwa inasonga nao wamenitelekeza sipati huduma kama zamani wanasema nijitegemee yaani maisha yamekuwa magumu kupita kiasi naona hapa wameniingiza mkenge kwanini wanifanyie hivi wakati mimi sikuwaomba wanilete huku duniani wangeniacha hukohuko walikonitoa hapa hawajanitendea haki kabisa" nawasilisha
Naamini uliandaliwa kujitegemea, shule walizokupeleka na pia naamini walikupa na elimu dunia. Acha kulaani waliokuleta duniani, pambana, maisha si kuhudumiwa milele.
 
UMEONGEA UKWELI MTUPU IJAPOKUWA KUNA AMBAO WATAKAO KUPINGA ..TENA HAO NDIO WAPO WENGI MNOOO
 
Back
Top Bottom