Najuta kuwa Mtanzania!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Najuta kuwa Mtanzania!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkulima wa Kuku, Sep 17, 2011.

1. Mkulima wa Kuku

Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

#1
Sep 17, 2011
Joined: Jan 13, 2011
Messages: 1,259
Likes Received: 81
Trophy Points: 145
Kuna sifa kadhaa za kuwa mtanzania:1.ukisema tu ukweli unachukiwa na kuzushiwa...inabidi kila unachosema uwe mwongomwongo fulani hivi...mfano wa waziri wa nishati, alisema makali ya mgao yatapungua mwezi sept na kesho yake mgao ukaongeza makali
2. Inabidi usiwe makini kwenye lolote utaambiwa dikteta...ukichelewa kazini watakusifu, usipoperform utapendwa, ukiperform utaambiwa unajipendekeza
3. Inabidi uwe mchakachuaji - kwenye foleni lazima upite pembeni ndiyo utaonekana mwanaume, ukikutana na daladala usipowapisha watakutukana,
4. Inabidi uwe mwizi-usipoiba utaishije? Mshahara mdogo na unataka uishi maisha ya zaidi ya mshahara wako...utajengaje? Hakuna sera za mikopo nafuu ya ujenzi au ununuzi wa nyumba
5. Uabudu viongozi na kikubaliana na kila wanachosema -usipofanya hivyo utaitwa msaliti, mhaini, asiyependa amani, nk
6. U-support ccm- usipoisupport wewe siyo mwenzetu na huitakii mema nchi yetu. Hakuna atakayekupa nafasi ya kutumikia wananchi hata kama unazo sifa na wananchi wanakupenda. Kama huamini waulize wote walio kwenye siasa kupitia magamba kama inngekuwa hiari yao wangegombea kupitia chama hicho.
Nawasilisha toka bandani

2. HAZOLE

HAZOLE JF-Expert Member

#2
Sep 18, 2011
Joined: Feb 25, 2011
Messages: 1,333
Likes Received: 64
Trophy Points: 145
mkuu ni noma. najua umeongea kwa uchungu sana kutokana na mwenendo wa maisha yasiyoeleweka ya sisi wa tz na viogozi wetu. lakini pia najua kujua kama taifa halipo sawia ni kutazama majirani na wenzetu wanaishije. sisi tunakosa silaha mbili kuu za maendeleo
1. akili (plz si akili ya kufanya hesabu-hizi zipo ila km ya kusaini mikataba hovyo ni ukosefu wa akili, pia wananchi unaona gari, meli imejaa lakini unataka upande tu)
2. uzalendo-hapa ni kwamba hatupendani ktk minajili ya fursa za maendeleo. unaona tunajaa makanisani lakini kwenye mambo ya maendeleo wa tz tunafanyiana uchawi na wivu usio na msingi.

unahaki ya kujuta but mbwa ukishamjua jina hakupi shida. tunaenda enda hivihivi

3. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#3
Sep 18, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,971
Likes Received: 2,967
Trophy Points: 280
Pole kaka. Najivunia kuwa Tanzania, ila sijivunii kuwa Mtanzania kwani wageni wanathaminiwa kuliko wazawa.

4. pascaldaudi

pascaldaudi JF-Expert Member

#4
Sep 18, 2011
Joined: Mar 25, 2009
Messages: 534
Likes Received: 3
Trophy Points: 0
Mie kuna siku nilitamani akitokea mtu aniambie niukane uraia wangu ningekubali, Maana wafanyakazi walio wengi wa serikalini wamejaa rushwa, kujuana, kuogopana kwa vigezo vya usalama wa taifa, hivyo unakuta kwa ujumla mambo huwa hayaendi, na wanasiasa ndiyo kabisaa hakuna kitu, kila kukicha wanajiona wao ni miungu, eti walizaliwa kuwa watawala, hawasikilizi wananchi na kazi yao kubwa ni kujilimbikizia mali na kuhakikisha wanawaweka watoto wao kwenye idara nyeti za serikali. Kwa ufupi hata mie naichukia Tanzania na watanzania kwa sababu wananchi ndiyo wenye mamlaka ya nani awaongoze lakini wanaendelea kudanganywa na wao kukubali, CCM wametugawa kwa itikadi za dini (CUF-waislam, CDM-wakristu) kiasi kwamba kwa sasa muislamu ukimueleza mambo ya CDM ansema eti chama cha wakristu, na mkristu ukimuambia naye atasema CUF ni cha waislamu na watu eti wamekubali kuwa watumwa wa hizi fikra, basi CCM imebaki kazi yake kuzusha tu mambo na siyo kushughulikia matatizo yanayowakabili wananchi. Na sasa CDM ni cha wachaga. Inauma sana!!

5. Mabagala

Mabagala JF-Expert Member

#5
Sep 18, 2011
Joined: Nov 27, 2009
Messages: 1,465
Likes Received: 42
Trophy Points: 145
Mimi siku zote nalia na polisi. hii taasisi imeoza kwa rushwa

6. K

Kicheruka JF-Expert Member

#6
Sep 18, 2011
Joined: Feb 2, 2009
Messages: 791
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
Tatizo kubwa ni: 1. utawala watu wang'ang'ani madaraka ili waibe na kujilimbikizia na uwezo wa kutawala na kuongoza hawana 2. Watanzania ambao ndio wenye nchi hatutambui tufanye nini kuleta mabadiliko kwani wasomi walio wengi ni ndumilakuli kila siku kujikomba wapate nafasi za kuteuliwa ili kuwalinda hao watawala wabovu, na wananchi wa kawaida kutwa kushabikia ujinga wa wanasiasa na kuuza kura kwa tshirt, kanda na pilau

7. Mbugi

Mbugi JF-Expert Member

#7
Sep 18, 2011
Joined: Jan 7, 2011
Messages: 1,488
Likes Received: 100
Trophy Points: 160
wakulaumiwa wazazi nafikiri walipaswa kukuzalia kati ya somali, irak, libya, nigeria, maana nadhani ungekuwa sasa uko juu sana

8. T

Topical JF-Expert Member

#8
Sep 18, 2011
Joined: Dec 3, 2010
Messages: 5,176
Likes Received: 11
Trophy Points: 0
Omba green card, wenzako wale watu wa complain sana wako nje wanaadika tu kwenye forums..grassroots hawapo

Loading...