Namshukuru Mungu kwa jinsi alivyonisaidia kuweza kujua mambo mengi ya maisha.Sasa wewe na wengine mnaokata tamaa kwa sababu eti mmesoma na hampati kazi kwa wakati mnaotaka nyie,mlishawahi kuwafikiria wale ambao waliishia darasa la saba au form4 wanaishi je?
Kabla hujalalamika je ulishawahi kujiuliza ni wapi walikuambia ukisoma mpaka chuo basi wewe ni uhakika utapata kazi?Ni kweli Jua linachomoza mashariki na kuzama magharibi hii ni universal law,je wewe kupata kazi kuna sehemu ulihakikishiwa?
Sasa kwa nini ukate tamaa kwa vitu ambavyo huna control navyo,pia kusoma chuo si issue kwani siku hizi vyuo ni vingi na quality yake siwezi sema.Sometimes huwa nawambia watu utajua kama course uliyosoma au chuo ulichosoma ni kizuri ukimaliza chuo.Vyuo ni vingi so mtu akiniambia amesoma mpaka chuo mimi hainifanyi nitetemeke kwamba anaweza sana au anaufahamu mzuri,it all depend on an individual effort.
Mengine hatuwezi sema ni aibu soma kwa makini magraduate wanavyo omba msaada hapa kwa mambo ambayo wanaweza yamaliza wenyewe.Seriously watu wengi hawajui kutumia internet,wanachojua ni kupost kuomba msaada na wakati wanaweza wakapata hizo information online.Sasa type hii ya generation inalalamika sana lakini haijitumi kabisa.
Fuatilia misaada na maswali yanayoulizwa then jiulize je hili mtu hawezi lipata online?
Tunarudi kulekule kwa kuandikiwa barua ya kuomba kazi na kuitumia pasipo kujua hata maneno yaliyotumiwa yanamanisha nini.
Kuna CV za watu ziko kimya namanisha unasoma CV ya mtu hata haina ushawishi wa kumwajiri huyo mtu imepoa,hapa unaweza usinielewe kama .. wako ni ....Ila kuna CV zimepoa,ziko kimya hazina mvuto hata wa kutaka uonane na huyo mtu na hizi ni nyingi.
Kwa sababu tunasoma ili tupunguze ujinga naamini kwenda shule siyo uhakika wa kuajiriwa so take it easy.Tumia elimu uliyopata kukuwezesha kupambana na maisha.
NB: "Ëducation is what remain after you have forgotten what you learnt in school" and
"There is no solution in complaining"