Najuta kupiga kura 2015, sitokaa nipige kura tena

Cdm walijichanganya wenyewe, si swala la wapiga kura..

Kumsimamisha edo kwenye nafasi ya uraisi ilikuwa ni sawa na kujarib kunywa soda yenye sumu huku umeahika kikombe cha maziwa ili kuondoa sumu...

Na hayo ndo matokeo wala c swala la kupiga kura
 
winners never quit, quiterrs never win. Kina Mandela wangekata tamaa apartheid ingeendelea kuwepo; mazingira ya kukata tamaa yalikuwepo lakini hawaku-give in. Soma " Long walk to Freedom" by Nelson Mandela
Asante mkuu umewakilisha wazo langu vizuri zaidi nilikuwa nahangaika kuandika kwa mtizamo wako.
 
Haijawahi kutokea CHADEMA wakakubali matokeo ya uchaguzi, haijawahi kutokea. Mwaka huu Lowassa aliwaambia kuwa atalinda kura yeye lakini cha ajabu sasa hivi analalamika wa kwanza. Ukweli ni kwamba Wananchi wameamua kumchagua Magufuli na ameshinda kwa haki kabisa. Hizo fomu zilizosainiwa na mawakala wenu zimetoka wapi???? Acheni kuipeleka nchi hii kwenye vita ninyi. Ukishindwa unakubali tu kushindwa basi maisha yanaendelea. Kama mlikuwa mnasoma posts zangu humu JF nilisema mimi Magufuli atashinda urais halafu CHADEMA watakataa matokeo kwa kisingizio wameibiwa kura. Tatizo lenu mnafikiri watu kujaa kwenye mikutano ya kampeni ndio matokeo ya kura. Niliwaambia mimi hapa hapa JF kama mnakumbuka, nilisema CCM ina mtaji mkubwa sana wa wapiga kura na itashinda. Unajua kwenye kampeni watu wengi wanajaa kutokana na hamasa tu ya kampeni lakini sio kweli kuwa watakupigia kura. Kingine nilichosema mimi ni vijana wengi sana under 18 kujaa kwenye mikutano ya UKAWA. Hawa vijana sio wapiga kura, lakini cha ajabu UKAWA hawakuliona hili, vijana waliokuwa wanajaza hii mikutano wengi wao ni wanywa viroba tu, ni vijana ambao hawakuwa serious katika kupiga kura. Matokeo yake wengi sana hawajapiga kura. Wameandikishwa watu millioni 22 lakini waliopiga kura hawazidi millioni 12, milioni 10 wote hawajapiga kura. Mimi hili nililijua tokea mwanzo kabisa ndio maana nilikuwa naandika kwa kujiamini kabisa kuwa Magufuli atashinda urais. Kingine ni kuondoka kwa Dk Slaa na Prof Ibrahimu Lipumba. Hawa viongozi hawakuondoka peke yao, waliondoka na watu wengi sana, hasa watu makini walikuwa pamoja nao. Amini nawaambia kama hawa viongozi wasingeondoka, leo hii Lowassa angekuwa anasubiri kuapishwa. Wapo mtakaobisha sana lakini huo ndio ukweli wenyewe. Mimi nakuambia hakuna kura iliyoibiwa. Sio rahisi kuiba kura kama mnavyofikiri. Magufuli ameshinda kihalali kabisa. Kitu kingine kilichomuangusha Lowassa ni kuongea kwa dakika mbili, Watanzania wanapenda mtu muongeaji, hawapendi mtu mkimya mkimya.
 
Marire ninavyokuheshimu sikutegemea kama utakuja na kitu cha hovyo kama hiki. Haya Zanzibar wanataka kurudia uchaguzi baada ya CUF kuonekana inaelekea kutwaa dola, say wewe ni Mzanzibar na ni member wa CUF, usingerudia kupiga kura?

Piga ili at last kila utetee kile unachokiamini, mwaka 2020 nikiwa hai nitapiga I wish nife CCM ikiwa haiko in power.( for the sake of my children and gradchildren's future)
 
Last edited by a moderator:
Siku zote mwenye upeo wa kufikili hawezi penda ccm wala kushabikia yani utakuta lijitu linasema tumeshinda ukimuliza anakuambia ccm tumeshinda alafu baada ya siku chache linaanza kulalama,
 
Kuna mtu kafuta picha tatu za mabox ya kura nimeweke kwenye huu uzi!!
Ni nani huyo
 
Yaani inauma sana. Wanatuhimiza kwenda kupiga kura wakati tayari wameshaweka maushindi yao mezani. Mlaaniwe ccm, mshukuru watanzania wapole
 

Natamani kulia haki ya nani. Naomba ulimwengu umuondolee heshima kikwete. Abakie ordinary kama akina Moi na Kibaki, asipewe majukumu yoyote ya kidunia na kiusuluhishi, awe ni rais mstaafu asiye na dhamani labda kwa ccm yake tu.
 
Last edited by a moderator:
ndugu yangu. Na kwa wale wote wenye mtazamo kama wako. Nawasihi msikate tamaa.

Demokrasia kwenye bara la africa bado sana lakini hatua kwa hatua itakuwa kama wananchi hawatokata tamaa.

Kwa sasa nchi za africa zina demokrasia ya unafiki. Ni tu kwa sababu wamelazimishwa na mataifa makubwa kufanya hivyo lakini bado tawala nyingi hazijawa tayari kufanya hivyo.

Mataifa makubwa bado yanaendelea kuwabana viongozi wa afrika kama vile baba anavyowabana watoto wake ili wakae kwenye mstari sahihi ama sivyo utachapwa viboko au utanyimwa chakula. Ndivyo hali ilivyo kwa sasa.

Kwa sasa mnaweza kuwa na hasira na kukata tamaa lakini kura yako katika uchaguzi huu ni ushindi mkubwa sana kwa wananchi kuelekea kwenye hatua inayofuata ya ccm kulazimishwa kukuza demokrasia ndani ya nchi yetu. Mtaona matukio haya ndani ya mwaka huu.

Hivyo, hima wananchi. Mmefanya kazi kubwa na nzuri kuelekea kwenye hatua nyingine ya kukuza demokrasia ndani ya nchi yetu na hivyo mnastahili kujipongeza badala ya kukata tamaa.

Endeleeni kuunga mkono mapambano ya msingi ndani ya taifa letu nayo ni kupata katiba mpya na mtaweza kufanya hivyo tu kama hamtakatishwa tamaa na yale yanayojiri kwa sasa.

Ikitokea ama uchaguzi wote unatakiwa kurudiwa au kuna jimbo uchaguzi unatakiwa kurudiwa basi tokeni kwa wingi ili muunge mkono upinzani badala ya kukata tamaa.

lazima tukate tamaa tunapigwa mabomu, tunatishwa na kutukanwa haina haja ya kupiga kura na viongozi wa ukawa nitawaona wanafiki kama watasusia matokeo ya uraisi tu na kukubali matokeo ya ubunge na udiwani. Viongozi wa ukawa wanatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kususia matokeo yote, kutohudhuria vikao vya bunge na mabalaza ya madiwanii na kutokubali kushiriki uchaguzi wowote ule mpaka kuwe na tume huru na katiba mpya itakayoleta fair ground na jeshi la police lisiwe chama cha siasa. Ama sivyo nitajua akina mbowe, tundulisu na viongozi wote wanalengo la masilahi binafsi ya posho na mapato yao binafsi. Naapa kutoshiriki zoezi lolote la uchaguzi tz hii kwa uendeshaji wa uchaguzi wa namna hii.
Lowasa simamia maamuzi magumu naamini katika maalim seif waliyoyafanya mwaka 1995 au 2000 kule zanzibar watayasimamia pia mwaka huu maana hata wao zenji wamedhulumiwa haki yao.
 
lazima tukate tamaa tunapigwa mabomu, tunatishwa na kutukanwa haina haja ya kupiga kura na viongozi wa ukawa nitawaona wanafiki kama watasusia matokeo ya uraisi tu na kukubali matokeo ya ubunge na udiwani. Viongozi wa ukawa wanatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kususia matokeo yote, kutohudhuria vikao vya bunge na mabalaza ya madiwanii na kutokubali kushiriki uchaguzi wowote ule mpaka kuwe na tume huru na katiba mpya itakayoleta fair ground na jeshi la police lisiwe chama cha siasa. Ama sivyo nitajua akina mbowe, tundulisu na viongozi wote wanalengo la masilahi binafsi ya posho na mapato yao binafsi. Naapa kutoshiriki zoezi lolote la uchaguzi tz hii kwa uendeshaji wa uchaguzi wa namna hii.
Lowasa simamia maamuzi magumu naamini katika maalim seif waliyoyafanya mwaka 1995 au 2000 kule zanzibar watayasimamia pia mwaka huu maana hata wao zenji wamedhulumiwa haki yao.

Nakubaliana na hoja yako kwamba itakuwa ni kuibaka demokrasia kama kura za urais zinabakwa halafu wabunge wa upinzani wanaingia bungeni. Na hapa tutajua mashujaa wetu wa kweli hapa Tanzania na wanafiki. Mbunge yoyote aliyeteuliwa kutoka kambi ya upinzani atakayetinga bungeni wakati kura za Urais zimebakwa basi huyo atakuwa Mbunge Mbakaji wa demokrasia ya nchi yetu.

Natoa jina rasmi la kutumika kwa wabunge wa upinzani watakaoingia bungeni katika mazingira haya waitwe WABUNGE VIBAKA (Wingi), MBUNGE KIBAKA (Umoja).

Maendeleo ya kukuza demokrasia niliyoyataja hapo juu yanaendana na kambi yote ya upinzani kususia SERIKALI KIBAKA ya CCM kama itapitishwa katika shughuli zote ndani jamii.
 
hii nchi kwa kura ccm haiwezi ondoka lazima watu tuje na njia mbadala hii ya kura for 25yrs ime prove failure
 
Natoa jina rasmi la kutumika kwa wabunge wa upinzani watakaoingia bungeni katika mazingira haya waitwe WABUNGE VIBAKA (Wingi), MBUNGE KIBAKA (Umoja).

Mbowe au Tundu Lissu walivyo na njaa ya pesa useme wasuse kuingia bungeni kisa kutokubaliana na Lowasa Kashindwa unaota wewe.Haiwezekani wataingia bungeni tena kwa mbwembwe
 
Back
Top Bottom