Marire
JF-Expert Member
- May 1, 2012
- 12,326
- 5,267
Wakuu
Huu uchaguzi umeniacha na majonzi sana!!!
Nawashangaa wanaoshabikia vyama vyao kushinda maana huku mtaani tumeshuhudia mabox ya kura na karatasi za kura za wizi zikizagaa kama njungu na tume haijatoa tamko lolote
Nchi imeingia kwenye gharama kubwa kwa ajili ya uchaguzi,chama cha siasa kama ccm wametumia gharama kubwa kwenye kampeni na kuwalipa wasanii ili hali mwisho wa siku kumbe wanakuja kuiba kura na kutoa matokeo ya uongo,kulikuwa na haja gani ya uchaguzi??
Jeshi la police wameagiziwa magari brand new 777 napiga hesabu ukigawa kwa kwa majimbo 264 kila jimbo linapata gari 2 na yatabaki cha kushangaza kuna jimbo halina ambulance hata moja wala kituo cha afya wala maji safi na salama!!
Kwa binafisi yangu sioni haja ya kuwa na vyama vya siasa wala kuwepo kwa kampeni maana zinagharimu pesa nyingi na maisha ya watu kama jimbo la nyamagana wameuana vijana wanne kwenye hizi kampeni...
Kwanini tusiwe na chama kimoja kama china???
Kama hali hii itaendelea sioni sababu ya kuwa na uchaguzi

Tuanze na hii quotation kwanza afu baadaye utajua namaanisha nini.
?I have never voted in my life... I have always known and understood that the idiots are in a majority so it's certain they will win.?
― Louis-Ferdinand Celine
TASFIRI
Sijawahi kupiga kura maishani mwangu....nimekuwa na uelewa kuwa walio wengi ni wapumbavu na ni lazima wapelekee ushindi
―Louis -Ferdinand Celine
Wapumbavu ni pamoja na wanaobadilisha matokeo ya kweli kuwa uwongo na ya uwongo kuwa kweli sitakuja kupiga kura Kama Tume itaendelea kuwa hii ya Lubuva hutakuja kamwe kuniona napanga foleni Kama katiba itaendelea kuwa hii hii ya Chenge.
Nipige kura ili iweje wakati badara ya kuokoa vuguvugu linarohatarisha uwepo wa Tanzania kule Zanzibar mnatuletea maigizo ya ziara za kushitkiza huu si mda wa kudunduliza Iman ya watanzania kwa serikari kwa ubadhilifu uliofanyika kipindi uchaguzi kwa kufanya ziara za kushtukiza?
Mh. Rais dk John P Magufuli ameanza kazi kwa mtindo wa ziara za kushitukiza ili kujionea ufanisi wa sekta mbalimbali hapa nchini .Mimi binafsi napongeza hili lakin ukiliangalia kwa undani si kweli kwamba Magufuli hajui kuwa Muhimbili wagonjwa wanalala chini, Ntashangaa Sana ukiniambia kwamba Magufuli alikuwa Hana taarifa kuwa Muhimbili mashine za kupigia picha ndan ya mwili( medical imaging) kama magnetic resonance imaging (MRI) ni mbovu?
Kiukweli ziara hizi za kushtukiza zina lengo la kurudisha Iman na Upendo kwa wananchi kwa serikari hasa baada ya uchaguzi mkuu uliomalizika October kujaa na mizengwe na utapeli wa hali ya juu (Racketeering of the highest order) hali iliyopekea siku ya kuapishwa raisi( inauguration) nchi kupoa Kama imemwagiwa uji.
Eti wewe Unadhan raisi alikuwa hajui kuwa muhimbili wagonjwa wanalala chin au muhimbili hakuna machine za kupigia picha ndani ya miili ya binadamu(medical imaging) ziara gani za kushtukiza wakat utendaji unafahamika.
Hembu tuache mazingaombwe Rais aliyemaliza mda wake yeye aliona suruhisho ni kupeleka magari ya kivita ili kutisha wanzanzibar na ww Mh unazani ziara za kushtukiza ndo zitaookoa muungano?
Siji kupiga kura Kama raisi wangu badara ya kuinusuru Zanzibar ambao ndo msingi wa Tanzania anaendelea kushitukiza sehemu ambazo utendaji wake unajulikana hembu tujiulize wewe umenunua maembe ukayaweka kwenye friji afu kesho uishitukize friji ili uone Kama maembe yamebadilika kuwa machungwa hahahhahaha tusitaniane ni dhahiri yatabaki maembe labda ukute yameoza ila ukitarajia kukuta machungwa ni dhahiri unahitaji daktari wa magonjwa ya akiri.
Kuna haja gani ya kupiga kura Kama Tibaijuka na Chenge wanarudi kuwa watetezi wetu bungeni nchi yangu Tanzania bana eti tunatetewa na kuwakilishwa na wezi.
Neno Tanzania lina Zanzibar ndani yake ni lazima tuiokoe Tanzania kwa kuinusuru Zanzibar kwanza.Hayo maigizo ya kufuta safari ya nini au hizo fedha mnataka mzihamishie kwenye uchaguzi mwingine aliousema Jecha au mnataka hizo fedha walipwe ma IT waliobobea kwa kuongeza kura ili yule mnayemtaka Zanzibar ashinde.
Labda kwa mbari ntaanza kujifikiria kupiga kura Kama hizi ziara za kimazingaombwe zitafanyika NEC na ZEC yani raisi ashtukize ZEC afu amuulize Jecha "aliyekwambia ufute matokeo wakati katiba haikuruhusu nani??" au ashitukize NEC afu amuulize Lubuva "aliyekwambia unitangaze Kama raisi wa Tanzania nani wakati kura za Zanzibar zilikuwa batili"
Pengine huenda nikabadirisha dhamira Kama Rasimu Ya warioba itasimamiwa mpaka ipite.
Au naweza nikashawishika kupiga kura Kama maneno aliyosema Nnape BBC kuhusu mahamaka ya mafisadi yawe ya uongo eti hatukuelewa waliposema mahakama ya mafisadi
Je na wewe hutakuja kupiga kura Kama Mimi au utapiga?
Sababu zipi zinazokupeleka uwe na maamuzi hayo je zinafanana na zangu au Una zako ni zipi hizo?
(Black days my country is crying����
KARIBU