Najuta kuoa mwanamke mlokole

Jaribu kumpa nafas nyingine kwanza huenda mambo yatakuwa kama utakavyo
 

Mi naona jaziba tu ndiyo zinazousumbua mkuu kwa kuwa anachokifanya hukipendi. Lakini ni bora mara mia afanyacho kuliko angekuwa anakuambia nipo nyumbani kumbe hayupo nyumbani au nipo kazini nimechelewa nivumilie kumbe yuko kwingine upande Fulani wa mji mkaao au nimesafiri leo nitarudi kesho kumbe yupo mahali furani ambako hawezi kukuambia na mengine na mengine (yote hayo mtoto atabaki na HG kumbuka!!!!).

Mi nakuomba ukubali kuwa umejaa jazba!!! kwa hiyo ili usaidike ondoa kwanza jazba na ufikiri vinginevyo utakuja kugundua kuwa umeoa mwanamke ambaye kwanza hukustahili kumuoa (yeye ameokoka wewe hujaokoka)na kumbe ni mke mzuri sana kwa mstakabali wa maisha yako na familia yako,

Mengine yote uliyosimulia hapa kama ni kweli yanazungumzika hasa ukiondoa jazba. Fikiria kidogo hapa kama kwa mfano asingezinduka kwa kipigo ulichokifanya kwake (pamoja na kujisifia kwako) ungekuwa jela na definitely ungefia hukohuko!!!! mwsho hivyo ulivyo ni matokeo ya yeye kuwa mke kwako kama utadhani natetea nisichokijua endelea na hako kamsimamo ulikoamua.

Muhimu sana msamehe halafu mshauriane kwa upole kwamba mfanyeje, nzuri Zaidi ni kwamba amekufuata na kutaka mazungumzo
 
Huyo kama ni kweli anafanya hivyo basi anahitaji kujifunza vizuri neno la Mungu
 
ndiyo mana mie siwezi kuoa mlokole maana walokole ndiyo malaya sana,,,,,,owa mwingine achana huyo

Completey rubbish. Walokole wa kweli, huwa wanajali familia na pia mambo ya Mungu pia. Yesu alisema, huwezi ukasema unampenda Mungu usie muona, wakati hauwajali wa nyumbani kwako. Asiye wajali wa nyumbani kwao ni mbaya na ameikana imani. Mungu ni wa utaratibu, kuna wakati wa kila jambo. Huyo mama itakuwa amepotoka na ahitaji msaada.

Lingine, unapaswa kuoa mtu mnafungamana imani, hilo lilikuwa kosa. Mngekuwa wa imani moja nafikiri ungeweza kumwelewa. Ninachokushauri, itisha kikao kati ya wewe, wazazi na pia mchungaji. Waeleze kila kitu, na mchungaji kama kweli ana hekima na ameitwa na Mungu atakuelewa. Haiwezakani kushinda kanisani kila siku asubuhi, mpaka jioni. Familia ndio kanisa la kwanza. Hii ndiyo torati ya kweli na manabii.Shalom
 

Kwanza pole! Neno la Mungu linasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.... Huyo dada na Familia yake wamekukosea sana Lk km Mkristo hayna budi kuwasamehe na kuendelea mbele maana ameshajifunza isitoshe hakuwa akifanya usaliti... Mungu ni Mungu wa Utaratibu kuna muda maalumu kwa ajili ya Mungu na Muda uliobaki kwa ajili ya familia na Kazi
 
Kwa maelezo yako na uwelewa wangu nianze na jinsi ninavyo kuona:
  • Mosi, unaelekeakuwa una wivu wa kupindukia kiasi kuwa hupendi mkeo atoke nyumbani hata kwa kwenda kanisani.
  • Pili una udikiteta fulani, ndani mwako ni amri tu hakuna mjadala (negotiation), Unalotaka ndilo linakuwa.
  • Una mapenzi ya kizamani ya kikurya ambayo yanahusisha kupigana pigana.
Ulipaswa kabla ya kuoa, uchunguze kwanza: Unataka mke wa kushinda kwenye baa au saloon ama kitchen party, maana hawa nao wapo ni wewe tu na upendeleo wako. Si rahisi kumbadilisha mtu mlevi akawa mlokole na mlokole akawa mlevi hivyo ulipaswa upate ready made kuliko kutransform. Mkeo, licha ya mapenzi yako ya kizamani ya kupigana pigana, amekusamehe, anataka mrudiane wewe hutaki. Maana yake huna roho ya msamaha. Waswahili husema 'Asiye samehe haliwezi penzi.' Kumbe wewe huwezi penzi ingawa unaweza kupanda.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kila mtu kuabudu imani aitakayo, lakini wewe unataka mkeo aabudu namna unavyotaka wewe, hivyo bila kujua, unataka kuwa juu ya Katiba ambayo ndiyo sheria mama ya sheria zote nchini. Masikini nduyu yangu hata hujui kuwa kuvunja Katiba ni kosa. Unaishi katika jamii ya watu wasiostarabika, wastaarabu huheshimu sheria zilizowekwa. Ni wanyama wa porini ndiyo wanaoishi kama unavyotaka wewe na mkeo muishi.
Sijazungumzia upande wa mkeo wala wazazi wake kwa sababu sijawasikia, lakini kubwa ni wewe uliyeomba ushauri na wao hawajaomba chochote. Ndoa ni taasisi inapaswa iheshimiwe na watu wote ukiwemo wewe mwenye ndoa. Mtu yeyote aliyemo kwenye ndoa hushawishiwa wakati wote na mtu mmoja mmoja vikundi vya watu marafiki mbalimbali wakike kwa wakiume, lakini wewe mwenye ndoa unapaswa kuwa na ushawishi mkubwa kushinda makundi yote. Tunapomshawishi mke hatumshawishi kwa mabavu, tunamshawishi kwa hoja huku ukinyunyiza juu yake UPENDO usiopatikana mahala pengine popote isipokuwa kwako tu
 
Asee umeeleza vizur sana ...wasiokuelewa nao watakuwa wametekwa akil Na pastor ...
 
Watu hawaoi wlokole wanaoa mke.ukioa ulokole fuata taratibu za ulokole ukioa mke pia fuata taratibu na makubaliano ya ndoa
 
Heheheee! Masimulizi yanahuzunisha ila presentation inafurahisha kwa kweli. Binafsi nahisi kama msipokua na mutual understanding baina yenu na maisha yenu, wewe ndio utakua kwenye upande wa kupoteza. Maana kupigana na mwanamke inaweza kukusababishia matatizo makubwa saana, unaweza ozea jela.

Maana hapo inaonesha kitu anachokifanya yeye na familia yake wanaona ni sawa tu, so kwa wewe kumbadilisha mawazo, kama hana akili ya kujiongeza, ni jambo gumu saana. Maana anaona wewe ndio umepotea.
 
Solution hawe pia kuwa mtu wa kanisa ndo mtaendana ila kama alikuwa hadanganyi hakuna haja ya kumfukuza mkeo rudiana na mkeo brada
 

mkuu lazima ukubali kuwa kuna wachungaji ni nguvu za giza tu.
we mchungaji anaomba mpaka salary slip yako ya nini?
si anataka kulinganisha mapato yako ili awe anakukamua zaidi?
lazima mujue kuwa sio kila anayehubiri katumwa na Mungu, kuna wengine wametumwa na matumbo yao.
 
mrudie keshajifunza huyo na ikiwezekana hameni mji am mtaaa. kaishi mbali na kwao!!!!!!!!!!
 
kama mama umemfungulia biashara,,na mchungaji awe kamshika,biashara inadumaa hata umuongeze mtaji wa bilioni yeye ataona maombi ya mchungaji ndo yameleta pesa na atazipeleka kwa mchungaji na biashara haiendi mbele

Kabisa usemalo hilo
 
ulokole bongo bhana, huyo dawa yake kumchukulia kifaa kingne then unampotezea hata asiporudi, mtu mzima na akili zake basi tu anakufanyia kusudi
 
Dah! Walokole weengi n kama wameshikiwa akili zao, manake wayafanyayo n tofaut na akili ya kawaida ya kufikiri, jamaa yangu flani pamoja na kupata zero form 6 pale kibaha baada ya kujaza vitu vya ajabu kwenye paper mpaka leo bado mlokole
Yaan kama vile wamemuazima mtu akili
 
Dah vaz la ulokole.......but ungemsamehe tu kwa kuwa hajachepuka ila kwa mashart mazito kuwa atabadilisha timetable za kanisa au ahame kanisa cos Mungu yuko pote na makanisa mazur yapo mengi tu
.Hata biblia imeandika mwanamke amtii na kumsikiliza mmewe sasa hilo kanisa linatumia biblia gani?na funzo kwa wakaka wengine mdada anakuvumilia weee wakat huna kitu halaf ukipata unajifanya oooh nataka mke mlokole.....mxuuuuuuuuu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…