Najuta kuoa mwanamke mlokole

Unajua kueleza na komaa usirudi nyuma
 
Aise pole sana..
Huwa najiona nina matatizo, nikisoma maandishi kama haya najiona nimebarikiwa kwa kweli..
Duh..
Pole sana...
 
Pole mkuu,,,siwezi kupinga hoja yako,ila mke wako hakuwa na busara,kumtafuta Mungu kanisani kuna thawabu yake, lakini unaweza kumtafuta Mungu ndani kwako huku ukiitunza ndoa,,,Mungu akuongoze katika kipindi hiki,
 
mie nlikuwa na mchumba akaja kuchezewa na pasta wake mkongo hapo knondon studio!

nikamtema! ila kuna cku Mungu atanilipia kwa pasta mshenz kwel yule
 
Inategemea,km wewe bado unampenda,endelea naye,ila km umemchoka,bas we jichukulie Rachel tu,maana na hao walokole nao hawaeleweki!!
 
Pole Ndugu. Kosa kwa kweli huenda si ulokole ama kanisa bali uongozi wa hilo kanisa. Huwezi ukatenganisha familia kwa sababu ya kukosa utaratibu mzuri wa kanisa. Uliosema yote nimekuelewa. Tatizo ni hekima ndogo ya baadhi ya wachungaji jinsi ya kuendesha kanisa. Wachungaji wetu wa makanisa waende vyuo vya Uchungaji wakasome masomo husika. Kanisa si kampuni ya mtu binafsi. Kanisa lina utaratibu. Nimesikitika sana. Ushauri wangu huyo mkeo amejifunza mpe nafasi nyingine madam amerudi na kuomba radhi. Huwezi kujua huyo uliomwacha naye atageuka. Mkeo ameponzwa na utaratibu mbovu wa makanisa mengine ambayo kiongozi hataki kuheshimu uhuru wa mwamini kifedha, kwa muda wake na kwa majukumu ya kifamilia. Kanisa si mahali pa matoleo yasiyo na utaratibu. Ila msamehe mkeo amejifunza. Mrejeshe tafadhali atabadilika. Mungu akubariki.
 
Mkuu pole sana kwa changamoto hiyo ,Hiyo ndo mitihani ya kimaisha ukiachana na ya darasani.Mkuu unaonekana wewe si MTU Wa church sana unaonaje ukaanza kuhudhuria na wewe ili kusolve tatizo hill au unaogopa kuwaitaonekana kama mkeo kakushika akili? Au kakubadilisha akili? Maana happ yeye kuacha ni ngumu na wewe ndo utaki kumwelewa.Kuna jirani yangu yeye na mkewe na watoto wanashindaga kanisani had I SAA sita za usiku hivo wanaenjoy sana ,

Tunarudi pale pale ndege wanaofanana huruka pamoja.
 
Ha ha ha apana mbona namruhusu mikesha, tatizo unakuta maombi ya kufunga bila taarifa na wewe unatka kula mzigo anakuambia amefunga 7 days !!! Wewe unaweza ?
Si unavumilia jamani kwani baraka anazotafuta si mnazipata wote mkuu? Unataka kula 1/1 - 31/12?
 
msg yako imenifanya nifikirie mara mbili mbili,ubarikiwe
 
Umeandika kila kitu mkuu......uamuzi wako ni sahihi, huyo hakufai, hata mimi ningemtoa mbio.
 
Du tuko wengi jpl matumizi yanakua makubwa Na ratiba mbovu wangu yuko vizuri mambo mengi ya nyumbani ila hawa wachungaji kama wamewaroga nilienda ck mmoja knsn kwao chungaji mwenyewe anaonekana kua mjanja mjanja
 
Duuh aisee bro inaonyesha umekasirika sana......pole sana.......
 
Pole saana ,,,mkuu hakuna maisha hapo,,
 
Karibia ni miaka miwili Sasa imepita Tangu hiki kisa kitokee.

Hebu leta mrejesho, ulirudiana na mkeo au ulirudi kwa Rachel wa chuo?
 
KWANINI UMPIGE MKEO?! KUMPIGA MKEO NI UDHAIFU, UJINGA NA USHAMBA.
Ninyi wawili mna mitazamo miwili tofauti, yeye anaona kanisa ni muhimu zaidi kwake na wewe unaona familia ni muhimu zaidi kwako kuliko kanisa. Mtazamo wake huu umetokana na malezi toka kwa wazazi wake (Hata wazazi wake walishakuambia kwamba wakati mwingine huwa wanalala kwenye mkesha kwa ibada). Hata na wewe mtazamo wako yawezekana umeuona kutokana na malezi au mapokeo jinsi unavyoishi na ulivyoyaona maisha kwa jamaa zako, n,k.

Ulichotakiwa kufanya ni kukaa chini na mkeo mpendwa (maana ulimchagua mwenyewe) na ulipaswa kuongea naye kwa upendo, heshima kama mwanandoa mwenzako na si kumuambia kwamba: 'ni amri na si ombi!'. Mlipaswa mjadiliane juu ya faida na hasara ya yote mawili - ingechukua muda lakini hatimaye mgepata suluhisho. LAKINI SIO KUMPIGA!

Kilichotokea ni kwamba kwa kuwa wewe ni dhaifu (huwezi kujenga hoja) ulishindwa kujenga hoja ya maana, ili kumshawishi mkeo aone umuhimu wa familia kwanza badala ya kanisa. Baada ya kushindwa kumshawishi ikabidi utumie nguvu (Maana ndicho hicho tu ulichonacho) na kuanza kumpiga.

Sasa unataka kukimbilia kwa Rachel, ili naye mkitofautiana mitazamo uanze kumpiga kama ulivyofanya kwa mkeo. Rachel labda yeye hataenda kwenye mikesha ya ibada, lakini lazima atakuwa na kitu/mtazamo tofauti kuliko wewe, utafanyaje? Naye utampiga? Utapiga wanmgapi!!!

Utawakimbia wangapi? Kwanini unakimbia matatizo??!
Mkeo sasa amekupa fursa ya kukaa naye mrekebishe mambo, tena amesema anakupenda na anataka kurudi nyumbani, sio ndicho ulichokuwa unakitaka?! Umeshazaa mtoto mmoja na mkeo, unataka ukamzalishe Rachel naye mtoto?, mgombane, umpige na kisha umwache! Utakuwa na watoto wawili na kila mtoto na mama yake, si ndio!!??

Rachel, huko uliko kama unanisikia akija huyu jamaa usimkubali, mwambie arudi kwa mkewe!

ACHANA NA RACHEL, USIENDE KUMHARIBIA MAISHA YAKE. YAANI WEWE UVURUGE HUKO, NA YEYE AKAE KUKUSUBIRI WEWE TU, HAPANA!. MRUDIE MKEO, WEKENI MEZANI HOJA ZENU (KANISA VS FAMILIA) NA KISHA MZIREKEBISHE. LEENI MTOTO WENU NA IKIWEZEKANA MUONGEZE MTOTO MWINGINE NA MWINGINE .

MWISHO - ACHA TABIA YA KUMPIGA MKEO, SHEMEJI ZAKO NA WAKE WA WENZIO
 


Tumesikia upande wako, hatujasikia mwingine, ila ngoja tu assume kwamba unayosema ni kweli:

- Huyo mwanamke anakosea sana, sana, na wachungaji wa hayo makanisa ya hivyo ni wa hovyo sana.
- Huna haki ya kumpiga mke hata siku moja, ni makosa makubwa sana. Ukimpiga lengo linakuwa nini?
- Hadithi yako umei pimp kidogo, unajua maana ya kuvunja mbavu?
- Swala la kumuacha au kurudiana naye ni lako mwenyewe, ila kama una tabia ya kupiga hivyo, ishi mwenyewe!
 
mkuu naona mineno ya ghadhabu inakutoka kwa Speed kali mno.!!!
1- POLE SANA kwa maswahibu yaliyokukuta.
2- Hongera kwa kustuka, kemea vikali kutekwa kiakili na kufanya hyo biashara ya kuwatajitisha wachungaji.
Huyo mkeo hajitambui mana nathubutu kusema aliitelekeza familia kwa sababu ya kanisa,
haiwezekan uwe na mtoto mchang ukakosa muda wa kulea eti kisa ratiba za kanisa zisizoeleweka.
PIGA CHINI huyo broo mwache akamtafute type yake kanisani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…