Najuta kuoa mwanamke mlokole

Sema umempa likizo after sometimes unamkumbuka na kumhitaji tena, bora zimwi likujualo.......
 
pole sanaa, ila una roho ngumu kaka yangu unapiga mtu anapoteza fahamu then unamfungia store!!!!!!!!!!!!!
 
HAHAHAHAAHAHAAH kuna mahali nimefurahi kwanza ume tembeza kichapo kwa wote hadi dada mtu. we muache kama mwaka hivi kwanza au muache kabisa maana hajuii umuhimu wa ndoa na pia kwanini anapenda sana kwenda huko au kuna mngine anafanya ila wewe hujui
 
Anyway, pole lkn suala la maombi nadhani ungemwachia Mungu. nimecheka tu kanisa kuomba salary slip, kwanza ningeshika mic nikatukana kinoma mpaka baba mchungaji ajione hafai
 
Polee sanaa kijana....watu wengi hawana uelewa na najua ww ndo unaonekana mkorofi
 
Wewe itakuwa ndo huyo mchungaji
 
Kiukwel ukipata mlokole aliyezama sana kwenye dini utaipata maana wanakuwa kama wale waislam wa imani kali.

Mkuu sasa we ulimuoaje mtu ambaye hujui tabia zake. Kwan wakat akiwa mchumba hukusoma ramani za maisha yake?
Pia napenda kukuuliza Je wew SIO MLOKOLE??? sasa uliwezaje kuoa mlokole maana si rahs kukukubali kama sio wa din yao
 
Stori ya kutunga. Ninachojua mimi makanisa ya kilokole yanakua na mkesha mara moja kwa wiki, au mara moja kwa mwezi. Hakuna mkesha kila siku. Hiyo ni chuki yako binafsi dhidi ya walokole.
 
Wenye wake Walokole wenye Ratiba za mikesha ni shida Hawa watu muda mwingi wanatumia kwenye mkesha
 
Walokole ni wakristo wenye msimamo mkali, sasa ulioa bila kujua misimamo yao ndo ulipokosea, ukotaka abadilike ni kumuhamisha dhehebu, Aje RC bia naambo ingine padre analegeza
 
Yale mashati ako ya kunga'aa na kuteleza, mashat ya vitenge uliyookokea itabidi uyagawe tuu huna jinsi, wape weny mavazi yao
 
Ukweli ni kwamba wanawake wengi katika ulokole hawatumii na hekima. Lile Neno kwamba tukae na wake zetu kwa akili ni kweli. Mimi mlokole na mke wangu pia.Naona amani ipo. Siku moja mch kaja kunipa taarifa eti wamemchagua wife kuwa mzee wa kanisa. Mi nikammuliza kwanini hakuuliza kwanza bali anakuja kunipa taaarifa wakati wao waliishapanga. Akawa hana la kusema eti Mungu kamchagua sio yeye. Kumwambia huyo Bro ana Jazba bora ukae kimya. Hujui.Ila mimi naona huyu Bro akamwone mch akifuatana na mke wake wakubaliane ratiba na mambo ya pesa yawe wazi. Bora mlokole,mi namshukuru Mungu nimekutana na mke nilienae. Kero zipo kwasababu ya udhaifu wa wenzetu ila mizani imezidi kwenye baraka na aman
Tatizo linakuja pale mke anapochukua tamko la mchungaji kama tamko la Mungu mwenyewe wakati mch ni binafamu wa kawaida.

. Bwana Yesu Asifiwe.
 
Ulitema big G kwa karanga za kuonjeshwa mkuu

Pole sana kwa kupata wife material feki
 
Mkuu pole sana hao ni aina ya walokole ambao hawajui maandiko na ndiyo wanaodhalilisha Ukristo. Huo ni ulokole wa kishamba ambao hauzingatii muda na ndoa za watu na familia kwa ujumla! Najikiri kabla hujamruhusu kurudi lazma aelewe msimamo wako na aelewe kuwa hupingi Ibada bali lazma kuwe na kiasi! Ili usije ukafungwa au kupata usumbufu ni heri aendelee kwanza kukaa kwao ili apate muda mzuri wa kuhudhuria hizo ibada za kitapeli ambazo. Biblia inasema ndoa na iheshimiwe na watu wote, bipi mchungaji apange ratiba zisizojali mahusiano?

Mke arudi ila ajue msimamo wako na aukubali!!!
 
sasa mungu kamchaguaje au mchungaji alionge nae akasema yule ndo chaguo.hahahahahahahahaah mchungaji kamzimia mkeo
 
Hii hadithi yako , kwangu naiona kama Time Travel ( nimetravel to the future )maana hiyo paragraph ya mwisho ni mle mle ninayoishi sasa, na hiyo ya hapo mwanzo ni kama vile kuna ushawishi upo ili nioe wa design hiyo [emoji85] .thanx kuna kitu nimepata hapa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…