Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 274
- 486
Najuta kumsamehe mke wangu sio kama sina moyo wa kusamehe au mimi ni binadamu nisiye na roho ya huruma hapana!! Lakini msamaha wangu kwake ulitaka kuondoka na roho yangu.
Mimi ni fundi furniture natengeneza vitanda, masofa, makabati nk. Mke wangu ni mama wa nyumbani na tuna watoto wawili wadogo. Mmoja wa miaka nane na mwingine wa miaka minne na nusu.
Siku hiyo nilienda kazini asubuhi na mapema lakini kufika sa tano nikaona nirudi nyumbani kupumzika kwani sikuwa na mood ya kufanya kazi siku hiyo.
Kufika nyumbani sikuamini macho yangu nilimkuta mke wangu akiwa na mchepuko wake juu ya kitanda changu wakifanya tendo la ndoa lakini sikutaka kukatisha starehe yao. Nilichofanya niliamua tu kuwasalimia kisha nikaondoka.
Yule jamaa nae kwa hofu hakuendelea na alichokuwa akifanya kwa mke wangu akaamua kuondoka.
Baadae nikarudi nyumbani sikuwa na maneno mengi na wala sikutaka kugombana na mke wangu nilihofia kumuudhi asije akachukia akaondoka nyumbani ikiwa bado nampenda na watoto wetu bado wadogo wanahitaji malezi yetu wote wawili.
Nikiwa nipo ndani nimepumzika nyakati za jioni mke wangu alimtuma mtoto wetu wa miaka nane akanunue sumu ya panya dukani kwamba kuna panya mkubwa amemuona anasumbua sana ndani.
Baada ya mapishi chakula kikawa tayari mezani. Mke wangu alichukuwa ile pakiti ya sumu akaichana na kunyunyiza sumu kwenye sahani ya chakula.
Alidhani hakuna aliyemuona kumbe binti yetu huyo mwenye miaka nane alishuhudia tukio zima ila akajikausha kama hajaona kitu. Mbio akaenda kwa jirani kuelezea alichokiona. Jirani kwa wema akampa kichupa cha maziwa akamwambia kama baba yako akila hiko chakula mpe maziwa haya anywe.
Mke wangu alikuja chumbani kuniita kuwa chakula kipo tayari.
Nilipofika mezani kila mtu akapewa sahani yake ila binti yetu akasema "baba mimi nimeshiba chukua chakula changu hiko chako utakula kesho." Nami nikamwambia basi funika hiko chako utakula kesho mimi acha nile hikihiki.
Nikaanza kula huku binti yangu akiniangalia nami nikachukua kipande cha nyama nikampa lakini mama yake yaani mke wangu akawahi akampokonya na kumsema kwa ukali "wewe si umesema umeshiba sasa kwanini unapokea hiyo nyama?"
Nikaona sio kesi nikampa kipande kingine akawahi harakaharaka akaweka mdomoni. Mke wangu alichukia sana.
Punde tumbo likaanza kuniuma binti yangu akawahi kunipa yale maziwa nikanywa. Mke wangu akamwambia "na wewe kunywa hayo maziwa mwanangu utakuja kufa bure."
Hapo ndio nikajua kumbe mke wangu alikuwa ameniwekea sumu kwenye chakula kwa dhamira ya kutaka kuniua.
Ilibidi niite majirani na viongozi wa mtaa ili washuhudie kile kilichotokea. Watu walipomuhoji "kwanini umetaka kumuua mume wako?" akawajibu "kwasababu amenifumania na hakunifanya chochote hivyo nilihofia labda alipanga kuniua kwa siri ndio maana nimeamua kumuwahi yeye."
Kila mtu alishangaa kwamba amekuwa mjinga kiasi gani hadi kutaka kuniua kwa kosa ambalo amefanya yeye mwenyewe. Yaani kwake mchepuko una thamani kuliko mimi.
Hapa nipo nawaza nimsamehe mke wangu ili tuendelee kulea watoto wetu pamoja au niache aende jela kwa kosa la jaribio la kutaka kuniua?
Naomba ushauri wako tafadhali. !! 🙏🙏🙏
#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn
Content By Mr George Francis