Najuta kuharibu ndoa yangu

Najuta kuharibu ndoa yangu

Unapaswa kuolewa na unayempenda hata kama anaye propose ni mwanaume..

Ndio maana kuna neno 'No'

Hizi ndoa za 'but' ...'but'...mwisho wake ndio huu...

Simpendi but ana roho nzuri...
SImpendi but ana mkwanja mrefu

simpendi but ananipenda..

Sikubali kabisa kuwa eti wanawake hawana choice ya nani wa kumuoa...nimekataa...
Of coz choice wanazo ila wakishakubali inatakiwa watulie, sio inakuwa mguu nje mguu ndani.
 
Of coz choice wanazo ila wakishakubali inatakiwa watulie, sio inakuwa mguu nje mguu ndani.
This was meant for them women...
Kwa sababu mwanaume anaweza asijue kuwa hakuna penzi...mdada ana pretend sababu kijana ana pesa...

Kama humpendi usimkubali...mwache atafute atakayempenda usimwaribie CV ya kuwa divorcee...

Na kwa mwanaume ukishajua hupendwi kabla ya ndoa ukitegemea pesa yako itanunua pendo expect chochote...lakini wengi wa cheaters waliolewa for reasons ambazo love is not one of them...

Unakuta mtu ametoka say majuu anawambia dada zake nitafutie mke...lazima apate opportunist...
Vijana hawana muda wa courtship...huwezi kuchukua muda kumfahamu unayefunga naye ndoa afu yatokee haya maajabu...
 
aisee kuna mtu wangu wa karibu sana yamemkuta km hayo
majuto mjukuu

geniveros ndio yule uliyetuambia anataka kuachana na mme wake ili aendelee na masomo?
Halafu uje na ule mrejesho wa ile siredi
 
Last edited by a moderator:
probabily jamaa alikua GOOD BOY mwanamke akaamua kumdharau...hicho kitu kinawasumbua sana black American...maana mademu black americans wengi walikuwa wanaacha au wanawadiss GOODBOY na kuolewa na mathughs...mwishoni unakuta masinglemotheer kibao maana mathugs(BADBOY) hayajali ..ni kwanini wanawwake wengi wanshidwa kwenda na good boy wanakimbilia kwa mathugs....? kuna msemo African americans wanatumia kwamba GOOD BOYS FINISHES LAST maana ukiwa GOODBOY ukianza mwanzoni HUMALIZI
 
Unapaswa kuolewa na unayempenda hata kama anaye propose ni mwanaume..

Ndio maana kuna neno 'No'

Hizi ndoa za 'but' ...'but'...mwisho wake ndio huu...

Simpendi but ana roho nzuri...
SImpendi but ana mkwanja mrefu

simpendi but ananipenda..

Sikubali kabisa kuwa eti wanawake hawana choice ya nani wa kumuoa...nimekataa...
Unapoolewa na usiyempenda matokeo yake ndio haya, wanasema majuto ni mjukuu. Halafu si vizuri kuumizana kisa mmoja wenu anaupendo kumzidi mwenzie , kuumiza ni tabia ya kinyama kabisa.
 
Mmmh! Hii stor tu.
Kweli baaa ya mwez mwanaume aoe?!
Lakn hadithi yako ina mafunzo mazur.

Inatokana na maamuzi yako si ajabu kunabinti alikua amesha msoma muda mrefu kama anafaa alipopata chansi akaamua kumuoa fasta kuziba machungu ili amsahau haraka
 
Mmmh! Hii stor tu.
Kweli baaa ya mwez mwanaume aoe?!
Lakn hadithi yako ina mafunzo mazur.


Mkuu huyu jamaa aliishaanza ktuafuta option baada ya kuona vituko vya bibie haviishi. Akawa anavuta kasi, baada ya kuona things kwenye msitari akamtolea uvivu..
 
Inasikitisha, lakini ingekuwa vizuri zaidi kama angeeleza sababu zilizomfanya amsaliti mumewe. hii itasaidia wanaume kuelewa jinsi ya kuishi na hawa viumbe...
 
Inasikitisha, lakini ingekuwa vizuri zaidi kama angeeleza sababu zilizomfanya amsaliti mumewe. hii itasaidia wanaume kuelewa jinsi ya kuishi na hawa viumbe...

Grow up brotherrrrr, usaliti umo moyoni mwa mtuu, hauna sababu, jst unagrow gradualy
coz uyo bidada alikua na muda wa kutosha wa kukaa na mume wake na kuongelea upungufu wowote ambao ungemfanya asaliti, other wise uyo dada ni malaya mshenzi, na wala bado na aendelee kuchezewa uko.
yule ni mume wake, ndio mtu pekee wa kuyaongelea matatizo yao.
 
Wanaume wengi wanapenda vya chee ukiwa na mume huduma nyingi anatoa kama makazi, malazi na mavazi. Ye wanje nikutomba nakukuacha bila hata hela ya ndoo ya maji. Unarudi nashombo kwa mumeo. Ndo tujue ndoa nizaidi ya ajira, unamzarau mumeo kwakumtoa kasoro kibao mwanzo kengeza ilikua chongo leo macho kumchuzi
 
Grow up brotherrrrr, usaliti umo moyoni mwa mtuu, hauna sababu, jst unagrow gradualy
coz uyo bidada alikua na muda wa kutosha wa kukaa na mume wake na kuongelea upungufu wowote ambao ungemfanya asaliti, other wise uyo dada ni malaya mshenzi, na wala bado na aendelee kuchezewa uko.
yule ni mume wake, ndio mtu pekee wa kuyaongelea matatizo yao.
Yeah i am & will grow... but, you have to be logical. Nimetoa maoni kuwa angekueleza sababu iliyomfanya amsaliti ili wanaume wajue mojawapo ya sababu inayomfanya mwanamke atoke nje. Umalaya ni matokeo na si chanzo...
Be objective and not subjective!
 
Kuna Dada mmoja nimetokea kuzoeana nae maeneo tunakofanyia kazi hata yeye ni Mjasiriamali mzuri tu. Siku moja nilimkuta amekaa peke yake akionekana ni mtu mwenye mawazo mengi inikajaribu kumdadisi nielewe kinachomsumbua kichwa maana kama ni kipato anacho cha kumuendeshea maisha.

Aliamua kunipa stori yake ya maisha kuwa miaka saba iliopita alikua ameolewa. Anadai mume wake alimpenda sana kwani alimjali sana pamoja na kumheshimu. Ila yeye kama yeye hakuona thamani ya upendo kutoka kwa mume wake kwani alimdharau na kumfanyia makosa mengi lakini mume wake hakuonesha kukata tamaa kwani aliendelea kumpenda na mara nyingi alitumia muda mwingi kumshauri ili ajitambue na vile vile aitambue Dunia kua haina mwenyewe.

Anasema alianza kumsaliti mume wake ingawa mume wake hakuonyesha dalili za kusaliti ndoa yao. Anadai alikua anatoka na kijana mmoja ambae alimpenda zaidi ya mume wake siku moja mme wake alifumania sms kwenye simu yake ya mapenzi na ndipo alipomuambia amemkosea makosa mengi ila kwa lile hawezi kumsamehe siku hiyo hiyo alimuandikia talaka yake huku mwanaume akitokwa na machozi kwa uchungu pindi alipokua anaandika talaka.

Kutokana na alivyokua anajiamini kuwa mume wake anampenda sana alijipa moyo kua lazima atamsamehe tu, alijaribu kumuomba msamaha lakini mme wake alionekana mgumu akaamua kuondoka akijua baada ya wiki mbili hasira zitapungua na atamsamehe tu.

Aliendelea na uhusiano na yule kijana baada ya wiki mbili alimuomba wakutane ili wayamalize ila mwanaume alikataa. Baada ya mwezi mmoja alisikia kua ameoa mke mwingine na ndipo alipokata tamaa kuwa ameachika moja kwa moja. Ilibidi aongee na yule kijana aliekuwa anacheat nae ili amuoe, hakuamini maneno alioambiwa kuwa hawezi kumuoa kua kamwe katika maisha yake hawezi kumuamini.

Yule dada akamwambia alikuwa anasaliti ndoa yake kwa kua alikua anampenda sana, yule kijana alimuambia katika maisha hakuna kitu kama hicho huwezi kusaliti ndoa yako kisa ulienae humpendi na kama alikua hampendi kwanini alikubali kuolewa nae na akamwambia iwe mwisho wa mahusiano nae.

Aliniambia alijiona ni mjinga kati ya wajinga na baada ya miezi minne yule kijana na yeye alioa. Anasema amekutana na wanaume mbali mbali ili aingie kwenye ndoa mara ya pili lakini ameambulia kuchezewa tu mwisho wa siku anaachwa. Ilifikia wakati akaenda kwa waganga wa kienyeji ili wamuangalizie kama mume wake wa kwanza alimloga asiolewe lakini waganga wawili walimuambia hakuna kitu kama hicho na hata kama akienda kwa mganga akimwambia amelogwa huyo mganga ni tapeli.

Mpaka sasa mume wake walioachana amebahatika kupata watoto wawili na hata yule kijana aliekuwa anatoka nae na yeye ana watoto wawili, kwa hiyo anasema roho inamuuma sana kuharibu ndoa yake ni mwaka wa saba toka aachike.

Ushauri wangu siku zote ukiona umependwa jua thamani ya kupendwa hata kama wewe utakua umempenda kwa wastani vumilia hivyohivyo na heshimu mahusiano yenu. Hasahasa akina Dada nyie ndo mnakumbana na changamoto nyingi hasa linapofika swala la kuolewa ukiona mwanaume amekupenda na ukaamini kweli anakupenda muonyeshe upendo na umuheshimu kwani kuolewa kwenu kunatoka na maamuzi ya mtu mwengine ni tofauti na wanaume.

Pole zake , masikini. Mwambie Bado hajachelewa kwa Yesu ,kwa sababu yeye hupokea mioyo iliyopondeka na kuvunjika kama zabihu kuu kwake . Aje kwa Yesu kwa kuwa Bado anampenda na atabadilisha historia ya maisha yake, amen. Mpe pole sana. Asante.
 
Back
Top Bottom