Najuta kuharibu ndoa yangu

Mlati

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
207
60
Kuna Dada mmoja nimetokea kuzoeana nae maeneo tunakofanyia kazi hata yeye ni Mjasiriamali mzuri tu. Siku moja nilimkuta amekaa peke yake akionekana ni mtu mwenye mawazo mengi nikajaribu kumdadisi nielewe kinachomsumbua kichwa maana kama ni kipato anacho cha kumuendeshea maisha.

Aliamua kunipa stori yake ya maisha kuwa miaka saba iliopita alikua ameolewa. Anadai mume wake alimpenda sana kwani alimjali sana pamoja na kumheshimu. Ila yeye kama yeye hakuona thamani ya upendo kutoka kwa mume wake kwani alimdharau na kumfanyia makosa mengi lakini mume wake hakuonesha kukata tamaa kwani aliendelea kumpenda na mara nyingi alitumia muda mwingi kumshauri ili ajitambue na vile vile aitambue Dunia kua haina mwenyewe.

Anasema alianza kumsaliti mume wake ingawa mume wake hakuonyesha dalili za kusaliti ndoa yao. Anadai alikua anatoka na kijana mmoja ambae alimpenda zaidi ya mume wake siku moja mme wake alifumania sms kwenye simu yake ya mapenzi na ndipo alipomuambia amemkosea makosa mengi ila kwa lile hawezi kumsamehe siku hiyo hiyo alimuandikia talaka yake huku mwanaume akitokwa na machozi kwa uchungu pindi alipokua anaandika talaka.

Kutokana na alivyokua anajiamini kuwa mume wake anampenda sana alijipa moyo kua lazima atamsamehe tu, alijaribu kumuomba msamaha lakini mme wake alionekana mgumu akaamua kuondoka akijua baada ya wiki mbili hasira zitapungua na atamsamehe tu.

Aliendelea na uhusiano na yule kijana baada ya wiki mbili alimuomba wakutane ili wayamalize ila mwanaume alikataa. Baada ya mwezi mmoja alisikia kua ameoa mke mwingine na ndipo alipokata tamaa kuwa ameachika moja kwa moja. Ilibidi aongee na yule kijana aliekuwa anacheat nae ili amuoe, hakuamini maneno alioambiwa kuwa hawezi kumuoa kua kamwe katika maisha yake hawezi kumuamini.

Yule dada akamwambia alikuwa anasaliti ndoa yake kwa kua alikua anampenda sana, yule kijana alimuambia katika maisha hakuna kitu kama hicho huwezi kusaliti ndoa yako kisa ulienae humpendi na kama alikua hampendi kwanini alikubali kuolewa nae na akamwambia iwe mwisho wa mahusiano nae.

Aliniambia alijiona ni mjinga kati ya wajinga na baada ya miezi minne yule kijana na yeye alioa. Anasema amekutana na wanaume mbali mbali ili aingie kwenye ndoa mara ya pili lakini ameambulia kuchezewa tu mwisho wa siku anaachwa. Ilifikia wakati akaenda kwa waganga wa kienyeji ili wamuangalizie kama mume wake wa kwanza alimloga asiolewe lakini waganga wawili walimuambia hakuna kitu kama hicho na hata kama akienda kwa mganga akimwambia amelogwa huyo mganga ni tapeli.

Mpaka sasa mume wake walioachana amebahatika kupata watoto wawili na hata yule kijana aliekuwa anatoka nae na yeye ana watoto wawili, kwa hiyo anasema roho inamuuma sana kuharibu ndoa yake ni mwaka wa saba toka aachike.

Ushauri wangu siku zote ukiona umependwa jua thamani ya kupendwa hata kama wewe utakua umempenda kwa wastani vumilia hivyohivyo na heshimu mahusiano yenu. Hasahasa akina Dada nyie ndo mnakumbana na changamoto nyingi hasa linapofika swala la kuolewa ukiona mwanaume amekupenda na ukaamini kweli anakupenda muonyeshe upendo na umuheshimu kwani kuolewa kwenu kunatoka na maamuzi ya mtu mwengine ni tofauti na wanaume.
 
Huwa kuna laana Fulani hivi kwa wanandoa ila ili itimie ni lazima yule anayefanyiwa makosa awe innocent, mazingira yake ni kama hayo hayo!

Unajua wenzetu mabinti huwa wanajisahau sana katika ndoa, kosa lao ni kuwa wakiambiwa " Nakupenda tyr wanaanza kupata hisia Fulani hivi"
 
giza yani narudia maneno yale yale kila saa! emb fanya ku edit kdog utenganishe hata kwa mafung! mweh!
 
Ahsante mtoa uzi nafikir msg imewafikia ndugu zetu..
mtoa uzi nimekubali sana uandishi wako..Umejitahidi kutulia na kuandika maneno kwa ufasaha zaidi pasipo kukosea herufi...

I wish angepata ujumbe huu..my....!!

angejifunza kitu hapa angejuta kwanini alikuwa akileta pozi alipogundua alipendwa kwa dhati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom