Wakuu kwema?
Daah kilichonikuta mimi najuta.
Kuna dada mmoja ofisini alikuwa ananizoea yaani inaonyesha wazi kwamba ananikubali.Mitego yake ya ajabu ajabu mimi nilishindwa kujizuia, niliona nikimwacha ataniona lafa.Wife alisafiri na watoto sasa nikaona ule ndiyo muda mzuri wa kula tunda la huyu dada wa job.
Hiyo siku tulikunywa sana pombe tukaamua tuende home tukamalize hiyo mitego tego. Kutokana na akili za pombe nikasahau kabisa kwamba ndiyo siku wife anarudi.Tulifika tukaanza kuchezeana sebuleni pale na mlango tulisahau kufunga. Tukaanza kuvua nguo tukabaki utupu.
Mara mlango unafunguliwa anaingia wife na watoto. Wakuu daah hata tunda sikulila lakini nani ataniamini?
Kilichofuata kwa aibu iliyonipata nimeamua kuhama nyumbani na kuja kupanga kwenye kachumba kamoja nikaacha nyumba yangu nzuri.
Sasa wakuu naombeni ushauri nianzaje kurudi nyumbani kuomba msamaha? Je watoto nitawatazamaje ikiwa wameona utupu wangu?
Ushauri wenu ni muhimu wakuu maana nimemiss my family.