Najua wengi hatumpendi Rais Magufuli ila tunayaonaje haya?

Huyu jamaa angekuwa rais wa Congo nadhani angekuwa anatembea na kikosi kizima Cha jeshi, yaani Kama hao wachache wasiompenda wanamtisha hivyo nadhani siku akijua wameongezeka either atatembea na kikosi kizima au ataongoza nchi akiwa Kigali
Tulieni ,vyote mlivyolimbikiza awamu ya nne mpaka virudi vyote,special mission kurudisha raslimali za serikali
 
Swala ni mtu? au chama ambacho kimekuwa kikiongoza? Magufuli atakuwepo milele? akiondoka yeye then back to square one?
Na vyama vingine vipi? Kimoja kinaongozwa na DJ zina mfumo mzuri wa uongozi? Ni afadhali mara 1000 tuongozwe na CCM ambayo ina mfumo unaoeleweka kuliko Saccos za watu binafsi.
 
Huyu jamaa angekuwa rais wa Congo nadhani angekuwa anatembea na kikosi kizima Cha jeshi, yaani Kama hao wachache wasiompenda wanamtisha hivyo nadhani siku akijua wameongezeka either atatembea na kikosi kizima au ataongoza nchi akiwa Kigali
Tutamlida zaidi na zaidi ili nyinyi wasaliti mkijitokeza tu tunakula vichwa!
 
Tutamlida zaidi na zaidi ili nyinyi wasaliti mkijitokeza tu tunakula vichwa!
Wala hakuna msaliti ila anajisaliti mwenyewe,ukishaanza kuwabagua watu wa nyumbani kwako mwenyewe,ndugu zako lazima uishie kulalamika kuwa unasalitiwa wakati ni ujinga wako mwenyewe.Huyu alianza kufeli pale alipoanza kubagua watanzania,na atafeli zaidi
 
Wala hakuna msaliti ila anajisaliti mwenyewe,ukishaanza kuwabagua watu wa nyumbani kwako mwenyewe,ndugu zako lazima uishie kulalamika kuwa unasalitiwa wakati ni ujinga wako mwenyewe.Huyu alianza kufeli pale alipoanza kubagua watanzania,na atafeli zaidi
Hakuna aliyebaguliwa ila walikuwa wanafisadi nchi yetu ndiyo wamekimbilia kwenye usaliti.
 
Tulieni ,vyote mlivyolimbikiza awamu ya nne mpaka virudi vyote,special mission kurudisha raslimali za serikali
Zinarudi kupitia mlango wa kulia then zinatokea mlango wa kushoto,ndo maana hatumtaki Prof Assad maana anataka kuziba ule mlango wa kushoto,hahahah kua uyaone mwanangu
 
Kwa wanaompenda kuna wasio mpenda wachache ,wamejificha kwenye kundi la wengi wanaompenda,ulinzi huo ni kwa ajili ya hao wachache wenye mawazo ya kishetani,wakijipendekeza tu,imekula kwao,hakutakua na namna ,ni kuwalaza tu

Kama anapendwa hivyo, huko kutokuheshimu box la kura inasababishwa na nini?
 
Nataka kukubaliana na wewe, Naona tajwimu na prove then kabla hujaleta hivyo naomba unishawishi kwa maelezo tuu japo kidogo hao watu wanakufaje, Kwamba magufuli anawaweka sumu, anawachinja au wanakufaje ila please naomba usiniambie hamna dawa za bure wakati Hizo dawa tunauziwa miaka nenda rudi ukiona umeshindwa kutoa prove then amini na wewe ni mmoja wa wanaookotwa na maneno ya watu na kufuata mkumbo bila kujua unaongea nini..

Yaani kiongozi mmoja wa upinzani akisema Magufuli kajinyea basi na wewe unaanza unalibeba kama lilivyo na unapokuta Mada au ukiwa na watu unaanza kusema Magufuli kajinyea..

JIFUNZE KUTOONGEA KITU AMBACHO HUNA UHAKIKA NACHO, JUST BECAUSE HUMPENDI MTU AU FLANI KASEMA KISA TUU KATOKA UPANDE WA UPINZANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja kati ya kitu kibaya ktk imani yangu binafsi ni kuwafanya wananchi matahira.
Upinzani ni nani hata wasababishe wanayoyatamka kuwa ndio imani ya wananchi?

Rais mwenyewe ndiye aliyeanza kuwatendea wananchi wasiyoyapenda.

Yeye ndiye aliyejenga chuki mioyoni mwa watanzania waliokuwa na matumaini makubwa na yeye.

Na walifikiri wamepata mtetezi wa kweli ambaye angesimama kwa ajili ya watanzania kwanza kumbe wakagundua wamemuweka mtu ambaye yuko tayari kulinda maslahi ya ccm kwanza
 
NAJUA WENGI HATUUPENDI UTAWALA WA RAISI MAGUFULI ILA TUKUMBUSHANE TUU:

1: Takribani miaka 107 imeshapita tangu zilivyotengenezwa reli nchini Tanzania na wakoloni mnamo miaka ya 1912, Raisi Magufuli amekuwa raisi wa kwanza Tanzania kutengeneza tena RELI.

Na kama ilivyo kawaida ya TANZANIA kufanya Project bora zaidi ya wenzetu East Africa na hata Africa kwa ujumla, Magufuli akaamua kutengeneza SGR bora zaidi kuliko ya wenzetu WAKENYA ambayo yao inatumia matreni ya diesel tofauti na zetu zitakazokuwa zinatumia njia za umeme kama Marekani & China.

Kwa africa.. Morocco, Ethiopia & South Africa ndizo nchi pekee zenye mradi kama huu.

2: Ndani ya miaka 57 tangu tupate uhuru, serikali ya Tanzania imefanikiwa kujenga hospital 77 tuu mpaka sasa ila kwa kipindi cha mwaka 1 na nusu au miezi 18, MAGUFULI amefanikiwa kujenga Hospital Mpya 67 na vituo vipya vya Afya vipatavyo 352 Nchi nzima. Na wanatarajia kuongeza vingine 27 katika bajeti ijayo..

HII NI MIRADI ILIYOWAZI, WAKENYA TUNAWAACHA MUDA SI MREFU.. NIMEWATAJA WAO MAANA NDIO KAMA WATANI WETU WA JADI KWENYE SUALA LA MAENDELEO IN EAST AFRICA.

Wakiwa katika mkakati wa kupanua Bandari yao ya Mombasa, TANZANIA nayo imeshatoa fungu la kupanua Bandari zake zote ambayo Upanuaji wa Bandari ya Dar Es Salaam utahusisha ujengaji wa Port kwa ajili ya Cruise ship, zile meli kubwa za starehe zitakazokuwa zinaanza kutunga nanga nchini kwetu na kushusha Watalii wake.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe TAZARA ilikuwa siyi reli ila njia ya punda!
 
Kama anapendwa hivyo, huko kutokuheshimu box la kura inasababishwa na nini?
Na bado ukirudi nyuma ikiwa mtoa mada anatizama watu wana mahaba naye, ya nini basi kuvihujumu vyama vingine visi show up? Ikiwa una 90% ya mahaba la wananchi?

Endeleeni kuwaona watz wajinga na umessenger wenu
 
Kama anapendwa hivyo, huko kutokuheshimu box la kura inasababishwa na nini?
Na bado ukirudi nyuma ikiwa mtoa mada anatizama watu wana mahaba naye, ya nini basi kuvihujumu vyama vingine visi show up? Ikiwa una 90% ya mahaba ya wananchi?

Endeleeni kuwaona watz wajinga na umessenger wenu
 
Anajenga kutumia our 2.5 trilion alizokwapua
Wewe unasikiliza hizi propoganda uchwara? Ana uzuri gani? Hivi budget zake zinatekelezwa kwa asilimia ngapi na hiyo miradi inajengwa kwa fedha zipi ambazo hazimo kwenye budget?Huyu ni janga tu
 
Serikali hii ya awamu ya tano kwa propoganda uchwara iko vizuri Sana,hebu tukumbushe serikali yako imetekeleza budget yake ya maendeleo kwa asilimia ngapi na Pesa ya Kujenga hospital hizo ilikuwa kwenye matumizi ya kawaida au budget ya maendeleo?
Unachotaka ni kujua hela imetoka kwenye budget gani au unachotaka ni kuona HOSPITAL IKIJENGWA???
 
Kwangu huo wote ni ubatili kama inatekelezwa sambamba na utekaji, upotezaji, mauawaji.............
 
Back
Top Bottom