Najiuliza tu; je, Biswalo anachunguzika?

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,393
Reaction score
4,085
Wadau nawasalimu.

Baada ya kusikia na kusoma Taarifa ya CAG juu ya Ushauri wa CAG kuwa Jaji Biswalo ACHUNGUZWE kuhusiana na PLEA BARGAINING nimekuwa napata KIGUGUMIZI kuwa, je ANACHUNGUZIKA?

mwananchi_official_1680979034054607.jpg
 
Wadau nawasalimu.

Baada ya kusikia na kusoma Taarifa ya CAG juu ya Ushauri wa CAG kuwa Jaji Biswalo ACHUNGUZWE kuhusiana na PLEA BARGAINING nimekuwa napata KIGUGUMIZI kuwa, je ANACHUNGUZIKA?

View attachment 2581651
Biswalo akipatwa na hatia, Rais ataonekana alimteua mtu kuwa Jaji bila vetting.

Biswalo asipopatikana na hatia, Rais ataonekana anatuchezea shere.

Kwenye mchezo wa chess hii ni checkmate.
 
Wenye mamlaka wa sasa sio waadilifu, na ni wafaidika wa uharamia wa awamu iliyopita. Hivyo wanasita kumchukulia hatua maana hata wao ni wafaidika wa amri zilizomfanya Biswalo kufanya alichokifanya.
 
Biswalo akipatwa na hatia, Rais ataonekana alimteua mtu kuwa Jaji bila vetting.

Biswalo asipopatikana na hatia, Rais ataonekana anatuchezea shere.

Kwenye mchezo wa chess hii ni checkmate.
Kwenye chess hii huitwa zungzwang, achague kipi kimojawapo lakini lazima achague. Jibu ni rahisi: DPP ni kazi ngumu, kumbuka sasa hivi taharuki iliyopo kuhusu ripoti ya CAG kuhusu hela za UVIKO na ndege overinvoicing. Biswalo yalikabili haya haya, akatimiza wajibu wake, in the process anapata maadui wengi watatumia mbinu zozote zile kulipa kisasi. Tayari wanasema Rais ajiuzulu, DPP wake je?
 
Biswalo hakutimiza wajibu wake.

Angetimiza wajibu wake kusingekuwa na kashfa ya Plea Bargaining kama ilivyo sasa.
 
Hii nchi ya hovyo sana, kila kitu kiko wazi juu ya alichokifanyq mganga sasa sijui kigugumizi kinatoka wapi??

Wafanya maamuzi wanaogopa nn?? Au ndio hii nchi tumewakbidhi majambazi??

Bunge linafanya nini?? Au liko pale kubaliki wezi, kweli juu ya bunge dictator JPM the devil and evil alituangusha sana, moto wa jehanamu uzidi kumchoma
 
Watu wanamsikiliza "Mama".

"Mama" naye alikuwa kwenye mfumo anaogopa akimwaga ugali, Biswalo atamwaga mboga.

"Mama" Anabakia kupiga siasa za danganya toto kula kunde nyama mbichi.

Ndiyo maana kamzawadia Biswalo Ujaji baada ya madudu yote hayo. Unafikiri rais alikiwa hajui haya madudu?

Hivi kwa nini hili linakuwa gumu sana kueleweka?
 
Tungekuwa na bunge serious hii serikali ingeanguka mwezi huu, lakini ni nani msafi kati yao? Kumgusa Biswalo ni kuigusa system nzima maana wanajuana kila mmoja kala ngapi
Kumchomoa Biswalo kwenye hili kuna mambo yaweza kufanyika kwa haraka
1. Kuundwa tume mfu ambayo baada ya uchunguzi majibu hayatatolewa.. Hapa ni ishu ya kucheza na muda ama pressure ikiwa kubwa atatafutiwa ubalozi
2. Kutaundwa tukio la kutusahaulisha ama kutupoza haya ya Biswalo, sasa hapa ni ishu ya mbuzi wa kafara, ni lazima kati yao wapatikane wachache wa kuwajibishwa lakini kwa makubaliano maalum ya siri, kwakuwa bila kufanya makubaliano hakuna atakayekubali kubeba gunia la chawa kwa niaba ya wengine.. Tuupe muda wakati
 
Hii nchi ya hovyo sana, kila kitu kiko wazi juu ya alichokifanyq mganga sasa sijui kigugumizi kinatoka wapi??

Wafanya maamuzi wanaogopa nn?? Au ndio hii nchi tumewakbidhi majambazi??

Bunge linafanya nini?? Au liko pale kubaliki wezi, kweli juu ya bunge dictator JPM the devil and evil alituangusha sana, moto wa jehanamu uzidi kumchoma
ORCA ACE kwenye chumba cha mahututi nani anaweza kuwa tabibu?
 
Tungekuwa na bunge serious hii serikali ingeanguka mwezi huu, lakini ni nani msafi kati yao? Kumgusa Biswalo ni kuigusa system nzima maana wanajuana kila mmoja kala ngapi
Kumchomoa Biswalo kwenye hili kuna mambo yaweza kufanyika kwa haraka
1. Kuundwa tume mfu ambayo baada ya uchunguzi majibu hayatatolewa.. Hapa ni ishu ya kucheza na muda ama pressure ikiwa kubwa atatafutiwa ubalozi
2. Kutaundwa tukio la kutusahaulisha ama kutupoza haya ya Biswalo, sasa hapa ni ishu ya mbuzi wa kafara, ni lazima kati yao wapatikane wachache wa kuwajibishwa lakini kwa makubaliano maalum ya siri, kwakuwa bila kufanya makubaliano hakuna atakayekubali kubeba gunia la chawa kwa niaba ya wengine.. Tuupe muda wakati
Tume ya Mama sasa akiwa "Site"
IMG-20230407-WA0036.jpg
 
Kwanza walianza na kujiwekea Kinga ya kuto shitakiwa kwa sababu walijua wanacho enda kukifanya na mama mwenye nyumba akampa na ulaji zaidi akijua kabisa alihusika kwenye madudu kama hayo, wana tuchezea picha tuu hao, na jengo lile lisilo kua na meno linaishia kubweka tuu na niwao walipitisha Sheria hiyo ya hovyo
 
Report ya CAG ni ubainifu wa mahesabu kulingana na vitabu alivyopewa. Na DPP pia sidhani kama alifungua akaunti ya Plea Bargain bila uwepo wa Sheria na matumizi yake.

Nakumbuka rais Magufuli katika moja ya hotuba zake, aliwaahidi Mahakama kushughulikia kesi za Plea Bargain akisema watapewa fungu kwa kila kesi ilohukumiwa na fedha zilofisadiwa kurudishwa.

Kwa hiyo, tusiwe wepesi sana kuhukumu pasipo kujua Sheria, kanuni na taratibu zilowekwa kufuatia mapato ya fedha hizo. Kama sikosei sheria ya plea bargain ilianzishwa mwaka 2021 kwa kuongeza vifungu vya sheria ya Plea Guilty (144) na kuna baadhi ya kesi zilisha fanyika chini ya sheria ya Plea Guilty.

Report ya CAG inasema fedha hizo ziliwekwa akaunti ya Plea bargain (kosa) na kiasi kidogo kiliwakilishwa hazina. Hakuna pahala katika report inasema baadhi ya fedha hizo zilipelekwa akaunti China au akaunti ya nani!

Sasa muhimu ni kusubiri report ya tume ya rais, hata kama waloteuliwa hawaaminiwi na Wananchi lakini tutaunganisha maneno ya rais na yale ya CAG kubaini mbivu na mbichi.

Binafsi naamini wamesha jikaanga wenyewe, na Wananchi wanataka kuujua Ukweli. I wish tungekuwa na Bunge la Senate ambalo kiongozi anaitwa Bungeni na kuhojiwa Live! (On Tv) Wananchi wanasikia jinsi viongozi wanavyojieleza mbele ya Senate.

Mapendekezo yangu kama tutaipata Katiba Mpya, ni muhimu sana tuwe na Senate naliita Baraza la Wazee, bungeni. Hawa wawe na mamlaka ya kumuita kiongozi yeyote kujibu tuhuma zozote za hujuma, Ufisadi ama Matumizi mabaya ya mamlaka au rasilimali za Taifa.
 
Back
Top Bottom