Najiuliza familia ya Hamza ilishiriki kumsaidia kufanya shambulizi lile? Kwanini walaumiwe Wazazi?

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,847
Imeandikwa na: Charles William.

JUZI nimeuona 'moyo' wa Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro ukigugumia kwa hasira na uchungu. IGP Sirro ameumizwa sana na mauaji ya vijana wake (askari) wanne, yaliyofanywa na kijana Hamza Hassan Mohamed.

Agosti 25, mwaka huu Hamza aliwashambulia kwa risasi askari na kuwaua askari wanne kabla ya polisi kujibu mapigo na kumuua kijana huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini. Hamza Alifariki kwa kupigwa risasi na polisi dakika chache baada ya kufanya mauaji karibu na ubalozi wa Ufaransa na daraja la Salenda.

Siku 3 baadaye IGP Sirro alipohudhuria tukio la kuwaaga askari waliouawa na Hamza alisikika akitoa kauli tata dhidi ya wazazi wa kijana huyo na wazazi wote kiujumla, hapa nchini.

Hiyo familia ya Hamza inajisikiaje? Wewe ungekuwa baba au mama yake Hamza ungejisikiaje? Kuzaa kwako umetuletea balaa Watanzania, kwahiyo naomba Watanzania wengine wasituzalie watoto kama Hamza" alisema Sirro. Ni wazi kuwa IGP Sirro 'alipata moto' na ukimsikiliza kwa umakini utabaini alikimbia na mipira mingi nje ya chaki.

Alionekana kuibebesha familia ya marehemu lawama na kuipa masimango katikati ya msiba mzito. Aliwalaumu hata wanaharakati kwa kukaa kimya. Akadai akifa raia wanaharakati huwa wanakuja juu, lakini wamekaa kimya kwenye mauaji ya polisi. Akawaonya askari kuwa wasidhani kila raia ni mtu mwema na wajifunze kutokana na tukio hilo.

Wakati Watanzania wakiwa bado wanasubiri uchunguzi wa polisi ubainishe kwanini Hamza alifanya mauaji yaliyowalenga askari na si raia wa kawaida, IGP Sirro hakudokeza lolote bali akawavaa wazazi wa Hamza, kisha akawaomba na Watanzania wengine wasizae watoto kama Hamza.

Najiuliza familia ya Hamza ilishiriki kumsaidia Hamza kufanya shambulizi lile? Kama ndivyo, mbona Polisi hawajaweka wazi kwa umma na badala yake inatupiwa lawama tu?

Kama haikushirikiana naye kwanini familia isimangwe kiasi kile kabla hata haijamzika ndugu yao? Simtetei Hamza, naitetea familia na wazazi wake ambao nao wana maumivu ya kufiwa na kufedheheka kwa kitendo kilichofanywa na mtoto wao.

Hivi ni kweli matendo ya watu wazima kama Hamza wanaostahili kubeba lawama ni wazazi?
 
Kwa ujumla wake hili tukio limewaumiza wengi, na mmoja wao ni mzee Sirro, lakini pia upande wa familia za pande zote wameumia sana pia.
Itoshe kwangu mimi kusema "Kila mmoja ni mchunga, na kila mchunga ataulizwa juu ya uchungaji wake".
 
Kwa ujumla wake hili tukio limewaumiza wengi, na mmoja wao ni mzee Sirro, lakini pia upande wa familia za pande zote wameumia sana pia.
Itoshe kwangu mimi kusema "Kila mmoja ni mchunga, na kila mchunga ataulizwa juu ya uchungaji wake".
Sirro alitakiwa kufunga mdomo wake na kutoongea akiwa na hasira
 
Back
Top Bottom