msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,471
Ni kweli kitendo kilichofanywa na kijana Hamza( R.I.P) sio cha kiungwana na hakifai kuigwa katika jamii

Lakini vile vile, afande Sirro amepotoka kwa kauli yake kwamba wazazi wasizae watoto kama 'Hamza' kwa sababu kuzaa ni mipango ya Mungu ambayo binadamu hawezi kujipangia au kuamua azae mtoto wa aina gani.

Pia mzazi anaweza kuzaa mtoto na kumlea kwenye makuzi na maadili mema ila akaja kubadilika ukubwani na kufanya vitendo viovu pasipo wazazi wake kufahamu.

Msikilize hapa Sirro akibeza uzazi wa mama zetu.

Sirro ana majibu ya uchunguzi tayari? Kwanini anakomaa sana kumshambulia marehemu? Watanzania walio wengi bado wanaona jeshi la polisi limekosa weledi kusimamia sheria. Ukimuuliza mtanzania wa kawaida asiye kada wa CCM atakuambia kuna kitu polisi walifanya ila wanaficha.

Wakifichaficha sisi tutatunga ukweli wetu, na huenda serikali na polisi wasiupende.
 
Ifike wakati lawama za kitendo cha mtu zimuendee mtu na sio mzazi....

Sio kweli kwamba Kaka zake wote Hitler wangekuwa kama yeye au Ndugu zake wote na Gandhi au Mother Theresa wote wangekuwa ni wanaharakati

Wewe leo unaweza ukawa sawa ila tendo litakalokutokea katika maisha yako likakufanya jambo utakalofanya kesho kila mtu akashangaa. Kila kiumbe ni tofauti na kila mtu hupokea vitu tofauti..., mwingine unaweza umponda na kokwa la embe akakutukana na kukuchukia wakati mwingine anaweza akakushukuru umempa mbegu ya kupanda...
 
Siro acha ushamba!watoto kama Hamza hawazaliwi wanatengenezwa kuwa walivyo na maaskari msiojali utu kama nyie!!!!Kwa miaka sita mmezalisha chuki kali katika jamii dhidi ya serikali inayotawala kwa kuwatesa na kuwaumiza wapendwa wao maksudi kabisa!!!vuneni mlichopanda!!!HAMZA ALISEMA WAZI KABISA ANA WATAKA NYIE WALA SI RAIA BALI NINYI!MJIULIZE WAPI MMEANGUKA MJIREKEBISHE!!!
 
Kamanda Sirro yupo kwenye stress. Apumzike weekend kwanza. Jumatatu atupatie majibu yaliyokamilika.

Ilikuwaje kada mwenzake kwenye chama akawavamia askari na kufanikiwa kuwaua wanne?

Ilikuwaje civilian aweze kupora AK47 za askari yeye akiwa na bastola?

Ilikuwaje mtanzania anayeonekana mtu wa kawaida kabisa, tena kada anayeshiriki mpaka kampeni za CCM na kukijengea chama matawi abadilike ghafla?

Ilikuwaje tetesi za kuporwa madini yake na askari, mbona hazikanushwi wala hazitolewi tamko?

.............R.I.P Hamza
 
Ni kweli kitendo kilichofanywa na kijana hamza(r.i.p) sio cha kiungwana na hakifai kuigwa katika jamii

lakini vile vile, afande sirro amepotoka kwa kauli yake kwamba wazazi wasizae watoto kama 'hamza' kwa sababu kuzaa ni mipango ya Mungu ambayo binadamu hawezi kujipangia au kuamua azae mtoto wa aina gani

Pia mzazi anaweza kuzaa mtoto na kumlea kwenye makuzi na maadili mema ila akaja kubadilika ukubwani na kufanya vitendo viovu pasipo wazazi wake kufahamu.

Msikilize hapa sirro akibeza uzazi wa mama zetu

View attachment 1912695
Ni vizuri wanaopata ujauzito waende kwa Sirro akazihakiki mimba, huo ni ulevi wa madaraka walionao polisi.
 
Ni kweli kitendo kilichofanywa na kijana hamza(r.i.p) sio cha kiungwana na hakifai kuigwa katika jamii

lakini vile vile, afande sirro amepotoka kwa kauli yake kwamba wazazi wasizae watoto kama 'hamza' kwa sababu kuzaa ni mipango ya Mungu ambayo binadamu hawezi kujipangia au kuamua azae mtoto wa aina gani

Pia mzazi anaweza kuzaa mtoto na kumlea kwenye makuzi na maadili mema ila akaja kubadilika ukubwani na kufanya vitendo viovu pasipo wazazi wake kufahamu.

Msikilize hapa sirro akibeza uzazi wa mama zetu

View attachment 1912695
Mods unganisheni hizi nyuzi za HHM zimekuwa nyingi tene zinajirudia tu

USSR
 
Back
Top Bottom