Najitokeza natafuta kazi ya unasihi/ushauri nasaha kisaikolojia

BioPsychologist

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
724
1,014
Habari za leo wana jukwaa!

Natafuta kazi ya unasihi au maarufu kama ushauri nasaha (Counseling services/Psychotherapy).

Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya Saikolojia (Bachelor's degree of Psychology 2018) nina uzoefu wa miaka 4 nikifanya unasihi katika taasisi za afya kama vituo vya afya na taasisi za kijamii NGOs pamoja na taasisi za elimu shule za msingi, sekondari na vyuo.

Nimewahi kuajiriwa kwa mkataba wa miaka miwili 2019-2021 baada ya makataba kuisha nikaendelea na kazi nyingine binafsi lakini sikuacha kuendelea na unasihi hadi leo.

Kwa sasa najitolea kwenye taasisi moja ya kidini kama msaikolojia mnasihi (Mental Health Advocate Psychologist) ninae toa maudhui kupitia vyombo vyao vya habari TV na Radio kila wiki kuhusu saikolojia na afya ya akili tangu mwezi wa 10/2022 hadi sasa.

Nimejikita kwenye makundi yote kuanzia vijana umri wa miaka 7 hadi wazee wanaume kwa wanawake na watu walioko katika makundi maalumu.

Maeneo sumbufu ninayo husika nayo ni kama msongo wa mawazo, sonona, uraibu wa pombe na madawa ya kulevya, mahusiano ya aina zote (familia, mapenzi, kazini ) elimu na wanafunzi level zote, kujiamini, kupambana na hofu au wasiwasi unayojuwa chanzo chake au usiojuwa chanzo chake na maeneo mengine mengi.

Kiufupi najitokeza kuomba kama kuna mtu binafsi, shirika,kampuni, taasisi n.k atakae/watakao ona inafaa nipate nafasi ya kufanya kazi kwa malipo baada ya maelewano.

NB; Huduma za unasihi kisaikolojia bado hazijaenea sana na watu wengi hawajafahamu umuhimu wake kutokana na huduma zenyewe kuchelewa lakini umbwe la watu wenye matatizo ya kisaikolojia na afya ya akili ni wengi sana.

Kama ukinihitaji pia kwa ushauri binafsi napatikana mkoa wa Dar es salaam na pia nafanya ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.

Kama kuna kosa au hujaelewa popote kwenye bandiko hili naomba kurekebishwa.

Karibu PM

Naomba kuwasilisha.
View attachment 2709191
 
Nyie ndio mliomua kuchagua UDSM hata kama kozi ulioyopangwa ni immature na haina dili kwa hapa kwetu.

ila mbona serikali imeajiri watu wengi ndani ya miaka hii 3 pale wizara ya afya wenye taaluma yako, kada yako ni mpya wizarani ila kwa sasa inapewa kipaumbele jaribu kuwa unatembelea Web ya utumishi
 
Habari za leo wana jukwaa!

Natafuta kazi ya unasihi au maarufu kama ushauri nasaha (Counseling services/Psychotherapy).

Mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya Saikolojia (Bachelor's degree of Psychology 2018) nina uzoefu wa miaka 4 nikifanya unasihi katika taasisi za afya kama vituo vya afya na taasisi za kijamii NGOs pamoja na taasisi za elimu shule za msingi, sekondari na vyuo.

Nimewahi kuajiriwa kwa mkataba wa miaka miwili 2019-2021 baada ya makataba kuisha nikaendelea na kazi nyingine binafsi lakini sikuacha kuendelea na unasihi hadi leo.

Kwa sasa najitolea kwenye taasisi moja ya kidini kama msaikolojia mnasihi (Mental Health Advocate Psychologist) ninae toa maudhui kupitia vyombo vyao vya habari TV na Radio kila wiki kuhusu saikolojia na afya ya akili tangu mwezi wa 10/2022 hadi sasa.

Nimejikita kwenye makundi yote kuanzia vijana umri wa miaka 7 hadi wazee wanaume kwa wanawake na watu walioko katika makundi maalumu.

Maeneo sumbufu ninayo husika nayo ni kama msongo wa mawazo, sonona, uraibu wa pombe na madawa ya kulevya, mahusiano ya aina zote (familia, mapenzi, kazini ) elimu na wanafunzi level zote, kujiamini, kupambana na hofu au wasiwasi unayojuwa chanzo chake au usiojuwa chanzo chake na maeneo mengine mengi.

Kiufupi najitokeza kuomba kama kuna mtu binafsi, shirika,kampuni, taasisi n.k atakae/watakao ona inafaa nipate nafasi ya kufanya kazi kwa malipo baada ya maelewano.

NB; Huduma za unasihi kisaikolojia bado hazijaenea sana na watu wengi hawajafahamu umuhimu wake kutokana na huduma zenyewe kuchelewa lakini umbwe la watu wenye matatizo ya kisaikolojia na afya ya akili ni wengi sana.

Kama ukinihitaji pia kwa ushauri binafsi napatikana mkoa wa Dar es salaam na pia nafanya ana kwa ana na kwa njia ya mtandao.

Kama kuna kosa au hujaelewa popote kwenye bandiko hili naomba kurekebishwa.

Karibu PM

Naomba kuwasilisha.
View attachment 2709191
Ww ndio mtu niliekuwa nakutafuta kwa muda mrefu, naomba nije private
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom