Najihisi mpweke wakati nina mke

Najihisi mpweke wakati nina mke

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Kwa masingle mnaweza nishangaa...ila ni kweli kabisa, ndoa sio suruhisho la upweke.

Ikiwa ni Mwaka wa tano sasa kwenye ndoa na hatujafanikiwa kupata mtoto maisha yangu yamejaa lots of common routines .

Tunaishi peke yetu , japo tunatembelewaga na ndg wa mke mara nyingi coz tunapoishi ndipo familia ya wife inapoishi na ndg zangu wako mbali sana, hata hivyo mm na ndg zangu tumekua mbalimbali sana kimawasiliano.

Siku za hivi karibuni kuna experience inaanza nitokea ya kujihisi mpweke sana japo nina mke, nikirudi home najaribu kujipigisha storiii.....ila finaly najikuta nimetulia. Kimtindo Nahisi life linanibore ..

Mimi sio mlevi wa pombe wala mpira au michezo ya kubet...ila nisidanganye napenda totoz ila sio mchepukaji .

Hobie yangu kubwa ni kazi yangu, zamani nilipenda church ila pia siku hizi naona wananizengua....story ni zile zile kutishana na kutiana moyo huku wenzetu wanapiga hela.

Wakuu ebu nipeni mawazo mbadala wa kipindi hiki ambacho naona maisha yanakosa maana na nashindwa kuenjoy mahusiano yangu ya ndoa.

Thanks in advance
 
Ww kinacho kunyima amani ni kukosa mtoto, jua mkeo naye ana hisia kama zako tena zaidi sabab mwanamke ana changanyikiwa zaid akichelewa kupata mtoto akiwa ndan ya ndoa
 
Pole sana
10_1.jpeg
 
Mkuu watoto wanaondoa upweke?
Kimsingi siko desperate sana na watoto
Tafuta mtoto nakuambia , Utaona maisha yanakua nafuraha mpaka basi.

Niuwepo wa watoto pekee, ndio humchangamaa baba..watoto tu , ukiwafikiria wala huo muda wakukaa uwaze upweke hautokuwapo.

Ukweli nihuu... maitaji makubwa ya mwanadamu ni haya
[emoji117]chakula
[emoji117]malazi
[emoji117]mavazi
[emoji117]SEX
[emoji117]WATOTO.

Ili uwe mwandamu mwenye amani na furaha , basi jua ukikosa kimoja wapo hapo utakua Mpweke tu!!

Tafuta mtoto ..upweke utakuisha, navyokuona ukikaa unajisimea "" Kazi ninayo, pesa ninayo, mke ninaye, navaa nakula naxhotaka , lkn kwann nimpweke???"""..

Jibu ni Mtoto ....... Alafu uendelee kusali...habar za mabadiliko ya kiuchumi binafasi sijawah kaa niziruhusu zinipe wakat mgumu.
 
wewe ni introvert kama mimi, upweke ndio tumeumbiwa, mimi hata kwenye sherehe basi najitenga na watu na napenda Zaidi kuwa pweke mda wote. Ni ugonjwa kaka. toka hapo ulipo, tafuta kijiwe kizuri uwe ndio maskani yako, tafuta hoteli nzuri hapo jirani yako uwe mara kwa mara unaenda kutulia na kupata walau soda huku ukitafakari, mimi nimefuatilia sana tatizo hili na tupo wengi duniani, hali ikizidi Zaidi unaweza kuzama kwenye depression na huko ndio kubaya Zaidi sikuombei kufika huko, mimi nimepata tabu mnoo
 
Furaha iko ndani yako na siyo ndani kwako mkuu. Kiasili kila binadamu ni mpweke tu na hasa kama hujapata mtu sahihi wa kuwa nae. Haijalishi una mke au uko single.
Fikiria ni kitu gani hukupa furaha kisha fanya hicho. Hata hivyo unaweza kujishangaa like yanayowafurahisha wengine kwako ni upuuzi tu.
NB:soma vitabu
Fanya mazoezi
Jaribu kuwa raia wa kawaida tu
Kama mazingira yanaruhusu fuga (it's wonderful).bustani pia huwa ni bonge la kampani
Inapowezekana katembee misituni! hutajuta it's
so funny.
 
Ww kinacho kunyima amani ni kukosa mtoto, jua mkeo naye ana hisia kama zako tena zaidi sabab mwanamke ana changanyikiwa zaid akichelewa kupata mtoto akiwa ndan ya ndoa
Nimekupenda bure Dada kwa kusema ukweli na chonde chonde usiniombe pesa ya sikukuu wala kukaribishwa na mimi sikukuu ya mwaka mpya kwangu.
 
Tafuta mtoto nakuambia , Utaona maisha yanakua nafuraha mpaka basi.

Niuwepo wa watoto pekee, ndio humchangamaa baba..watoto tu , ukiwafikiria wala huo muda wakukaa uwaze upweke hautokuwapo.

Ukweli nihuu... maitaji makubwa ya mwanadamu ni haya
[emoji117]chakula
[emoji117]malazi
[emoji117]mavazi
[emoji117]SEX
[emoji117]WATOTO.

Ili uwe mwandamu mwenye amani na furaha , basi jua ukikosa kimoja wapo hapo utakua Mpweke tu!!

Tafuta mtoto ..upweke utakuisha, navyokuona ukikaa unajisimea "" Kazi ninayo, pesa ninayo, mke ninaye, navaa nakula naxhotaka , lkn kwann nimpweke???"""..

Jibu ni Mtoto ....... Alafu uendelee kusali...habar za mabadiliko ya kiuchumi binafasi sijawah kaa niziruhusu zinipe wakat mgumu.
Asante sana kwa wazo bora Kaka
 
Try travelling; The experience can be very eye opening. Mchukue mrs muende mapumzikoni. Miji ama mahali ambapo hamjawahi tembelea. Z'bar, mbugani, Nairobi etc. Ili muenjoy make sure una save hela ya kuweza kulala hotelini and the like. Otherwise, kufikia kwa watu ama kwa ndugu tends to be limit the fun
 
wewe ni introvert kama mimi, upweke ndio tumeumbiwa, mimi hata kwenye sherehe basi najitenga na watu na napenda Zaidi kuwa pweke mda wote. Ni ugonjwa kaka. toka hapo ulipo, tafuta kijiwe kizuri uwe ndio maskani yako, tafuta hoteli nzuri hapo jirani yako uwe mara kwa mara unaenda kutulia na kupata walau soda huku ukitafakari, mimi nimefuatilia sana tatizo hili na tupo wengi duniani, hali ikizidi Zaidi unaweza kuzama kwenye depression na huko ndio kubaya Zaidi sikuombei kufika huko, mimi nimepata tabu mnoo
Me too. Guilty as charged. Sipendi watu kabisa japo nina marafiki wachache wa kweli. Kinachonisaidia ni kusoma mavitabu na kuwa karibu na Mungu. Kwa mwezi naweza kusoma mavitabu hata 10; na hili limenisaidia sana kuwa mwenye tafakari. Na nina kijiwe changu cha tangawizi na wazee hapa mtaani basi kila jioni huwezi kunikosa hapo. Kujichanganya na watu inasaidia sana na ni lazima uwe na marafiki wa ukweli kabisa kabisa vinginevyo mtu unaweza kujikuta unaingia katika depression kali ukaishia kuishi kwa huzuni na hata kujidhuru na kudhuru wengine.
 
Duh!!! Zamani nilidhani Nina elements za kichawi aisee!sipendi watu,sipendi shangwe,sipendi kelele na wala hainipi shida sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom