Najihisi mimi wa tofauti humu ndani

Najihisi mimi wa tofauti humu ndani

sontable

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2018
Posts
261
Reaction score
536
Kuna siri nzito ndani ya JF
Kwanza napenda tu kuwapa pole na majukumu ya kila siku,nimeamua kusogeza hapa mtazamo wangu ili na mimi kidogo nijione mwenye kufanana na ninyi kwa mawazo,mijadala na michango mbalimbali ,lakini kuna kitu ambacho huwa kinanifanya mimi nijione wa tofauti kidogo na wenzangu humu ndani hadi kufikia hatua ya kushindwa kuandika nyuzi za kuelimishana kwa kushindwa kuwatambua vyema watu wa humu ndani kuwa ni wa namna gani, baadhi ya vitu vinavyoniashiria kuwa mimi ni watofauti ni kama vile

1.watu wanaonizunguka; yaani kila nikiwaangalia watu wanaonizunguka na kuwafuatilia maongezi yao sijawahi kuona wakizungumzia maswala ya jamii forum kama ilivokuwa kwa mitandao mingine kama facebook,instagram,twiter,whatsapp,youtube lakini kuisikia JF sijawahi ila naweza kuisikia mara moja kwa miezi miwili kupita

2.michango,majadiliano,na hoja ndani ya JF, kila nikifuatilia michango na hoja za watu mbalimbali humu ndani huwa nahisi kuwa hawa watu ni wa familia moja,ni kikundi cha watu,au wanafahamiana maana asilimia kubwa maongezi yao kama yanafanana ivi na kila nikisoma baadhi ya hoja na comments huwa naishia kustaajabu na kufurahia saana maana watu wa humu kidogo wamejaariwa kauli

3.misamiati inayotumika;kuna baadhi ya misamiati huwa naisikia humu tu kwenye majukwaa mbalimbali ya JF na haijakuwepo kwenye social network zingine kama vile watu wa lumumba,buku saba na mengine mengi ambayo yamepata kibali mbele ya jf na si mitandao mingine

4.watu wa mtaani na simu zao;kuna watu wengi sana ambao nipo karibu nao au nawaona barabarani,kwenye daladala na maeneo mengi sijawahi kuwaona wakisoma habari yoyote kwenye app ya JF ila utawakuta fb,insta,whatsapp na mitandao mingine ila siwaoni JF, lakini pia hata nikipekua simu zao ili nione app walizonazo sijawahi kuona app ya JF na inafikia kipindi nawafundisha na kuwasaidia kuinstall app ya JF na kisaikolojia ukiwaangalia watu wengi wanaonekana kutoijua vizuri app hii ambayo pia watu wengi wanaonekana kuitumia

Sasa hao wanaoitumia wako wapi?

5.baadhi ya hoja zinazotolewa/kuanzishwa na watu humu ndani:KUNA BAADHI YA HOJA HUMU HUWA ZINAANZISHWA NI HOJA AMBAZO SI ZA KAWAIDA YAANI INAONEKANA MTU ALIYEIANDIKA ANA AKILI ZA JUU SANA YAANI KILA UKIANZA KUISOMA UTAONA KUWA ENDAPO HUYU MTU ANGEKUWA KIONGOZI ANGEISAIDIA NCHI PAKUBWA SANA ILA UKIJA KATIKA MAZINGIRA YA KAWAIDA HUWAONI WATU WENYE HOJA KAMA HIZO KWENYE MITANDAO KAMA YA WHATSAPP HUKO NA KATIKA MAZINGIRA YA KAWAIDA
SASA HAWA WATU WAKO WAPI WAJITOKEZE HADHARANI NA WATOE MICHANGO ILI KUSUDI WAHUSIKA WANAOKUSUDIWA NA HOJA HIZO WAJIREKEBISHE NA KUFUATA USHAURI WENU KULIKO KUJIFICHA HUKU JF??

Nina vielelezo vingi sana ambavyo vinanifanya mimi niwe wa tofauti humu ndani

Kwani mara nyingi huwa naishia kusoma tu comment za watu kwani sijajua type ya watu wa humu sijui mkoje yaani utafikiri hampo kwenye nchi yenu ni wakati sasa wa wanaJF kujulikana kuwa nanyie mpo kwenye mazingira yetu maana inaonekana mtu akiwa JF ni mtu tofauti na mimi

Haya ahsante na maandalizi mema ya sikukuu yetu ya muungano wa zanzibar na Tanganyika tarehe 26april
 
Umesomeka...vzr sn.ukweli tafiti zako uko sahihi.watu walio jf ni watu wa makamo,elimu ya juu,upeo mkubwa, busara nyingiii.pia wana jf ashindwi kujitokeza ktk jamii,ila wasiwasi wangu WANAWAOGOPA WATU WASIO JULIKANA.
hahahah mi simoo we fukunyua tuu.
 
When you choose to be anonymous, its only right that you remain anonymous everywhere especially in public.

When your ID is verified, it means you have chosen to expose yourself and you have no worries discussing JF anywhere, or using the app lets say in a bus.
 
Nimefurahi Sana aiseee, hii Mada Kali Sana. Mwezi uliopita nilinunua Fulana ya JF, cha kushangaza nilipokwenda nayo mtaani na ofisini kila mtu alikua ananiangalia kwa Jicho la tofauti.

Huu ni mwaka wangu wa kumi (10), Nimekutana na Marafiki wengi Sana, very friendly Sana tu

Humu ndani wako akina Prof Tibaijuka, Mwapachu, mawaziri wenye akili na wasio na akili, wapo wapenda ngono, na tuna jukwaa letu kabisa la mambo ya Kikubwa, Yaani kuna Memba huwezi mkuta Popote pale zaidi ya jukwaa la mambo ya Kikubwa. Kuna jukwaa la Biashara, Ujasiriamali huko nako kuna fursa za kufa mtu, Ukitaka zile networking business Haya, bitcoin, Rifaro, Qnet, na akina Nani Yule wa Jangid Plaza, wapo.
Kwa kifupi Jf ina content zote Z Ukifika jukwaa la Afya, utashangaa watu wanabishana kuhusu uwepo wa AIDS Yaani ni facts tu. Unatamani au ukajilaumu Kwanini Ile mambo unaigonga kwa mpira wakati iko safe!

Njoo kwenye Siasa, kuna vilaza wakila aina, hadi watu wamebatizwa majina.

Ukianza kuandika kuhusu JF hutakaa uimalize
 
Hhahaha hatari sana boss naona hapo kwenye AIDS unamzungumzia mtu mzima deception
 
Mada nzuri sana kiongozi.

Ulivyojielezea tu na ulivyoshusha mawazo yako, unaonekana muelewa wa mambo.

Ili uifaidi JF na mada zake zitolewazo na michango (comments )ya wadau; ni lazima uwe CRITICAL THINKER.

Home of Great Thinkers ni tofauti na tarajia mambo tofauti na yale ya Fb, Insta, badoo n.k.

Ila kwenye watu hawakosi binadamu, na walipo binadamu hapakosi watu.
Hivyo; wapo wenye tabia za fb, insta n.k.
 
  • Thanks
Reactions: a45
Tatizo kubwa la JF ni wachoyo sana wa likes, ukiona mtu kapewa likes 80 kwa posti moja ujue ametoa Pointi nzito sana, kwa hiyo kama umezoea likes nyingi ni bora uchukue tumizigo twako ufungashe uondoke
 
Like za nini boss kama shida yako imetatuliwa
 
Wakishanunua magari,na kumiliki majumba kama wana jeifu walioko huku basi wataijua tu automatically
 
Nimefurahi Sana aiseee, hii Mada Kali Sana. Mwezi uliopita nilinunua Fulana ya JF, cha kushangaza nilipokwenda nayo mtaani na ofisini kila mtu alikua ananiangalia kwa Jicho la tofauti.

Huu ni mwaka wangu wa kumi (10), Nimekutana na Marafiki wengi Sana, very friendly Sana tu

Humu ndani wako akina Prof Tibaijuka, Mwapachu, mawaziri wenye akili na wasio na akili, wapo wapenda ngono, na tuna jukwaa letu kabisa la mambo ya Kikubwa, Yaani kuna Memba huwezi mkuta Popote pale zaidi ya jukwaa la mambo ya Kikubwa. Kuna jukwaa la Biashara, Ujasiriamali huko nako kuna fursa za kufa mtu, Ukitaka zile networking business Haya, bitcoin, Rifaro, Qnet, na akina Nani Yule wa Jangid Plaza, wapo.
Kwa kifupi Jf ina content zote Z Ukifika jukwaa la Afya, utashangaa watu wanabishana kuhusu uwepo wa AIDS Yaani ni facts tu. Unatamani au ukajilaumu Kwanini Ile mambo unaigonga kwa mpira wakati iko safe!

Njoo kwenye Siasa, kuna vilaza wakila aina, hadi watu wamebatizwa majina.

Ukianza kuandika kuhusu JF hutakaa uimalize
kabisa mkuu, ukija kwenye gambling kuna experts wanajitolea kumfilisi muhindi utadhan wana undugu na wabetiji wakina Pdidy DeepPond etc
ukipigwa tungule mtafute mtaalam Mshana Jr
Fix na story za uongo utazipata kwa GuDume
pia Jf haiko nyuma sababu tuna mpaka wagonjwa wa akili wakina Deogratius Kisandu

hekoo JF
 
Mkuu kitaan wananiheshim coz kichwan nipo smart n they group me mipngoni mwa wenye Akili mno

Nikija JF sometimes naogopa Ku comment au kuleta Uzi nikijua kwa great thinkers waliomo humu ninawwleza kia nimeandika upupu kihuni utumbo

Watu wa humu bana uki comment tus wanakujibu kistaarabu na kujioma ujinga uko comment ustaarabu wanaeza jibu tusi

Any way JF ni home of great thinkers
 
Uwe makini sana na post zako mkuu maana humu watu ukipost tu wanafanya saving for future uses

Wapo vizur sna kufatilia mtu kuliko hata hao usalama wa taifa

Na hawachelewi kufukua makaburi

Anyway karibu jf ndugu ujionee utamu uliojificha ambao wengi wanaukosa
 
Back
Top Bottom