Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 661
- 1,005
Serikali iliahidi kuanzisha bima ya afya kwa wote ndani ya siku mia moja ya awamu ya sita.
Mwanzoni mwa mwaka huu nilisikia kwamba zoezi hilo limeanza kwa makundi maalumu na kaya masikini.
Hata hivyo mpaka sasa sijawahi kuona watu hao wakiandikishwa na kupatiwa bima.
Hata sisikii elimu na matangazo yakitolewa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kujiandikisha na kupatiwa bima.
Kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii bado tunashuhudia baadhi ya watanzania wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali wakiomba kuchangiwa pesa ili waweze kwenda hospital kupata matibabu.
Huwa najiuliza kwa nini hawa wachache wanaoomba kuchangikiwa wasiwe wa kwanza kupatiwa hiyo bima ya kwa wote badala ya kusubiri michango?
Au ni bima kwa wote tulidanganywa tu, ipo kweli?
Je wewe mtaani kwako zoezi hilo limeanza?