Najaribiwa jamani

Najaribiwa jamani

LWENYI

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
1,839
Reaction score
2,173
Habari wana MMU,

Ni mara yangu ya kwanza kuanzisha uzi hapa ingawa ni msomaji mzuri sana wa mada mbali mbali za jukwaa hili kwa muda mrefu, leo naombeni na mimi mnishauri kwa haya yanayonitokea. Ni hivi, kuna sehemu nimepanga wakati nimefika hali ilikua shwari wapangaji wote walikua wa kiume kwahiyo kila mtu alikua akija na project zake from outside vivyo hivyo na mimi pia. Miezi kadhaa baadae wakaja wapangaji wa kike na ndipo vitimbi vilipoanza.

Kuna mdada alikuja akanipenda from day one akataka niwe rafiki yake ila akisisitiza ana mtu wake na mimi sikuona tatizo nikawa naye jirani akiniomba ushauri na kuonyesha care za juu sana kwangu ila sikutaka kutia shaka. Tukakaa muda akiniletea zawadi za hapa na pale na mimi nilizipokea kwa moyo wa amani sana.

Miezi kadhaa baadae akaniita room kwake nikakuta analia sana akanieleza kuwa boyfriand wake kamuacha na hataki tena wanaume ila mimi siyo wa wasichana sana na toka aje hajawahi kuona nimeleta msichana chumbani kwangu. Akanililia pale nikamfariji yakapita. Siku kadhaa baadae akaja na boyfriand mpya ingawa akaniambia anataka amsahau yule wa kwanza kwa kupata kipya nikasema kazi kwako.

Miezi kadhaa wakaachana ndipo alipoanza kuonyesha dalili flani kwangu za ndani kidogo ila mimi sikutaka kutupa ndoana yangu kabisa, kuna mpangaji mwenzangu akaanza kummendea msichana akaja akanipa stori nzima na mimi kama kawa nikamwambia kazi kwako. Akawa anakaa na yule jamaa huku akiniongelea mimi stori ni nyingi sana.

Sasa mada kuu ni hii ya siku za karibuni alisafiri kidogo wakati anarudi akakuta nipo, yule mpangaji mwenzangu akampokea lakini swali la kwanza ilikua ni mimi niko wapi? Akaambiwa nipo ndani akafikisha mizigo kwake na dakika chache akaja na zawadi mkononi na lawama za kwanini sitaki kumpokea.

Nikajitetea sikusikia kama umefika akasema najua hunipendi ila mimi nitajipendekeza tu hata iweje nikaona hapa kuna kitu ila sikuwa tayari kuwa naahisiano na yeye. Tumekaa kidogo akaja na rafiki zake wawili wakawa wanaishi wote cha ajabu wote wakanipenda bure nikachukulia poa pia sasa sikuwa na mpango wa kuwa na msichana pale.

Sasa wiki kadhaa zilizopita waliniita room kwao yeye akawa mzungumzaji mkuu na lawama zilikua ni kwamba mimi najifanya kipofu sioni alinipenda since day one na sikuonyesha kutaka kutake over na hawezi kuishi bila mimi kwahiyo wenzake wamsaidie nilisema ok nilifanyia kazi swala hili. Cha ajabu kesho yake room mate wake kaja kanichana live kuwa yeye pia ananipenda kwahiyo kazi kwangu kuchambua mchele.

Yule wa tatu naye ananiita majina ya kiuchokozi na sijajua nia yake nini, sasa kupunguza aibu nikaita yule wa zamani nikamgegeda, sasa mapenzi yamekolea balaa vitimbi vinaanza asipokuwepo yule aliyenichanaga anakuja na mitego ya ajabu sanaa na nakaribia kushindwa kuvumilia. Mbaya zaidi naanza kuona kutokuelewana baina yao wote watatu wanazozana siyo kama zamani na wote wanapenda kushinda na mimi.

Nishaurini wakuu nifanyaje?
 
Me nkajua shetwani anakukaribu kumbe unaadithia yaliyopo online Message sent
 
Kabla ya yote naomba majibu ya maswali haya
je wewe ni handsome au unavijihela?
je wewe ni uhai?
je hii story ni ya kweli au umetunga?
 
Kazi ni kwako...

Kila la kheri.......
 
Aaaah wanakujaribu, Sasa sikia weka mfupa wa nguruwe hapo mlangoni kwako utaona kama watakusumbua tena
 
kabla ya yote naomba majibu ya maswali haya
je wewe ni handsome au unavijihela?
je wewe ni uhai?
je hii story ni ya kweli au umetunga?

Wote wananiambia mm hb, mrefu & decent

Hela sina mkuu nnazo za kula tu

Hii ni kweli kbs tena sujaweka detail nyingi maana ningekua na hadithi ndefu sana aysee
 
Kuna riwaya fulani ya mtunzi IRENE MWAMFUPE,nimesahau jina tu nikikumbuka nitakuambia,isome vizuri sana maana inafanana kila kitu na mkasa wako
 
Kuna riwaya fulani ya mtunzi IRENE MWAMFUPE,nimesahau jina tu nikikumbuka nitakuambia,isome vizuri sana maana inafanana kila kitu na mkasa wako

Sawa mkuu yaweza kunipa funzo
 
Wanafunzi ndivyo walivyo hivyo usipoangalia utapiga wodi zima ya hostel....
 
Back
Top Bottom