Naitwa...

Mpevu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,805
173
Wanajamvi,
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipatwa na hali ya mshangao kwa raia wenzetu wa Tanzania hususan wale aidha wapo serikalini, ama wameshastaafu au ni watumishi wa umma (wabunge, madiwani, wenyeviti wa siasa wa mikoa kivyama) kwa majina ya 'mheshimiwa'. Leo nimekutana na jaji mmoja mstaafu na wakati nachukua mawasiliano yake nikamuuliza niweke jina gani ili iniwie rahisi kimawasiliano? Akasema 'andika mheshimiwa 123', nikareudia kumuuliza kana kwamba sijasikia vizuri...nae akarejea tena kwa msisitizo kuwa andika 'mheshimiwa123'. Nimejiuliza pasipo majibu kwa yafuatayo:-
  1. Je 'mheshimiwa' imekuwa ni ibada?
  2. Je 'mheshimiwa' ni cheo ktk jamii?
  3. Je usipotanguliza neno 'mheshimiwa'...umemdharau? umemkosea heshima?
  4. Maneno your excellence, honorable, respected etc....je yanatumikaje ktk jamii ili kutenganisha viongozi wakuu wa nchi, viongozi ktk jamii na viongozi wa kidini...ktk kuonyesha kuwaheshimu ni neno lipi kihadhi linastahili ili kuwapa hadi yao ya kidunia?
Naomba niwasilishe na tueleweshane kiuungwana.
 
Back
Top Bottom