Naitazama UKAWA kama "Safina", Lowassa kama "Nuhu"

Naitazama UKAWA kama "Safina", Lowassa kama "Nuhu"

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,623
Reaction score
164,679
Uchaguzi mkuu wa Oktoba utakuwa ni kama "gharika" mithili ya gharika iliyotokea enzi za Nuhu hivyo wanasiasa wengi wa chama tawala wanajaribu kuingia ndani ya safina(Ukawa) ili kuepuka dhoruba hiyo ambapo Lowassa kama ilivyokuwa kwa Nuhu, ndio mwenye jukumu la kuingiza wana-CCM wake kwa waume ndani ya Safina hiyo kabla ya kufunga milango ya Safina Oktoba 25.

Ukawa ni Safina wanasiasa ingieni kuepuka dhoruba ya Oktoba 25.

Ole wenu nyote mtakaokuwa nje ya Safina hii pale gharika kuu itakapotua kwani mtalia na kusaga meno.
 
ninaanda mbwa wangu nitamweka dirishani na mlangoni achunge wale mamuluki wanaweza kulitoboa safina safari ikaishia njiani.
 
mtu mchafu na mwenye tamaa kama lowasa umlinganishe na Nuhu?! Waumwa bila shaka
 
Huyu fisadi mfananishe na mafisadi wenzake siyo mtu mwingine hata kidogo.
 
Huu umati wa watu leooooo mmmhhh bt nabakisha maneno maana wakati wa lyatonga nlishuhudia akibebwa sitaki kujiaminisha sn kuwa nchi inaenda kwa ukawa.All is all tubaki na amani tu tujenge taifa hata kama mabadiliko yatatokea.
 
watanzania wote tuwahi kuingia kwenye safina kabla milango haijafungwa
 
masikini rais wetu wa mioyoni'' mbowe wewe ni mubayaa! yaani umemtosa rais wetu wa moyoni!
ulituaminisha kuwa 2010 alishinda kumbe ulikuwa unatuhadaa. na sasa umedhirisha kuwa hakushinda na wala asingeshida ndo maana umemtosa. ama kweli mbowe wewe ni mubaya. masiki rais wetu wa mioyo! inaniuma sana nikifikiria nalia!
 
Yaani mnaonyesha hadi jazba zenu kwenye maandishi!Kweli CCM mmetota..
 
kweli hiyo ni safina ya watu wengi sasa vipi kuhusu ndugu yetu LIPUMBA Kujiondoa ndani ya safina hapo tutegemee nini hapo baadae? swali kwenu jamani.
 
kweli hiyo ni safina ya watu wengi sasa vipi kuhusu ndugu yetu LIPUMBA Kujiondoa ndani ya safina hapo tutegemee nini hapo baadae? swali kwenu jamani.

Lipumba atarudi tu huyo baada ya UKAWA kupitia Chadema, ataomba radhi na kurejea kama mwanachama wa kawaida sana ndani ya chama cha CUF.
 
mtu mchafu na mwenye tamaa kama lowasa umlinganishe na Nuhu?! Waumwa bila shaka

Hakika mwaka wa miujiza....ni mwaka 2015.

CCM mlizoea kudanganya...kwa miaka 54..sasa mwisho umefika....

vipofu wanaona.....

viziwi wanasikia....

viwete wanatembea....

wajinga na wapumbavu wooote wamekuwa werevu..kila mtu atapiga kura...


mwaka huu hata washirikina wataandamana kupiga kura za haki.

Hakika...Tanzania inazaliwa upya...asie amini asubiri october 25.

MUNGU IBARIKI TANZANIA...



MUNGU MBARIKI LOWASSA.....
 
masikini rais wetu wa mioyoni'' mbowe wewe ni mubayaa! Yaani umemtosa rais wetu wa moyoni!
ulituaminisha kuwa 2010 alishinda kumbe ulikuwa unatuhadaa. Na sasa umedhirisha kuwa hakushinda na wala asingeshida ndo maana umemtosa. Ama kweli mbowe wewe ni mubaya. Masiki rais wetu wa mioyo! Inaniuma sana nikifikiria nalia!
we toa hadi kamasi.... No one have time for that.... Mabadiliko ndicho kilicho moyoni mwa weng
 
Back
Top Bottom