Naitaji share holder

Naitaji share holder

ruhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
5,035
Reaction score
8,075
Habari za asubuhi wana JF!

Nilimaliza shahada ya kwanza ya Uhandishi wa Umeme mwaka 2013, ninayo wazo na dhamira ya kufungua kampuni ya Electrical Installation kama class seven siyo mbaya.

Naomba mwenye dhamira na wazo kama yangu tushirikiane kuanzisha hiyo kampuni, naomba awe na taaluma ya Umeme.

Kufikiria kumaliza kazi ya watu kwa ufanisi bila kujua umeongeza fedha kiasi gani kinachosha kweli.

Kwa mawasiliano 0764727925 niko G/MBOTO Dar es salaam.
 
Brother, a word of advice. Sidhani kama hii ni njia nzuri ya kutafuta business partner. I can assure you kutafuta mke ni rahisi sana kuliko kutafuta business partner.

Najua kuna watu unawafahamu kwa muda mrefu na huko nao kwenye hio fani. Hao ndio your first potential business partners, tafuta mtu ambae mtakaa chini mtaweza kuzungumza kwa lugha moja. Kama hakuna mwenye hio nia, anza kwanza kwa kubadilisha fikra zao.

Its just my advice. You hav option to take it or leave
 
Ahahaha...dogo anatafuta business partner kama anatafuta demu kona baa. ahahahha...hiyo ni kazi ngumu sana kuliko hata kutafuta rais wa tanzania.

Umemaliza chuo jana kwanini unataka kuanzisha company ya umeme ya ukandarasi?....kazi utapata wapi?...unayo network ya kazi?...mtaji wako ni nini hasa ili umvutie huyo partner kukujoin?.....angalia dogo usikute una tester na screw drive ukaona unaweza ku-run electrical company....bado sana.

Ushauri wangu kama kaka mkuu.

1- Endelea kufanya kazi kwa waajiri wako ili ukuze uzoefu na client base yako ikuwe.

2- Tunza kiasi unachokipata na kusajili kampuni yako kwanza

3- Anza kuomba kazi toka kwa clients uliowahi kufanya nao kazi kupitia waajiri wako ukiwaambia umeanzisha kijikampuni chako wakusaidie kazi kikuwe.

4- Kusanya msingi wa kutosha kununua kazi moja ya kutokea kisha ukishapata kazi moja hiyo jienguwe kwenye ajira ya maboss wako.

5- Serious partner atatoka huko utakakokuwa unafanya kazi na wenzako au ma-clients waliofanya kazi na wewe.

Kama unaona ushauri wangu unafaa niambie nijuwe nimechangia kubadilisha maisha ya kijana mmoja wa kitanzania, ila kama unaona haufai pia nijulishe nijuwe nimemuharibia maisha kijana mmoja wa kitanzania ili jumapili niwahi kanisani kufanya sala ya toba.

Ni hayo tu.
 
Mawazo yako yamemjenga kijana hata kama hajasema.
 
Back
Top Bottom