Naitafsiri kama ni rushwa

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Habari wanajamvi.

Rushwa ni adui wa haki! Hii zamani ilikuwa ni ahadi ya Mwana TANU lakini kwa bahati mbaya haikurithiwa na wana CCM.

Juzi tumeona tausi lukuki wakitolewa kwa Marais wastaafu kama zawadi. Kwangu mimi ile ni rushwa tena first class. Nitafafanua.

Kwangu mimi ile ni rushwa kwasababu siku chache zijazo vikao vya maamzi makubwa ndani ya chama cha mapinduzi, CCM vitaanza. Jamaa akisoma alama za nyakati anaona dalili mbaya upande wake hasa kuhusu mambo mawili au matatu.

Mosi, ni kuhusu hatima ya Bernard Membe, jambo lile si jepesi kisiasa.

Pili, ni kuhusu Makamu Mwenyekiti wake kuwekewa viuatilifu wakati wa vikao vyao vya ndani.

Sasa kulikuwa na haja kubwa sana kuwaleta pamoja viongozi wastaafu ili walau apate kuungwa mkono na watu maarufu ndani ya chama. Hii ni rushwa of its own kind.

Zawadi zozote mwaka wa uchaguzi kutoka kwa wanasiasa ni RUSHWA. Wale tausi ni rushwa!
 
Hivi TAKUKURU wanaweza kumwanzishia uchunguzi, maana naona umetufungua macho hapa
Ingekuwa TAKUKURU wabajitambua wangeweza kuanzisha uchunguzi ili kuona ni nani amelianzisha wazo lile la kutoa zawadi ya tausi. Kama yeye ndio mwanzilishi inakuwa ni Rushwa tu ili wawe upande wake wakati wa vikao muhimu vya maamuzi vya chama.
 
Watu mnapenda kuwa negative kila kitu. Wale tausi wapo wengi sana ikulu,tausi 2260 si mchezo, kuwa marais wastaafu inaweza ikawa ni njia ya kuwapunguza pale ikulu.
 
Watu mnapenda kuwa negative kila kitu,wale tausi wapo wengi sana ikulu,tausi 2260 si mchezo,kuwa marais wastaafu inaweza ikawa ni njia ya kuwapunguza pale ikulu
Tatizo siyo kuwa tausi wapo Wengi ila nani kaamua kuwatoa na muda gani? Wamegawana Mali ya umma.
 
Back
Top Bottom