Naisusa Halotel na huduma yao ya Halopesa

successiful dreamer

Senior Member
Sep 10, 2019
103
189
Kampuni ya simu ya Halotel nimegundua kuwa ndiyo kampuni ya hovyo kabisa katika maswala ya miamala. Jana nilikosea kutuma pesa ikaenda kusikotakiwa.

Nilijaribu kuwasiliana na huduma kwa wateja mara tu baada ya kugundua kuwa nimekosea kutuma pesa lakini sikufanikiwa kuongea na mhudumu yeyote japokuwa simu iliita kwa muda wa dakika tano na nusu, leo pia nimepiga namba ya huduma kwa wateja bila mafanikio. Nilijaribu kumpigia aliyepokea hiyo pesa kimakosa akaniita tapeli wa kiwango cha lami na akagoma kuirudisha hiyo pesa.

Nimekaa nikajiuliza maswali mengi je ni kweli kampuni ya halotel ina watu wa customer service? Kama wapo kazi yao ni ipi? Je wanajisikiaje kuacha kupokea simu za wateja wakati kazi yao ni kusikiliza na kutatua kero za wateja?

Huduma yao ya internet pia imekuwa ya kusuasua kwa hapa Moshi mjini baadhi ya maeneo huduma za internet ukiwa na line ya halotel huwezi kuipata. Naona bora niwakimbie na nijiunge rasmi na TTCL kwa ajili ya internet, huduma za miamala nitaangalia mtandao upi kati ya M-pesa au Tigo pesa nitumie. Halotel wameniboa vya kutosha.
 
Hao halotel mi nilikwangua vocha vibaya namba moja ikawa haionekani vizuri.
nimewapigia wana niambia hawana Hiyo huduma ya kujua namba hiyo ni ipi wakaniambia niitupe tu vocha.
 
Back
Top Bottom