REAGAN C.MABOGO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 1,269
- 1,007
Mtakumbuka mauaji ya halaiki (massacre) yaliyotokea mwaka 2001 huko Zanzibar.Wahanga wa mauaji hayo ya kinyama walikuwa ni wafuasi wa CUF. Harakati hizo za mauaji ziliambatana na msako mkali majumbani mwa watu ambapo waliwatoa wafuasi wa CUF na kuwatesa kwa vipigo na kuwafunga magerezani!
Namna iliyotumika kuwatambua wafuasi wa CUF ni kasumba ya ubaguzi wa rangi, ambapo imekuwapo kasumba ya kwamba watu wenye mchanganyiko wa damu ya kiafrika na kiarabu ndiyo wanachama ama wafuasi wa CUF.Kwa hiyo watu hao mchangayiko wa damu, maarufu kama machotara ndiyo walioandamwa na msako wa askari waliotumwa na Benjamin William Mkapa, amiri jeshi mkuu wakati huo.
Nimekuwa nikijiuliza: nani kailoga ICC mpaka ikashindwa kuyaona mauaji na mateso waliyoyapata Wazanzibar?! Wakati haikuchukua muda kuyaona yaliyotokea Darfur, Sudan, na Kenya baada ya uchaguzi. ICC ilihitaji mabadiliko hata kabla ya Fatou Bensouda! Louis Moreno Ocampo alikuwa na ajenda yake kuyafumbia macho mauaji na mateso ya kinyama waliyofanyiwa wazanzibar.!