Tanzania raha sana ila mauaji na mateso wakati wa uchaguzi yanatuharibia aina ya maisha yetu

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Wacheni masihara Tanzania kama Tanzania ina maisha ya raha yaliyojaa undugu baina ya watu wa rika mbalimbali, matajiri na masikini alie na kazi na asie na kazi, kwa kweli tumeridhika na hali zetu kama nchi na raia wake.

Tulizoea uchaguzi kama moja ya starehe za ndani ya nchi kwa miaka kumi au zaidi iliyopita, leo hii unapokaribia uchaguzi raia huingiwa na hofu na furaha yao kutoweka wakiwa na wasiwasi wa kuvuka salama ndani ya kipindi cha uchaguzi.

Sera nzuri au mbaya walala hoi hata haziwashughulishi wao wana kazi zao na wanasiasa nao ni kazi zao wakiwemo wajumbe! Husubiri siku ya kupiga kura, uchaguzi ulikuwa kama mechi za mipira washabiki wengi japo kucheza mpira hawaelewi na ndio ulivyo uchaguzi, masihara na mizaha baina ya wafuasi wa vyama ilikuwepo na walishindana kwenye vibaraza bila ya kuingiana mwilini, na ulipofika siku ya uchaguzi walienda kupiga kura na kusubiri matokeo, na akitangazwa alieshinda stori zimekwisha.

Leo uchaguzi umekwisha bado watu wanafariki kutokana na mateso na vipigo waliyoyapata, kitu gani kimetufikisha hapa?
 
Mwaka gani uchaguzi ulifanyika na hapakuwa na "skendo" za kishamba kama hizo??
Your just typing as if there is children here, shame on you

Punguza kulamba miguu
 
Wacheni masihara Tanzania kama Tanzania ina maisha ya raha yaliyojaa undugu baina ya watu wa rika mbalimbali, matajiri na masikini alie na kazi na asie na kazi, kwa kweli tumeridhika na hali zetu kama nchi na raia wake.

Tulizoea uchaguzi kama moja ya starehe za ndani ya nchi kwa miaka kumi au zaidi iliyopita, leo hii unapokaribia uchaguzi raia huingiwa na hofu na furaha yao kutoweka wakiwa na wasiwasi wa kuvuka salama ndani ya kipindi cha uchaguzi.

Sera nzuri au mbaya walala hoi hata haziwashughulishi wao wana kazi zao na wanasiasa nao ni kazi zao wakiwemo wajumbe! Husubiri siku ya kupiga kura, uchaguzi ulikuwa kama mechi za mipira washabiki wengi japo kucheza mpira hawaelewi na ndio ulivyo uchaguzi, masihara na mizaha baina ya wafuasi wa vyama ilikuwepo na walishindana kwenye vibaraza bila ya kuingiana mwilini, na ulipofika siku ya uchaguzi walienda kupiga kura na kusubiri matokeo, na akitangazwa alieshinda stori zimekwisha.

Leo uchaguzi umekwisha bado watu wanafariki kutokana na mateso na vipigo waliyoyapata, kitu gani kimetufikisha hapa?
Utawala mbovu wa CCM umetufikisha hapa
 
Back
Top Bottom