Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,427
Kenya kuna wachumi nje na ndani ya serikali. Lakini tatizo ni kuwa wanasiasa ndio wanaoamua ni kitu gani kitakachowekwa kwenye budget na gani hakitawekwa. Kwa mfano hio SGR waliofanya uamuzi wa kuijenga ni wanasiasa. Wachumi walifanya economic feasibility study ili kuchunguza ikiwa hio SGR italeta mapato ya kutosha katika life-time ya hio project. Kazi ya mchumi ni kuadvice. Kwa hivyo ikiwa Ndii ametoa advice kwamba mradi fulani ni mbaya lakini serikali ikampuuza basi hakuna atakachoweza kufanya zaidi ya hapo. Halafu kuna Wachumi wasiozingatia walichofunzwa. Kwa mfano Henry Rotich aliyekuwa Waziri wa fedha ana masters ya economics from University of Nairobi ila yeye ndiye alikuwa mstari wa mbele kuenda nje ya nchi kuchukua madeni ya Eurobond 1 and 2. Yeye ndiye aliyeongeza debt to Gdp ratio ya Kenya kwa kiasi kikubwa. Ilikuwa ni jukumu lake kama mchumi kumweleza rais kuwa sio vyema Kenya kuomba deni zaidi ya kiwango fulani. Kwa mfano angetoa proposal ya kupunguza expenses ya serikali. Kwa mfano hakuna haja ya wanasiasa na majaji kuendesha mercedes benz. Wapewe VW Passat ambayo hainywi mafuta mengi. Watafute njia zingine za kupunguza public expenses ikiwemo kutumia PPP. Miradi kama Nairobi expressway ambayo ni PPP inasaidia serikali kutoomba deni kwa sasa, kwa sababu private investor ndiye anayeshugulikia ujenzi huo.Tatizo sio kusoma darasani, muhimu ni kuelewa na kuinyambulisha. Tony254 kuwa mkweli, kwa mambo na maamuzi yanayofanywa na GoK, kuanzia katika miradi ya nchi, kukopa, kuendesha serikali kwa gharama kubwa, uzalishaji wa chakula na gharama kubwa za kufanya uchaguzi, kweli unaweza kuamini kweli Kenya kuna wachumi?, kumbuka haya yote David Ndii amekua akiyapigia kelele " Economically"