Naipongeza rasmi UKAWA mpaka hapa ilipofikia

H.T.P

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
1,169
Reaction score
1,298
Kwakweli kwa mtanzania anayefikiri kwa kina ataungana na mimi kwamba, pamoja na hujuma na figisufigisu nyingi zilizofanyika ambazo ziko wazi japo ukweli hausemwagi Tanzania, UKAWA kwakweli wameimarisha upinzani.

Ninachokiona mimi ni CCM kuwa chama cha kawaida cha upinzani siku za usoni.. Sasa hii itawezekanaje? Twende pamoja nitoe yangu ya moyoni

1. Niwakati sasa wakutambua kwamba kwakuunganisha nguvu ndo dawa pekee itakayosaidia kummaliza mtawala CCM. Kwa hili naomba niseme viongozi wa UKAWA zitambueni fitna zinazotimiwa na CCM kuwachonganisha na kuwagawa, naomba muwe werevu muwazidi akili zaidi shikamaneni.

2. Hakikisheni mnapigania kwa udi na uvumba kupatikana kwa katiba mpya yenye dira na muelekeo sahihi, itakayoweza kusema fulani kashinda mpeni haki yake,

3. Jikiteni Sasa kutoa elimu vijijini ambao wengin kwasababu hawazijui changamoto kali za maisha na wengine wakiamini kuwa CCM ni ile ile ya nyerere y ujamaa basi wa
naipa kura tu,

4. Dumisheni Democrasia kwa vyama vyote vya "UKAWA" viwe na haki sawa ya kutangazwa na kuimarishwa,

5. Tofauti na chama tawala nyie wekeni uwazi wa kila kitu kinachofanyika ili kuongeza imani za wafuasi

6. La mwisho kwa sasa, dumisheni kwa pamoja na kwa uhalisia kumtegemea Mungu aliyeumba majira na nyakati.
 
Point kati ya 4 na 6 ndo sababu ya anguko kuu la UKAWA..point ya 5 (lack of transparency/uwazi) inaendelea kutafuna chadema! Reference is made to Viti Maalumu
 
wimboo

tunaisoma namba wewe vipi umeisoma ni ngapi
 
Point kati ya 4 na 6 ndo sababu ya anguko kuu la UKAWA..point ya 5 (lack of transparency/uwazi) inaendelea kutafuna chadema! Reference is made to Viti Maalumu

ndo maana tunasema waboreshe kuanzia sasa
 
Hakika ukawa pamoja na dhoruba zote walizopata bdo wanaendelea kuimarika.
 
demokrasia ingeanzia ktk uteuzi wa mgombea urais, uwazi tkt viti maalim, kulipa posho za mawakala, hapo ningewaunga mkono
 
Tukiacha unafiki huko kote democrasia ilikuwepo...walichoangalia ni mtu anayeweza kupambana na CCM sio mtu ni mtu tu..na matunda yameonekana duniani kote..tena kwa hili nawapongeza zaidi
 
kwahiyo b4 hajaja mamvi Chadema mlikua hamna wa kupambana na ccm?
 
Point kati ya 4 na 6 ndo sababu ya anguko kuu la UKAWA..point ya 5 (lack of transparency/uwazi) inaendelea kutafuna chadema! Reference is made to Viti Maalumu

Fafanua zaidi mkuu hasahasa ukizingatia hatua ya upigaji kura, ni kwa nini ilikuwa bayana kwamba UKAWA haina wakala?!
 
True big up ukawa endeleen kudumisha umoja huu msirud nyuma maana ccm inatafuta jinsi ya kusambaratisha umoja huu
Changamoto ni sehemu ya maisha na inatoa fundisho kuona wapi hapakuwa vizur ili kupaimarisha
 
Muunganiko wa vyama vinne ila bado hamuoni ndani kwa CCM, kweli CCM noma Na mtaendelea kuisoma namba
 
Siku Ccm ikisimama yenyewe bila kukingiwa kifua na DOLA ndipo haki itaposimama. Ref. Zanzibar unatamba wakati mnashindwa kukubali matokeo ?! Ajabu
 
Naomba mfanye kazi na zitto msimtenge,malizaneni tofauti zenu ,unganeni,zitto ungana na ukawa ,ujue ccm haina muda wa kumuachia mtu,madaraka,hivyo unganeni mupiganie tume huru ya uchaguzi
 
Kwakweli kwa mtanzania anayefikiri kwa kina ataungana na mimi kwamba, pamoja na hujuma na figisufigisu nyingi zilizofanyika ambazo ziko wazi japo ukweli hausemwagi Tanzania, UKAWA kwakweli wameimarisha upinzani.

Ninachokiona mimi ni CCM kuwa chama cha kawaida cha upinzani siku za usoni.. Sasa hii itawezekanaje? Twende pamoja nitoe yangu ya moyoni

1. Niwakati sasa wakutambua kwamba kwakuunganisha nguvu ndo dawa pekee itakayosaidia kummaliza mtawala CCM. Kwa hili naomba niseme viongozi wa UKAWA zitambueni fitna zinazotimiwa na CCM kuwachonganisha na kuwagawa, naomba muwe werevu muwazidi akili zaidi shikamaneni.

2. Hakikisheni mnapigania kwa udi na uvumba kupatikana kwa katiba mpya yenye dira na muelekeo sahihi, itakayoweza kusema fulani kashinda mpeni haki yake,

3. Jikiteni Sasa kutoa elimu vijijini ambao wengin kwasababu hawazijui changamoto kali za maisha na wengine wakiamini kuwa CCM ni ile ile ya nyerere y ujamaa basi wa
naipa kura tu,

4. Dumisheni Democrasia kwa vyama vyote vya "UKAWA" viwe na haki sawa ya kutangazwa na kuimarishwa,

5. Tofauti na chama tawala nyie wekeni uwazi wa kila kitu kinachofanyika ili kuongeza imani za wafuasi

6. La mwisho kwa sasa, dumisheni kwa pamoja na kwa uhalisia kumtegemea Mungu aliyeumba majira na nyakati.

Unaota?

Umesahau mgombea wa Urais wa ukawa kapatikana vipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom